afadhali umesema unadhani, kwa sababu hiyo requirement ni ya uraisi tu, kwa VP ni kujua kusoma na kuandika kiswahili AU kiingereza, ndio maana Dr Slaa hajawekewa pingamizi kwa mgombea mwenza hadi leo, otherwise angekua ameshang'oka kwenye kibnyeng'anyiro.
tatizo si katiba inasema nini as inatoa minimum requirement, ila je is that the best Chadema can do in regard to mgombea mwenza aka VP mtarajiwa?
tunahitaji watu wachapakazi, sio wanaofuata posho na mishahara minono, matokeo yake watu wanaacha taaruma zao wanaanza kupiga porojo!
Mkuu, nadhani ulimaanisha taaluma.
Kuna kila sababu ya kuheshimu mawazo yako,lakini ebu tuwe wakwelidarasa la saba awe makamu wa raisi,na imekuwaje mpaka amefikia umri huu ameshindwa kujiendeleza ili kuongeza madarasa japo kidogo.Kwa dunia yetu ya sasa hauwezi kusema elimu haina nafasi katika harakati za kuchagua kiongozi.Semeni msemavyo kama jamaa ni darasa la saba,chadema wamechemka.HIVI HII NCHI INAELEKEA WAPI.
Sitaki kuamini kuwa ni darasa la saba, lakini ukweli utabaki pale pale, kama tumekuwa na watu wenye shule zao lakini wametumia shule zao kuwahadaa wa -TZ, ni bora huyo std 7 kama atakuwa mjapakazi!
Ndugu yangu soma vizuri hiyo cameron's governments. Inaonekana hata wewe mwenyewe huelewi unachosema. Kuna tofauti kati ya great Britain(England, wales and Scotland) and united kingdom(Britain and northern Ireland) statistics za 2007 zinaonyesha kwamba united kingdom(Britain and northern Ireland ) inazaidi ya watu mil 61Hivi Dr. Slaa na CHADEMA mmecheck usahihi wa mifano mnayotumia?
Argument ya ukubwa wa serikali ni nzuri sana lakini mifano inayotumika haiko sahihi. Mara mbili nimesoma Dr. Slaa akitoa mfano wa UK kuwa na baraza la mawaziri dogo na kutaja namba ya 14 lakini ukweli unapingana na hayo madai yake.
Uingereza ina mawaziri wapatao 100 kama unajumlisha na mawaziri wadogo na sio 14 kama anavyodai Dr. Slaa. Pia Uingereza ina watu karibu 60M na sio 300M anavyodai Dr. Slaa. Hata ukichukulia mawaziri kamili basi wako karibu 30, sijui hiyo namba ya 14 kaitoa wapi?
Mbali na serikali ya UK yenye hao mawaziri karibu 100 pia kuna serikali ya Scotland, Wales na Northern Ireland na kwa ujumla kufanya nchi iwe na baraza kubwa sana la mawaziri.
Baraza la mawaziri la UK linaweza kupatikana hapa:
BBC News - Cameron's government: A guide to who's who
ni kweli wanaweza wasifike mil 300.
Apunguze kasi. Atumie watu wanaojua wanachokifanya kabla ya kutoa hizi hotuba. Makosa kama population ya uingereza hayastahili kwa mtu ambaye anataka watu waamini kuwa anastahili kushika uskani wa nchi hii.
Hivi anaamini kweli kuwa yeye atachukua urais na chama chake kitazoea majority ya vitu kwenye bunge? Very likely hata akishinda urais itambidi apanbane na hostile bunge. Sitashangaa kuona vyama vingine vikiungana na CCM ili mradi kuinyima majority Chadema!
Amandla.........
Kwani hawa waliosoma mpaka wakakubuhu wametufikisha wapi?Hapa ndio nilikuwa napataka.. Nakubaliana kabisa na kufutilia mbali manaibu waziri, kuunganisha wizara. Lakini sikubaliani na kuanzisha serikali nyingine ya tatu, sababu nayo itaongeza ukubwa wa serikali na kuongeza matumizi. I think serikali mbili ni sawa, na Tanzania haiwezi kuafford cost za serikali tatu.
Kuhusu kufuta wakuu wa mikoa na kuanzisha balaza la madiwani nadhani nalo ni matope. Dawa ni kufukuza wakuu wa wilaya, na kuestablish system ambayo itakuwa inamsaidia mtanzania bila ukiritimba. Tatizo ni kusave pesa na kuondoa ukiritimba.
Kingine kutuwekea std seven ambae anakwenda kubishana na watu kama IMF, World Bank au Paris Club is total irresponsible. Chadema nadhani wanaleta masihala, at 21 century mnaleta mifano ya mwalimu na serikali yake? Mnakwenda kubisha na policy za WTO ambazo zinatukandamiza kisha nyinyi mnaleta masihala......
2015 tuleteeni mgombea mwenza wa ukweli... this is sold out..
Kwani hawa waliosoma mpaka wakakubuhu wametufikisha wapi?
I think you answer prove why Tanzania need change. So, kama waliosoma wamesababisha Tanzania kufail then dawa ni kuweka wasiosoma? You know JF has become like genge la shekilango, people doesn't use their brain to think.
kajifunze kwanza lugha kabla ya kujaribu kuitumia.
Watu kama wewe eti mnajiita mmesoma? aibu tupu
Swali lipo pale pale. Makamu wa raisi ndio msaidizi/mrithi wa raisi pindi raisi anapoanguka (death). Sasa kama Mr one breath away yeye ni std 7, na watu kama wewe wanasupport. Then sidhani kama tunataka mabiliko ya ukweli, au tunataka kubadilisha kanzu.