Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

Thanks C/Mkwawa for useful info, nauliza, nikitaka kumnunulia mtu zawadi Samsung S 5 ya clone mpya ambaye sio mtaalam wa mambo ya sim, je ataweza kujua kama hio sio original ? Yaani kuna namna awezagundua kirahisi ?
 
Naomba mnielekeze na aina ya vioo ambavyo havivunjiki kirahisi hasa simu ikidondoka, maana uzembe wangu upo kwenye kupasua vioo.

1.saphire
2.gorrila glass 2
3. rugged smartphone

1.saphire screen
hivi ni vioo vigumu kushinda hata gorila glass lakini so far sijaona simu ya chini ya milioni moja yenye hivi vioo

2.gorilla glass 2
hivi ndio vipo kwenye flagship nyingi sana havipo strong sana ila vinasaidia navyo

3.rugged smartphone
hizi ni simu ambazo zimetengenezwa kuvumilia mazingira magumu na huwa si rahisi kuharibika zikidondoka mfano simu za caterpillar
 
Thanks C/Mkwawa for useful info, nauliza, nikitaka kumnunulia mtu zawadi Samsung S 5 ya clone mpya ambaye sio mtaalam wa mambo ya sim, je ataweza kujua kama hio sio original ? Yaani kuna namna awezagundua kirahisi ?

hata asipogundua akienda kuringishia marafiki zake wapo wajanja wataigundua. kama budget ndogo tafuta simu unique za bei ndogo
 
Mkuu nakubaliana na wewe hasa kwenye kwenye gorilla glass,maana nimewai kutumia kwenye HTC desire S.
ila hivi vioo vya TFT naona kama chenga hivi yaani ubora wake wa kutilia shaka.

Hivyo vya saphire ni vyema ungefafanua vinatoka na simu gani Bila kujali bei.
 
Naomba utaje na simu nzuri ambazo ni bora sana za kuanzia 500k hadi milion moja kama hutojali ambazo hazifi haraka chember ya sim Card

Huawei Ascend G700,hutajuta,ina RAM ya 2GB,5.5inch screen,internal memmory 8gb.
 

Mkuu kwenye maswala ya simu upo vizuri hakudanganyi mtuu asee nakukubali naku PM namba yangu kwa stor zaid thanks
 
Mkuu mi nilikuwa nauliza ni simu ipi ya bei Poa mwisho Tsh 150,000/= yenye camera nzuri ambayo inauwezo wa kutoa picha safi na bei yake plz
 

simu za mabilionea wa kirusi wala usiulize bei maana ya bei rahisi utaambiwa dola elfu 10, ila kuna tetesi iphone 6 inakuja na saphire glass haipo mbali unaweza isubiria hio
 
Mi nna Lumia 710, yaani ni choo cha kike, nifanyeje ili niweze kudownload na kutumia huduma za pesa pesa?
Wana JF jaribuni kuipata TECNO PHANTOM A PLUS, hapa wameweza kwa kweli

mkuu hio sh ngapi!?
 

hapo kwenye kupoteza imei nadhani ni kwa wale tu wanaopenda kufanya rooting na kuweka custom roms tatizo ambalo lipo sana hata kwenye samsung. updates za kitkat za mtk mbona zipo sema ni kwa makampuni machache sana ila wenye tecno wasitegemee updates.
alafu mbona mtk6582 zina perfomance nzuri tu japo ni A7 antutu score ya 17000 plus is good enough kwa matumizi ya kawaida.
downside kubwa ni kwamba mediatek devices zinazopatikana bongo ni zile zenye quality mbovu at higher price sanasana tecno.
 

Baada ya Samsung Galaxy S2 yangu kuzima na kutowaka tena, niliamua kuhamia Windows. Nilinunua simu ya bei rahisi kwa majaribio tu, na kwa vile nina mikono mikubwa, simu niliyonunua ilikuwa ni Lumia 625.

Baada ya kuitumia kwa muda niliipenda sana hiyo simu kwani ilikuwa inafanya kazi vizuri sana licha ya kuwa ina RAM 512 tu. Nimefanya utafiti na nikagundua kwamba simu hizi hazihitaji RAM nyingi kufanya kazi vizuri, tofauti na simu za android ambazo ili zifanye kazi vizuri bila kukwama kwama, zinahitaji RAM sio chini ya GB 1 na hizo huwa na bei kubwa.

Ni hivi juzi tu nime upgrade simu yangu kuwa na Windows 8.1 na utendaji wake umekuwa mzuri zaidi. Nashauri wale wote ambao wanataka kununua simu za kuaminika kwa bei nafuu wanunue Lumia 520 au Lumia 630 ambayo ni mpya zaidi ambayo imeingia sokoni hivi karibuni.
 
Mkuu samahani kidogo naomba ufafanuzi hasa unaposema MTK maana yake nini?
 
Ninahitaji simu;
ngoja niombe wakuninunulia kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…