Slaa awasha moto mwingine

Slaa awasha moto mwingine

Big up Dr Slaa cha msingi ni kuwa umeongea watekeleze wasitekeleze ni juu yao ni wanajifanya wengi wape!
Ipo siku kitaeleweka tuu.
Aluta continua mpaka kieleweke
 
Thanks Asha,nimpigiwa simu toka dodoma kwa hiyo hoja ya Slaa,ila wabunge fulani fulani wa CCM wanaendelea kumpinga Slaa,japo kwa pale bungeni ILA NAAMINI MOYONI WANAMKUBALI SANA HUYU MZEE WETU maana huwa anawapasha haswa!
Bravo Slaa
 
Na pia asubuhi Dr Slaa alimbana Marmo haswa kuhusu nafasi za wabunge ktk makampuni ambapo kuna mgongano sana wa kimaslahi na Marmo akasalimu amri japo alijidai haewi hilo mpaka KIONGOZI wa upinzani bungeni aliposimama akamfafanulia,na mwisho akajibu kuwa Serikali italifanyia kazi
 
naona wenye daladala wanataka kuongeza Nauli ifikie 700...wenye mashangingi yanayolipiwa kilakitu itamgusa saa ngapi? wakati watoto wao hata daladala hawapandi...?
Budget yetu bado ina mapungufu mengi, bahati mbaya Bungeni tunapeleka waimba Kwaya na wacheza Drama, watapata muda gani wa kuipitia Hio Budget...bado wao wana vibiashara vyao vya kujiongezea mapato, wanabeba mabrief case tu, na hakuna anaekwenda kusumbua AKILI yake alau kusoma.... I do believe wapinzani kwa number yao...kila mmoja akosoe pale panoonekana ni udhaifu, na ikibidi kama KUSUSIA upitishaji wa Bajeti hio ufanyike...Alau kususia ni ALAMA ya kuonesha kuwa hukubaliani na bajeti isiyokuwa na Maana kwa wananchi...
 
Kuna msemo usemao "they lough at you because you look different but I always say lough them back cause they look the same"
 
Tumeliwa kabisa wazalendo ikiwa mambo yenyewe ndo haya
 
Nafikiri Kuna kila haja ya sisi kuwahamasisha wananchi wawe wanafuatilia bunge na kusikia yale wabunge wao wanayoyasema bungeni.

Hili litasaidia kujua nchi yetu inakoelekea coz kuna baadhi ya watu wamekunywa maji ya kijani hawatki ckia lolote baya kuhusu sisiemu.

Nadhani wakisikia kwa mackio nakuona kwa macho yao wataamini yale tunayawaambia hapa JF na huko mitaani.

Bravo Dr Slaa "Drive of Change"
 
Hapa ndipo wagombea binafsi wanapohitajika ndugu zangu.
 
Hongera Slaa

Kuna baadhi ya wabunge akiwa mwakilishi wako hata unajidai, kusema nina mwakilishi haitaji vyeti kujua amekata shule, nafikiri wapiga kura wa Slaa na watanzania kwa ujumla tunajisifu kwa kuwa na mbunge huyu bungeni.

Nashindwa kuelewa wale Maprofessor kama akina Sarungi hivi bado wako Bungeni?
 
Wabunge wengi wako pale kwa ajili ya posho, hata mimi ningejivunia sana kama Slaa (ama mbunge yeyote wa upinzani) angekuwa mbunge wangu! Kwasababu angalau wao wanagusa mioyo ya wananchi wa Tanzania!
 
tufanyeje tuwe na wabubge wengi kama akina slaa? MUNGU TUSAIDIE, uifanye mikono wa mafisadi ife ganzi kila wanapotaka kuchukua fomu za kupigania ubunge, uzifanye biashara zao za kifisadi ziwe mahame, wakose hata ndururu za kununulia hizo fomu, uwapige na ukoma na kamwe wasisahau JINA lako wewe mwenye uweza
 
Nina imani hapa ndipo tunapoona mantiki na haja ya kuwa na wabunge wenye shule inayoeleweka kuweza kupambanua mambo kwa ufasaha, uzalendo wa kweli na kujua nini kilichowapeleka huko bungeni. Lakini wengi wa wabunge wa CCM sidhani kama wana muda wa kuichambua hotuba ya bajeti kwa kina na kutoa kasoro kama alizogundua Slaa... yawezekana baadhi yao pale wanaangalia hesabu ya siku anazoingiza seating allowance basi akafungue mradi akirudi kwake..
 
**********************
Natumaini kwa mchango wake huu Dr.Slaa, sasa tutakubaliana kuwa ni muhimu kwake akawepo ndani ya Bunge kuliko kujaribisha uraisi na hatimaye kubaki nje ya Bunge na kuwa mtazamaji tu. Keep it up Dr.Slaa.
*********************************
 
Dr. Slaa bado naamini wewe ndio unafaa kugombea Urais wa Tanzania mwaka 2010. Usiwaachie vichwa maji kina Kikwete wazidi kuitumbukiza Tanzania kwenye Umasikini.
 
Tatizo kubwa ni kuwa wabunge wenyewe hawana hata ule uwezo wa kuweza kuchambua kwa kina vile vipengele vya katiba na implicatios zake katika uchumi. Wao walipoambiwa tu kuwa kodi ya mafuta haijaongezwa wakasahau kwamba kwenye bajeti ni zaidi ya kodi ya mafuta. Kuna umuhimu wa wabunge wetu kuwa na uwezo
 
Back
Top Bottom