Elections 2010 Slaa na Mbowe, nani atafaa kwa urais 2015?

Chadema ni chama makini sana hakikurupuki kitajipanga na kitatupatia mgombea makini na sasa ni mapema sana kusema ni nani atagombea urais kupitia chadema kwa kuwa tuna watu wenye sifa wengi sana na waadilifu kwa hiyo kwa sasa tujipange tupate katiba mpya na tupate tume huru ya uchaguzi ndio tutamjua mgombea uraisi kupitia chadema uwenda akatoka ccm au akatoka humo humo ndani chadema
naomba kuwasilisha peoples powerrrrrrrrrrr
 


Wewe ndiwe mmoja wa vijana wa Nape mliotumwa kuleta mashambulizi siyo, hebu mjaribu kuwa na kumbukumbu kama mnataka kuwa waongo. mara mjadala makao makuu ya CDM mara majada wa pale mtaani, lipi ni lipi?
 
hapa ndipo ccm watakapo patumia kuimaliza cdm
watakuwa wamekula ngombe mkia umewashinda
 
Acheni kwenda kwa kubahatisha!

Mambo ya uongozi wa juu lazima yaanze kufanyiwa kazi mapema. Hoja ya msingi ni kuendelea kuwatambua (na sio kuwachagua, wala kuwatangaza, au kuwapamba) watu wenye sifa na uwezo, na ambao watakuwa na uzoefu wa kutosha- by then - nasisitiza uzoefu, meaning ufahamu mzuri wa masuala ya kitaifa. Tuepuke kusukumizia Wa -Tz mtu ambaye ataonekana na baadhi yetu kuwa anafaa ati kwa kuwa ana jazba tu kama Big Ben alivyokuwa hadi akataka kuuza mpaka hewa tunayovuta! Kisa - ubovu wa mashirika ya umma na sera zake mbumbumbu za ubinafsishaji. Kwa sasa hivi tu concentrate kwenye kukijenga chama ili kuuondoa huu uozo uliopo madarakani lakini tuwe makini kukumbuka uchaguzi unakuja.

 


Gurtu watu walikuwa wanabadilishana mawazo, hili ni jambo la kawaida. Hawakuwa wanagombana.
 
Makao makuu ya CHADEMA, watu wanabishana kuhusu nani agombee 2015, wewe ungeweka tu kama wewe uonavyo na wala hakuna cha watu wala mtu, ila mimi sintakuita umetumwa na Nape. Jitahidi kuweka thread za maana na za uhakika, tusonge mbele
 
Wasipokuwa makini mwaka 2015 nao watagawanyika kama CCM.

kATAVI, Chadema ni chama makini, hakuna mgawanyiko wo wote. Sikubaliani na nia ya mleta hoja hata kama amewanuku watu waliokuwa wanabadilishana mawazo kwa nia njema. Kwanini alete hoja hiyo mapema humu?. Anataka kutugombanisha au anataka kutuondoa kutoka kwenye focus ya kujenga chama. Nadhani huyu ametoka chama cha mapinduzi. Hatutakii mema. Sisi tunakwenda kiutafiti zaidi, hatushindani kwa kutoa fedha za rushwa kama cha cha xxxx. Thx
 

napita tu jamani, ngoja niendelee kuichambua budget kisha nirudi kwenye mchakato wa katiba, then ntarudi kwenye mchakato wa nani anafaa kuwa raisi ikifika mwaka 2014.
 
Gurtu watu walikuwa wanabadilishana mawazo, hili ni jambo la kawaida. Hawakuwa wanagombana.

Mikael P Aweda, Mkuu hayo maandishi ya bluu chini ya Avatar yako nimeyapenda, ahsante kwa kumtia moyo Gurtu lakini bado na mashaka na hao waliokuwa wanabadilishana mawazo kuhusu nani anafaa kati ya Mbowe na Slaa
 
Mambo ya utais kwa si hoja ya msingi,muda bado na anayefaa anafahamika.
 
Kwani nyie ccm mnadhani nani anafaa kuwa kwenye hiyo nafasi ya Urais kati ya hao mliotupatia.kati ya Mh Dr W.P.Slaa NA Mh F.Mbowe.Pendekezeni jina moja maana wote sisi tunawaona ni vinara.
 
wote wanafaa, ila kwa kuwa katiba inatambua prezidaa mmoja, basi mmoja itabidi ampishe mwenzake
 
Angalieni amejiunga lini na nini lengo la thread yake kabla ya kuaanza kujibu.

Join Date : 12th May 2011
Posts : 22
Thanks 0 Thanked 1 Time in 1 Post

Rep Power : 0
 
It is too early now to discuss about Chadema presidential candidate in 2015!!!it is convinient time now to discuss about strategies on how to alleviate ordinary Tanzanians' poverty!!!
Mimi nilidhani wewe ni bushmen utaongea lugha tofauti kumbe hata ung'ng'e unaujua!

Kidding....
Badilisha avatar yako basi mkuu!
 
Kwa mtazamo wangu nafikiri CDM wafanye kama walivyofanya CCM kipindi ambapo Mkapa na Kikwete wote walitaka kugombea (i think ni 1995) na mwalimu nyerere akamwambia Kikwete muda wake bado asubiri so Mkapa akapita ingawa alikuwa na umri mkubwa kuliko Kikwete. So nafikiri Mh. Mbowe inabidi naye aambiwe bado muda wake amwachie mzee wa ukweli Dr. Slaa atuvushe kwenye haya matatizo.
 


wewe sio mwana wa daudi bali ni mwana wa goliati, japo kuna vita ya chinichini kati ya mbowe na hisia za slaa juu ya 2015, ila mbowe asiumize kichwa kuota urais hana jia ya kupitia.
 
Huyu katumwa na Nape. Hana lolote. Kwanza, nani kamwambia kuwa Mbowe anataka urais? Hata mwaka 2005 alijitosa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuombwa na chama. Mbowe hakutaka kugombea nafasi hiyo.

Sasa nami namuuliza: Kati ya Wilson Mukama, Lowassa, Rostam, Migiro, Hussen Mwinyi na Benard Membe AKA Joka la Mdimu, nani atafaa kugombea urais?
 
Huyu katumwa na Nape. Hana lolote. Kwanza, nani kamwambia kuwa Mbowe anataka urais? Hata mwaka 2005 alijitosa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuombwa na chama. Mbowe hakutaka kugombea nafasi hiyo.<br><br>Sasa nami namuuliza: Kati ya Wilson Mukama, Lowassa, Rostam, Migiro, Hussen Mwinyi na Benard Membe AKA Joka la Mdimu, nani atafaa kugombea urais?
 
Kwani nyie ccm mnadhani nani anafaa kuwa kwenye hiyo nafasi ya Urais kati ya hao mliotupatia.kati ya Mh Dr W.P.Slaa NA Mh F.Mbowe.Pendekezeni jina moja maana wote sisi tunawaona ni vinara.

Kweli wao ndo watuambie ni nani wandhani anwafaa kuwa Raisi wao? Sisi wote wawili ni majembe yanayoweza kubadilishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…