Elections 2010 Slaa: Mgombea sahihi katika wakati mbovu.

Mkandara--
Kiukweli Chadema wasingemuweka Slaa, uchaguzi ungekuwa kalas. Mi naona the only way for CCM to behave and govern appropriately is for Chadema to gain more strength. The guy is unlikely to win this election, but if he can get 30+ percentage points na viti 70-100 vya ubunge. That would be a powerful remainder for CCM to actually start to govern.

Swali ni can Chadema be a serious opposition party? can they organize themselves in nyumba 10-10, come up with sera za maendeleo ya uchumi that is alternative to CCM's and be able to sell them kwa Mtanzania wa kawaida kama mimi. If they can do that, and sustain it for long time, then they can gain the trust ya mtanzania wa kawaida. And they have to remove the label ya uchaga. Najua wadau hawataki kuisikia, but kwenye vijiwe vya mtaani it resonates a lot kwa non wachaga watanzania. I will speak kama mwanachama wa CCM, I think we need a strong Chadema in this country to make politicians in power more accountable.
 
napata kichefuchefu kuona post yenye wehu kama ya ngoda, nyerere alivyopata madaraka uzoefu wake kauanzia wapi????
 
Hivi kuna wapenzi/washabiki wa sisiemu wenye hata kadigrii kweli?. Maana huwa naona wengi wao wanaupeo mdogo sana wa uelewa wa mambo.Ni kama walivyo kubaliana kukataza wagombea wao kushiriki midahalo.Kwani ss tunachagua sura?.Nadhani wengi wa washabiki wa sisemi wamepofushwa na maslahi wanayopata.Kama huyu ameandika waraka mrefu usio na facts zozote kha!.
 
Haha Slaa fixi tu, nilimsikia jana ati akichaguliwa ataleta high speed train, Mwanza-Dar in 3 hours... Msanii tu

It can be done, buddy. Hakuna kisichowezekana katika nchi tajiri kama Tanzania. Kupanga ni kuchagua tu.
 
Haha Slaa fixi tu, nilimsikia jana ati akichaguliwa ataleta high speed train, Mwanza-Dar in 3 hours... Msanii tu
Hiyo avatar yako inaonyesha namna ulivyo.....Fisadi....ahahaaaahhhhah!
Kuwa na high speed train ni kitu kinachowezekana kabisa!
 
Hakuna chajadili na mawakala wa mafisadi
 

Nimetembelea majimbo 15, kati ya hayo 10 ya vijijini na 5 ya mjini. Huwezi kuamini katika majimbo 10 ya vijijini, majimbo 6 hata jina la Slaa hawalijui. Tumebakiza mwezi mmoja na nusu, kweli Slaa atafanikiwa kujiuza huko? Ninawasiwasi!

Moshi na Mara huko atashinda kwa kura zaidi ya 65%, lakini hizo hazitoshi kwani mikoa hiyo haina hata 10% ya watanzania wote. KUSHINDWA KWA SLAA KUSIWAFANYE WANACHADEMA KUDHANI KUWA WAMEIBIWA, NA KULAZIMIKA KWENDA MABARABARANI KUANDAMANA.

Kwangu Upinzani si dhambi, ni kinyume. Usichoelewa na kukubali ni ukweli kwamba Slaa kushinda urais 2010 ni ndoto ya mwendawazimu isiyotekelezeka. Angalia alivyoanza kutoa ahadi zisizotekelezeka, akidhani watanzania ni majuha. Kweli huyu kaishiwa na kapoteza kiti cha ubunge.

Unajua Mzee Mapesa Cheyo, alianza kugombea urais mara kadhaa. Wajuzi wakamshauri kuwa hayo ni maji mazito kwako, laiti ungegombea Ubunge ungepatata na kuwawakilisha wananchi wako na Chama chako ipasavyo. Akawa mtulivu na kusikiliza wajuzi, leo hii kiti hicho si rahisi chama chochote kukichukua, hata kama hatapiga kampeni. Ushauri huu wa bure Unamfaa Slaa vile vile. Asiposikia la mkuu atavunjika guu. Furaha yenu inakoma siku ya uchaguzi!

Tumepoteza kiti cha mbunge maarufu, nitaikosa sauti yake pale Bungeni.
 


Think smarter, not harder
 
mi nilifikiri ukiandika kwa kiswahili kidogo unaweza kujenga hoja.....maana thread zako za kingereza huwa nikisoma nasikia kichefuchefu kwa zile "direct translation" sasa nimeelewa tatizo sio lugha ni akili tu hapa!:becky:
absolutetly.
 
Nimetembelea majimbo 15, kati ya hayo 10 ya vijijini na 5 ya mjini. Huwezi kuamini katika majimbo 10 ya vijijini, majimbo 6 hata jina la Slaa hawalijui. Tumebakiza mwezi mmoja na nusu, kweli Slaa atafanikiwa kujiuza huko? Ninawasiwasi!

