Sky Walker kwa hili la Diamond na Davido umeonyesha udhaifu

Sky Walker kwa hili la Diamond na Davido umeonyesha udhaifu

Kwenye hili swala naona baadhi ya watanzania wakiwemo-Bong5.com, wameamua kumfanya mkosaji kuwa ndiye-aliekosewa na aliekosewa kuwa ndiye mkosaji. Huku ni kukosa uzalendo, lakini pia ni kiwango cha hali ya juu cha kuthamini wageni mpaka tukakubali kuwa mabwege!-

Nimejiuliza tu, hivi ingekuwa kauli ile "tata" (wamedanganya tena) kaisema Diamond dhidi ya Wanigeria, jee kweli kuna mnigeria au chombo cha habari cha nigeria kingemkingia kifua Diamond? SI dhani!

Nianze na-Bongo5.com.-Nilishangazwa sana na kukurupuka kuanza kuwa wakili wa Davido. Ni kweli HEKIMA ilihitajika kutafsiri kauli yake tata, LAKINI tafsiri yoyote ambayo mtu angeitumia kutafsiri tungo ile tata bado mtu huyo angebaki kuwa sahihi, mpaka tu pale mtoa kauli ile (Davido) atakapo toa tafsiri sahihi zaidi ya kauli ile. Mathalani nikisema "Juma kapanda mchungwa" Hii ni tungo tata, tafsiri yoyote utakayokuwa nayo ni sahihi. Yaani kama utafahamu kwamba Juma ka kwea mchungwa (kupanda juu ya mchungwa) au Juma kaotesha mchungwa,tafsiri zote hizo mbili zinabaki kuwa sahihi mpaka pale mimi mtoa kauli hiyo ntakapo bainisha ipi sio sahihi.

Bongo5.com-mkaja kwa pupa ile ile waloitumia watafsiri (Watanzania) wa kauli ya Davido, na nyie mkaja na uetetezi kwa Davido, huku uetetezi wenu ukiwa umejaa kauli za "kuwezekana (Possible")" ( 0.05 > P < 1). Huwezi kumwambia mwenzako hayuko sahihi kwa utetezi wa kauli ya " inawezekana"

Bongo5.com-ningewaona mna busara na wamaana pia katika swala hili kama mmngeandika makala kumlaumu Davido kwa kutokufafanua kauli yake mpaka leo hii. Yeye Davido akiwa kama msaniii anaeheshimika na Watanzania, ambao pamoja na umaskini wetu tumechangia katika utajiri wake, kwa kodi zetu analetwa hapa nchini, analipwa ma milioni ya fedha (mara kumi zaidi ya walipwavyo wasanii wetu), kwa kwa viingilio vyetu tunahudhuria matamasha yake kwa wingi. Hilo tu lilitosha kwake yeye Davido kuona umuhimu wa kufafanua kauli yake, ili kuondoa sintofahamu kama hakuwa na nia mbaya.

Bongo5.com-kwa chuki zenu, mmelalia upande wa Davido ambae kutokana na ukimya wake, tafsiri pekee yenye nguvu kwa sasa "Probable" (0.05 < P < 1) ni hiyo iliyotafsiriwa na Watanzania walowengi mpaka sasa. Kama Davido alikuwa na maana zaidi ya hiyo, basi ukimya wake unamaanisha "he does not care" watazania watachukuliaje.-Kwa maana watanzania si lolote si chochote kwake, "They (Tanzanians) are nothing". Ama kwa lugha ya mwambao anamanisha " watanzania "hawazimi hawawashi". Wakikasirika au wakifurahi hawana athari yoyote katika maisha ya muziki wake. Hii ni dharau, ni matusi makubwa zaidi.

