Tuijali nchi yetu. CCM ipumzishwe mwaka huu. Binafsi nitajitahidi kushawishi watu wengine zaidi ya kumi ili wamchague Dr. Slaa, huu ndiyo mchango wangu kwa nchi yangu Tanzania.
Na huu ndio mchango uliotukuka. Wenzetu walioendelea walifahamu maana ya neno mabadiliko.....ni vizuri na wengine wakapewa nafasi ya kutuongoza ili tuwe na adabu katika kazi ya uongozi.
Hivi cheo ni dhamana au CCM wanataka iweje???? kwamba cheo ni roho hata ukifa unaondoka nayo????
Ili uchaguzi 2015 uwe na maana.....ili tuone maendeleo kwa Taifa hili miaka 5, 10, 15....200 n.k ijayo...ni lazima CCM ing'oke 2010.
JK angeweza kufaa kwenye ukatibu wa chama cha mafisadi ngazi ya kata lakini si urais wa nchi kama Tanzania.......hawezi. Hii nchi kwa miaka mitano iliyopita imeharibiwa mno....yaani Taasisi za serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ndio vimeongoza Taifa hili tangu 2005.
Ni kwamba JK ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa ukiwa Rais basi huna kazi.....kwa kuwa chini yako kuna watu wanakufanyia kazi...kwa hiyo kazi yako wewe ni kula na kulala, kuzunguka zunguka na kutalii nchi za kigeni, kufanya anasa za kila rangi na aina na mengineyo mengi....sasa kama huu sio upunguani ni kitu gani. Ukiongoza mazuzu hili linawezekana.
Urais ni kazi ngumu sana tofauti na watu kama JK wanavyodhani.
Watanzania naomba mjue kuwa JK ameboronga mno na hili litathibitika atakapotoka madarakani....na ndio maana anaogopa mno kung'oka. Na hata 2015 tayari anataka kupandikiza mtoto wa swaiba wake...Rais wa Zamani ili kwa miaka mingineyo 10 hadi 2025 asiwepo wa kuhoji kuboronga kwake.