Wewe umetembelea, mimi maisha yangu kwa miaka 14 sasa yamekuwa ya kuishi na kufanya shughuli zangu vijijini kwa zaidi ya asilimia 60 ya muda wangu kwa mwaka, Dr Slaa anafahamika. Subiri kivumbi cha tarehe 31 Oktoba,2010.
 
Vibaka? Ha ha hhha. Waulize Jamaica, jeshi walipambana na kibak zaidi ya siku kumi, zaidi ya watu 200 waliuawa. Sikwambii huko Latin Amerika.

Watanzania mtakusoma na kupindukia bila kujua matatizo ya msingi yanayowasumbua. Kweli nyie badooooooo!
Kumbe ww sio mtz? .kwa hiyo wewe tayari?

LOW
 
Wewe unawasiwasi gani?.....inakuwasha pasipo kunika bila usaidizi nini?

LOW, again
 

Tutajie majimbo hayo kwanza kabla haujaendelea na kampeni zako.

manake napata shida kukuelewa eti kuna mahali fulani ndani ya nchi hii ya kambarage hajawahi kusikia jina la Dr. Slaa?? Bahati nzuri mlipoanza mipasho na udaku kuhusu maisha yake ya ndoa mkidhani mnambomoa kumbe ndo mmempandisha chati kila kona nchi hii watu wanaulizana Dr. Slaa ni nani na wanataka kumjua. Manake kule vijijini kila mmoja anatembea na karedio kake, vipindi vyote vya magazeti kwenye redio zote wanasikiliza, halafu bila aibu unamwaga pumba bila aibu? kweli ccm hamna haya hata kidogo.
Je, unataka tuamini kwamba mkakati wenu wa kuiba kura umeshakamilika?Manake kama unatuthibitishia kwamba Dr. Slaa atashinda Mara na Moshi tena kwa 65% basi ccm mwaka huu mnatisha. Labda nikubaliane na wewe kwamba utaikosa sauti yake pale bungeni, lakini usipate tabu, sauti yake utaisikia ikirindima kutoka magogoni.
 
Kama unahisi na kuamini kuwa Dr. Slaa ni mwepesi kwa JK, kwanini unahangaika nae? SI umwache usikie matokeo tu? Maana katika post yako hii, sijaona ukizungumzia mgombea mwingine wa uRais zaidi ya Dr. Slaa. Hii inathibitisha kuwa, huna uhakika sana na ulichokiandika hapo juu.
Naamini unatania unaposema kuwa Slaa angegombea wakati wa Mkapa angekuwa na nafasi bora zaidi. Maana sijui tathmini yako hiyo inatokana na nini. Kama inatokana na ufanisi wa kazi za Urais kati ya Mkapa na JK. Ni dhahiri kuwa JK hajafanya lolote la maana kwa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, endapo utamlinganisha na Mkapa.

Naamini kuwa, JK alishinda kwa kishindo zaidi mwaka 2005 kutokana na hisia za wengi kuwa, alikuwa kwenye serikali iliyofanikiwa sana ya Mkapa, na hivyo uzoefu wake ungeweza kuendeleza mazuri ya awamu ya 3 na kuanzisha mema mengine kwa awamu yake. Ila ukweli uko wazi kuwa hata yale mazuri aliyokuta ameyadhoofisha. maarufu wake umeshuka sana.

Unaposema JK amemaliza matatizo ya kimsingi ya mTanzania, unataka kuanzisha kilio kwa wengi. Ingekuwa vyema kama walau ungesema alijaribu kushughulikia masuala ya usalama (japokuwa usalama wa nchi sio mzuri wa kujivunia).

Lakini masuala ya msingi sio usalama pekee. Kuna masuala ya uchumi (hajui hata maana yake). Masuala ya sheria na katiba ambayo ameyakiuka kila alipopata nafasi ya kufanya hivyo. Masuala ya afya ambayo bado nchi iko hoi na hakuna unafuu hasa katika afya ya mama na mtoto ambayo nadhani ni ya msingi zaidi. Elimu, inaonyesha (statistically) kuwa kuna ongezeko kubwa la wanafunzi wanashindwa mitihani kila mwaka.

Sasa hayo unayoita ya msingi ni yapi Zawadi?

Nadhani ni vyema tusubiri tuone matokeo yatakuwaje ndipo utajua kuwa waTanzania wana hasira an serikali yao. Ukizunguka kidogo na kuongea na watu utajua nia ya watu kupata mabadiliko.

Lakini hata kama Dr. Slaa akishindwa kwenye uchaguzi huu (sioni kivipi kama tunajua tunachotaka), atakuwa ametoa funzo kwa watawala wanaodhani kuwa haiwezekani siku moja nchi kuongozwa na upinzani. Pia, ni dhahiri kwa ushiriki wake kwenye uchaguzi huu kama mgombea wa Urais, Dr. Slaa anatenegneza nguvu kubwa sana kwa wapinzani, na ni dhahiri kuwa watakuwa na viti vingi bungeni kuliko kama asingegombea. Wakati mwingine, ni vyema kupoteza kidogo ili kupata vingi zaidi.

