Huyu katumwa na Nape. Hana lolote. Kwanza, nani kamwambia kuwa Mbowe anataka urais? Hata mwaka 2005 alijitosa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kuombwa na chama. Mbowe hakutaka kugombea nafasi hiyo.<br><br>Sasa nami namuuliza: Kati ya Wilson Mukama, Lowassa, Rostam, Migiro, Hussen Mwinyi na Benard Membe AKA Joka la Mdimu, nani atafaa kugombea urais?
Wanajamvi,
Jana nilikuta mabishano makao makuu ya chadema. Wengi wao ni wajumbe wa Baraza kuu ambao wanaamua hatma ya mgombea urais wa chadema 2015. Wanasema Rais ajaye atatoka chadema. Lakini mgawanyiko ukaanza pale ambapo wanamjadala waligawanyika ktk makundi ya Mbowe na Slaa.
Wanaosema Slaa wana sababu hizi;
Umaarufu wa Chadema umejengwa na Slaa.
Watanzania wanampenda Slaa zaidi ya mtu yeyote Chadema akiwepo Mbowe.
Slaa anajua mambo mengi kwa kuwa alikuwa bungeni 15 years?
Slaa ana elimu kubwa kuliko Mbowe.
Changamoto zake.
Ana umri mkubwa 2015 atakuwa na 67.
Historia ya upadri inawasumbua baadhi ya wapiga kura hasa waislamu. Mbona 2010 alipata kura nyingi? Still debatable.
Waungaji wa Mbowe.
Mbowe umri mzuri kuliko Slaa -- 62 vs 50 ya mbowe. 2015 atakuwa 55
Mbowe atatusaidia kwa fedha zake wakati wa kampeni.
Anajua kujieleza sana kupita hivyo atawashawishi wapiga kura.
Changamoto yake
Ana elimu ndogo.
Watanzania kutowaamini wachaga
Baada ya mjadala ule wa mtaani nikampigia moja wa mrafiki zangu ambaye ni kiongozi wa chadema wa makao makuu kujua wanampango wa kumpitisha nani awe mgombea wao wa Urais wa mwaka 2015. Akaniambia vikao vya chama vitaamua. Hata hivyo, kuna ukweli kwamba Mbowe baada ya kuona kuwa chadema inaungwa sana mkono anafikiria kutaka kugombea mwenyewe tena. Halafu akamalizia japo kuwa Mbowe ni rafiki yangu naona kama hajakubalika kama Dr Slaa.
My take; Mbowe na Slaa wakiingia wote ktk mchakato wa kura za maoni wataivuruga Chadema.Heri wakubaliane moja wao agombee baada ya kufanya utafiti.
We Narubongo, kwanza na wasi ms uraia wako. Alafu Internet bill yako iko subsidized na CDM utaacha kutetea?
Dr Slaa inawezekana asipate ridhaa ya mh Mbowe kuwania urais. Inaonyesha kuwa Mh Mbowe ana mkakati wa kugombea urais mwenyewe na hi inadhirika kwa kutaka uongozi bungeni na kungagania uenyekiti.
Harakati zake zimeanza. Alimwachia Slaa 2010 maana alijua kumtoa incumbant kikwete ni vigumu lakini kuwania na mtu mpya 2015 ni rais.
Hata na Zitto anataka. Ugomvi umeanza. Mode usinichakachue