Bongo5.com-mlitakiwa muingalie hali hii katika usawa (mkiweka uzalendo mbele). Badala ya kuanza kumuandama Diamond ili ajione kakosea, eti amuombe samahani Davido. Duh ubegwe wa kiasi gani huo, Hivi inamaana mtu akikusaidia ndio unakuwa mtumwa kwake? Hivi mtu akikusadia ndo anapewa kibali cha kusema atakacho juu yako kisa tu alikusadia? No way! Kila mtu katika fani yoyote alisaidiwa na alisadia kwa namna moja ama nyengine, na bado unae msaidia unatakiwa umpe heshima yake, wala huna kibali cha dharau juu yake.

Davido kweli alimsidia Diamondkwa kumfanya ajulikane huko Magaharibi mwa afrika, lakini ni sahihi pia Diamond nae alifamya Davido ajulikane zadi huku mashariki mwaAFRIKA hasa Tanzania (mimi binafsi si mpenzi wa Music wa nigeria na sikuwa namjua huyu jama kabisaaa, baada ya No 1 remix ndo nikaanza kumfatilia kazi zake, I hope wapo wengi kama mimi huku east africa). Zaidi, Davido hakufanya collabo bure, alilipwa, so kuna faidia ya kifedhai pia aliipata, pia nominations zilizotakana na nyimbo hiyo, ziliendelea kumueka Davido kwenye ramani ya muziki Afrika na duniania, hivyo basi mwisho wa siku ushirikiano wao ulikuwa na "mutual benefit" or "win-win collobaration" Si sahihi hata kidogo kumsimanga na ´kumuapiza Diamond.

Na nani hasa aliesema kwamba kwa Diamond kurudia kuandika "Ahsante Allah tumedanganya tena...." alimaanisha kumjibu Davido katika hali ya kumaanisha (kwamba alikuwa serious)! Kwanini tusiamue basi kutumia busara hiyo hiyo mnayotumia kumtetea Davido kwa kauli yake, basi tumtete Diamond kwamba pengine na yeye alikuwa ana "joke" (mzaha tu). Yaani aliandika sentensi hiyo katika hali ya kuendeleza mzaha uloanzishwa na rafiki yake. Ni mara ngapi tumeona Diamond akiandika mizaha (kufuraisha mashabiki zake) kwenye akaunti yake ya instagram na facebook! Kwani si juzi tu aliaomba asemehewe gharama za picha alizopiga studio flani, jee alimaanisha? Hapana ulikuwa mzaha tu!

Tuwe wazalendo na mapenzi na wasanii wetu. Tuachekujidhalilisha na kuwa mabwege hata kwa haki iliyoyetu. Davido kama ni muungwana na mstaarabu, na kama si "egotism" inayomsumbuwa basi anapaswa awaombe radhi Watanzania. Au atoe ufafanuzi wa kauli yake (alimaanisha nini), hapo ndo kama nikuombwa msamaha ataombwa kwa kutokueleweka! Kukaa kimya na kuendelea kuandika mafumbo, nimuendelezo wa DHARAU na MATUSI kwa watanzania. Diamond does not owe Davido an apology,HOWEVER, we (Tanzanians) are owed an apology by DAVIDO, unless he (DAVIDO) clarifed his ambiguous sentence into a plain and clear message!

Diamond kama kufika mbali atafika tu, who is Davido by the way? Iliandikwa tu na Mungu kwamba kupitia yeye (Davido) Diamond ajulikane huko West, lakini angeweza kuwa WIZKID, IYANYA au yoyote yule. Diamond kwa juhudi zake na kama bado Mungu amempangia aendelee kwenda juu atakwenda tu! Diamond bado ana Connection na wasanii kibao wanijeria, na nchi nyengine. Napia naamini iko siku watayamaliza na Davido (wao wenyewe) sio kwa kuandamwa na-Bongo5.com na wengine .

kaka kwanza hongera sana kwa kutumia mud a wako mrefu kuandika ili kuwaelimisha watanzania kwa upande nimekuelewa na I support u 100% I think hakuna haka ya kutoa more clarification
 
Back
Top Bottom