Dr. Slaa atapata kura za kutosha tu. Anachotakiwa kufanya ni kuongeza bidii katika kampeni na kufika kila kona ya nchi na kushawishi wapiga kura wamchague.
 

Kufika kila kona ya nchi ndilo litalomuangusha na ndilo nililolizungumzia. Hili si rahisi, kukiwa kumebaki siku 45.

Slaa hana silaha ya kushinda uchaguzi.

Sikuzungumzia wagombea wengine kwa sababu, sijaona kama mnawaandika sana. Isitoshe tuna muda wa kuwazungumzia na ni wengi, hivyo ili kutowachosha wasomaji ni bora kuwagawa katika makundi. Hapana shaka akuina Lipumba , Mrema na wengineo watakuja katika makala ayajayo.

Nasikitika kuangushwa kwa Slaa katika uchaguzi huu.
 

Haya kila ukweli utaitwa 'UDAKU', nia yenu ni kutufunga midomo. Hilo hamtafanikiwa, kwani Slaa akivuruga wote tutaumia.

Nitaandika mapungufu yote ya Slaa hapa ubaoni, si kwa nia ya kumuangusha bali ni kuwaelewesha watanzania kumuelewa kwa karibu sana Slaa, mgombea Urais.

Hii ni wiki ya SLAA. Msichukie, la msingi nikosoeni pale nitapomuelezea yasiyosahihi.

SLAA HANA SILAHA YA KUSHINDA URAIS.
 
Huyu aliyeanzisha thread hii wakati mwingine inatakiwa aone aibu. Duh! Anapenda vibaya.
Eti Kikwete 'kaviunganisha vyama' wakati yeyena wana-mtandao wenzake ndio waliokuza mgawanyiko na makundi ndani ya hicho chama kimoja (CCM).
Wanamtandao wakajiona ndio wametwaa madaraka, wala sio CCM kama chama. Na nafasi nyeti akawapa hao wenzake kwa kuzingatia uana-mtandao na ushkaji, wala sio uwezo wa utendaji. Matokeo yake ndio haya tunayoyaona. Uozo mtupu kwenye utendaji.
Ila in a long run Tanzania itafaidika kutokana na utendaji m-bovu wa Kikwete, kwani mwaka huu anang'olewa na kura za wananchi.

Kuh Zitto, huyu thread-starter asipotoshe kuwa vijana tunawapigia kura watu kwa kuangalia umri wao, au sura zao. Tumeumizwa 2005, sasa tumeshtuka, tunaangalia uwezo. Anataka kupotosha watu hapa. Ni Dr Slaa tu sasa. Zitto naye anapambana jimboni kwani anahitaji kurudi Bungeni.
Ni kama vile mpiga porojo Makamba aliposema kuwa CCM inamhofia zaidi mgombea mwingine wa urais kuliko Dr. Slaa. Actually, the opposite is true.
Wanamhofia Dr. Slaa ndio maana wanajaribu kurusha madongo kwake. Tumeshtuka.

Kwa hiyo Kikwete hajaondoa tofauti, ila ameongeza tofauti na kuimarisha makundi ndani ya CCM kwa kuweka juu uana-mtandao badala ya uana-CCM. Hongera kwa hilo. Tanzania kama nchi itafaidika kwa utendaji m-bovu kwani wengi walioangalia SURA zaidi au kujali CHAMA zaidi badala ya UWEZO wa mgombea sasa wanazidi kujutia na KUBADILIKA.

Mungu ibariki Tanzania...
 

Zawadi, nadhani hukusudii kuniaminisha kuwa Dr. Slaa hajaanza kampeni. Maana ukizungumzia siku zilizobaki bila kujali alizotumia, na jinsi alivyozitumia, inakuwa sio sahihi.

Kama zimebaki siku 45 na ameshapata ushabiki na uungwaji mkono wa kiasi hiki, basi ni dhahiri kuwa anaweza sana kupata kura nyingi sana na si ajabu akashinda uRais.

Usijali sana kuwepo kwake Bungeni. Kinachonipa matumaini ni idadi atakayoipeleka Bungeni wakati huu.

Kutoka kwake nimejifunza kuwa, ukitaka ushindi wa kudumu, wezesha wenzako kushinda kwa wingi bila wewe kushindwa kabisa. Ila, kama angenag'ang'ania kukaa Bungeni na kuacha wenzake wakiwa wanagalagala nje, ni dhahiri kuwa ingefika siku angekuwa nje ya Bunge, na wenzake wangebaki wanagalagala zaidi. Hatua yake hii, ni ushujaa tosha.
 

Nimesoma mabandiko yako mawili. Yametulia hasa na yamepandisha madarasa kiasi cha kutosha. Bila shaka Zawadi atakubaliana na wewe na atafunga mada hii
 

Kama Dr Slaa hafahamiki, Mabilioni ya CCM ya Kampeni ya nini?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…