macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
VicentKatiba ya Tanzania, wabunge wanatumwa na chama, Dr. Slaa hawezi kumchukua mbunge wa CCM bila ya ridhaa ya CCM kwani chama chake kikimfukuza uanachama na ubunge anakuwa amepoteza
Naenda kwenye sanduku la kura nikiwa na akili moja kichwani. KUMTOKOMEZA MKOLONI mweusi aliyezikalia fikra, elimu na hatima zetu for more than 15 yrs. Nyerere hausiki na haya madudu yaoDictator,
Umati huu unaleta matumaini ya kweli. Sala yangu kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba CCM wakubali hali halisi. La sivyo, nchi yetu itaelekea pabaya.
Hivi washauri wa J.K. wanamwonesha picha hizi? Wanamthibitishia kwamba Chadema hawana mabasi na malori ya kuleta watu mikutanoni?
Ni dhahiri kwamba Watanzania wameichoka ccm, na wanataka mabadiliko. Mabadiliko ya kweli yatakuja tu pale kura zao za tarehe 31 Oktoba 2010 zitapigwa kwa uhuru na zitahesabiwa kwa haki.
Mungu Ibariki Tanzania. Amina.
Vicent
Kinachowaunganisha CCM sasa hivi ni ugawanaji wa ulaji tu. Ikitokea hiyo scenario ya Dr. Slaa kushinda na asipate wabunge wengi hilo halitaleta shida kama wengi wanavyofikiria kwani yule kingi wao atakuwa 'keshauawa' na wengine watasambaratikia mbali. Naomba tusisahau nguvu za kikatiba alizopewa rais wetu!
Katiba ya Tanzania, wabunge wanatumwa na chama, Dr. Slaa hawezi kumchukua mbunge wa CCM bila ya ridhaa ya CCM kwani chama chake kikimfukuza uanachama na ubunge anakuwa amepoteza
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?
Unajua kuna watu wako CCM na ni wazuri tu,tunachotaka ni mabadiliko tu pale juu (mjengoni).Hata akiunda serikali na CCM bado serikali ya Slaa itakuwa better off kuliko kama akija JK na familia yake tena! Ieleweke kwamba Uraisi wa nchi hii si suala la familia kama alivyotaka Kikwete tuelewe. Na kama kuna kitu anakosea sana ni kuihusisha familia yake kwenye kampeni kama vile Urais ni mradi wa familia.
Katiba ya Tanzania, wabunge wanatumwa na chama, Dr. Slaa hawezi kumchukua mbunge wa CCM bila ya ridhaa ya CCM kwani chama chake kikimfukuza uanachama na ubunge anakuwa amepoteza
Mmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?
kumbuka kuwa kuna watu wataisaliti CCM kama CHADEMA ikishika dola na interest za taifa ni juu zaidi ya chama! Hii CCM unaiona hivi kwa vile inashika dola ikiingia upinzani itafyata halafu hawataweza kuzua wabunge kama wanavyofanya sasa maana mbunge akisema anajivua uanachma maana yake uchaguzi mpya na sidhani kama watataka hilo! usiwe na wasi mkuuMmoja wa makada wa CCM niliyezungumza naye amekiri Dr Slaa anashinda ila hawezi kuunda Serikali kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kupitisha mswaada wowote. Sijui wapenzi wa Chadema kuunda Serikali bila idadi kubwa ya wabunge hiyo serikali itafika miaka 5 kweli?