NON-VIOLENCE PROTESTS FRIDAY!!!!!
Ndugu zangu watanzania, tangu uhuru, ni karibia miaka 50 sasa imepita. Hali ya mtanzania wa leo na yule wa mwaka 60 ni mbaya zaidi. Masikini anazidi kudidimia kwenye umasikini, na matajiri, masultani na wenye madaraka wanaishi kama wafalme.
Tutazidi kuishi kama watumwa kwenye nchi yetu hadi lini?
Tutazidi kuwatumikia watu, hadi lini?
Tutazidi kuishi kwenye ufukara hadi lini?
Tutazidi kuvumilia unyanyasaji hadi?
Tutazidi kunyimwa haki zetu za msingi hadi lini?
Tutazidi kuwaonga wenye nguvu ili kupata haki kwenye mahakama zetu hadi lini?
Tutazidi kuonewa na watu wenye uchu wa madaraka na ulafi usio na kikomo hadi hadi lini?
Ukombozi wa nchi ni lazima iletwe watu wenyewe,na gharama hiyo muda mwingine inakuwa na maisha yetu. Utulivu na amani tunayoidumisha imekuwa ni kama sababu ya wenye madaraka kutunyanyasa ni lazima tujitoe mhanga leo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Nipo tayari kufa leo ili mtoto wangu apate maisha mazuri hapo baadae.Hatuwezi kuwaachia wachache watuamulie tunavyoishi tunavoishi.
Tumechoka na Kikwete, Tumechoka na Makamba, na viongozi wengine walio madarakani. Huu ndio muda wa mabadiliko. Fedha nyingi zimechotwa kwenye hazina ambazo zingewawezesha watoto wetu kusoma bure, lakini wezi hadi leo wapo huru. Baadhi ya vijana walioiba kuku wapo jela kesi zao wala hazijaguswa, mafisadi wapo huru na wanazidi kutumia hela zetu za kodi.
Tumechoka!
Wanamagari ya kurusha maji ya kuwasha,
Wana maaskari wenye bunduki wanaolipwa na kodi zetu,
Wana walinzi wao wanaowalinda tusiwafikie, haina shida.
Lakini sisi tuna mikono mitupu na matawi yanayoashiria amani.
Watuue, dunia yote itashuudia. Lazima tuandamane kudai haki yetu ya kuwachagua tunaowapenda. Uhuru tulishaupata lakini wachache wanatunyang'anya
Ikiwa kudai haki yetu itaitwa uchochezi, basi iwe ni uchochezi, lakini hatuwezi kulazimishwa kuwakubali watu ambao hatukuwachague watuongoze. Kikwete, na mwanae Ridhiwani wanatuona kama wapumbavu. Makamba na familia yake wanaitumia nchi yetu kama shamba lao. Kwa nini tusilalamike?
Huu ndio mda wa ukombozi, lazima vita vya amani vianze. Maandamano ni haki yetu ya msingi, hatutumii silaa ya aina yoyote zaidi ya kuandamana. Watanzania wenzangu, tunaanza maandamano ijumaa kwa wiki moja, ni lazima matokeo yabatilishwe au kura zihesabiwe upya ili wale tuliowachagua watuongoze.
Ikiwa mtu atapoteza maisha yake, genge zima la majambazi, NEC (Jaji makame na kundi lake) Familia ya Kikwete, Makongoro Mahanga na wengine wengi wawajibishwe na kama itawezekana wafikishwe katika makama ya kimataifa. Wao ndio chanzo cha matatizo yote, wamtuchokoza. Bila kuiba kura zetu tusingefikiria kuandamana.Hii itakuwa fundisho, kwa kizazi hiki na vijavyo kwamba anayekubali, kuonewa atazidi kuishi kwenye umasikini na ukiwa
Tupo tayari kupigania kile tunachoamini ni chetu; Haki yetu!!!
Mungu awabarikini wote