Smoothie inatengenezwaje?

Smoothie inatengenezwaje?

Aiseeee we kama unapenda ndizi, chukua tikiti maji changanya na ndizi, parachichi na embe, dah!! Nilitengeneza kitu hicho, ni noma, nzitooooo balaaa, haiitaji sukar wala nini
Hivoo,ladha yake je?
Naona km tikiti lipo offside hivi
 
Jaribu tikiti(water Mellon) mtindi, vanilla na sukar kdogo, usiweke maji! Afu uje uniambie
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hahahahaha we ni noma
Ni kweli mkuu. Yaani naweza kukata likikombe lizima la smoothie na nikajisikia kushiba kabisa lakini nikiona ugali na dagaa wa Kigoma na bamia chukuchuku pembeni nao nautwanga tu bila wasiwasi. Haya mambo nimegundua yanataka will power na kujinyima sana vingine utakunywa smoothie mpaka uchoke na kilo nazo zinazidi kungezeka tu.
 
Maziwa fresh 1/2+parachichi1
Maziwa1/2 +parachichi1+embe1
Maziwa1/2 +tikiti maji robo
Maziwa 1/2+ndizi 5
Maziwa 1/2+ ndizi 3+papai1/2
Maziwa 1/2+tende+parachichi

Waweza weka na abatsoda/uwatu ukipenda
Unaweza kunywa bila Sukari japo ukishindwa pia waweza kuweka
NB:Ukitumia asali Asali ni bora zaid kuliko sukari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4CABE11C-AF3D-4585-BCE1-5DBF5798F488.jpeg
9A9E1B7E-8813-4A0E-98A9-4302175D85C1.jpeg
8B0034F7-71E6-48C4-810A-53537764A716.jpeg
26F61CB0-0D4E-482A-BCD9-B6E6A9FE8643.jpeg
 
ngoja niweke comment japo ni zamani saana
 
Mi napenda ya tende na maziwa. Unaweka na ndizi kdg na karanga na habbat sauda.

Au parachichi na maziwa na na sukari. Unaweka na arki ya strawberry au vimto.
Maa Salam kwa sasa
Naomba maelezo kidogo kuhusu hiyo ya tende, maziwa na karanga. Nimewahi kunywa somewhere daah ilikua tamu sana. Anyone please?
 
Maziwa fresh 1/2+parachichi1
Maziwa1/2 +parachichi1+embe1
Maziwa1/2 +tikiti maji robo
Maziwa 1/2+ndizi 5
Maziwa 1/2+ ndizi 3+papai1/2
Maziwa 1/2+tende+parachichi

Waweza weka na abatsoda/uwatu ukipenda
Unaweza kunywa bila Sukari japo ukishindwa pia waweza kuweka
NB:Ukitumia asali Asali ni bora zaid kuliko sukari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tips kidogo kuhusu tende + karanga + maziwa.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Tips kidogo kuhusu tende + karanga + maziwa.
Chukua tende 10 zitoe mbegu
Kisha chukua maziwa glass mbili
Parachichi nusu
Karanga kijiko kikubwa 1 au korosho punje 5
Ndizi iliyoiva nusu
Kisha saga kwa pamoja hadi utakapoona inafaa kwa kunywa
Kama ni mpenzi wa vitu vitam zaid unaweza tumia asali kuongeza utam

Ukitoka hapo umeshiba
Unaweza jikuta ndo lunch yako hiyo
 
Naomba maelezo kidogo kuhusu hiyo ya tende, maziwa na karanga. Nimewahi kunywa somewhere daah ilikua tamu sana. Anyone please?
Tende ile ilorojeka ndio nzuri kiasi kama robo kdg. Maziwa kiasi kama lita moja. Ndizi mbivu moja (pupusa). Karanga kama one handful. Unaweza kununua zile karanga za Mia tano. Na habasoda kdg kwa ajili ya harufu kama vipunje Kumi tu.

Ukishatoa mbegu kwenye tende zako. Weka kwenye blender vyote kwa pamoja. Saga sana mpk iwe kama uji (puree)

Utaongeza maziwa kadri iwezekanavyo kupunguza uzito
 
Smoothies yangu ya leo

1. Papai dogo lililoiva

2. Karanga kavu, zilizochambuliwa maganda 150g

3. Ndizi mbivu 4 medium size

4. Matango 2

Nime blend hivyo vitu na maji 1.5 ltr

Nimeanzia kama Breakfast inaonyesha hata lunch sitohitaji ugali
 
Back
Top Bottom