Sms ya mdogo wangu akiniomba msamahama

Sms ya mdogo wangu akiniomba msamahama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakuu hawa wadogo zetu wanakoelekea sio kuzuri.Inahitajika busara za ziada kuwarudisha kwenye mstari.

Hii ni sms ya mdogo wangu wa kike miaka 19 akiniomba msamaha baada ya kurudi akiwa pombe mbaya siku ya Pasaka

"caca naomba unixamehe,nimecoxa ctarudya tena maxoca yangu bro.am xory,ni koxa la kwanza"
 
hahahhhahaaaa atakua na undugu na kabila la Nkosa! atakua anatoka kwa Mzee Madiba (RIP)
 
Unakazi ya kuanza kumfundisha kuandika kwanza ndo ije habari nyingine
 
Ha ha ha Mkuu.. Wala sio jambo la kushangaa kwa kuwa utandawazi unasaidia kueneza lugha hizi za mitaani.. Unajua hata sie zamani tulikuwa na maneno ambayo hayakuwa lugha rasmi.. Ila tofauti kubwa wakati wetu hatukuwa na platform ya kutumia lugha kwa maandiko.. So maneno mengi yaliishia kwenye kuongea tu na sio kwenye maandishi.. Siku hizi hawa vijana wana platform za kutosha (social networks & sms messengers) kuandika maneno kwa lugha zao na ndo sasa tunaona sana siku hizi vijana wakiwa wanatumia maneno ya hayo.. hasara ya hii ni kubwa hapo baadae..
 
nachukizwa sana na hii yakutumia haya maandishi ya x kwenye s, for sure kama ni mie hata ikiwa unanipa taarifa ya msiba ukatumia huu uhaini wa lugha nakutukana
 
ilinichukua zaidi ya mwaka na nusu kuelewa neno Hacra kuwa linamaanisha Hasira mpenzi wangu wa kale alipokuwa ananiandikia hizo herufi.. dah...
 
Daaaah yani hamna kitu huwa kinanichefua kama mtu anapoweka x kwenye s. Hata mimi natumia vifupisho ila pale penye maana ya kuweka kifupisho. Mimi nitasema mm, sasa nitasema ss okey nitasema ok. Sasa logic ya kuweka x kwenye s na neno linabaki vilevile kwa idadi ya alphabet ile ile huwa siielewi kwakweli. Xo Xorry
 
Hii ni hujuma kubwa sana kwa lugha zetu, hasa ile ya kiswahili ambayo imeathirika zaidi na matumizi haya mabovu ya herufi! Potelea mbali, mkuu kazi unayo kwa huyo mdogo wako, kwanza unapaswa umfundishe juu ya matumizi ya lugha sahihi, atofautishe maneno anayoweza kutumia kuongea na wewe na ama rafiki yake, mdogo wake na kadhalika, kwa kiigereza wanaiita "stylistics"! Lakini pia umkanye juu ya mienendo yake mibaya kimaadili, hasa katika kipindi chake hiki cha kupevuka kiitwacho "foolish age" wakati mwingine! Ni chungu kutamka, ila ni ukweli, muonye pia dada yetu huyu, inaonekana wazi ameshawajua mabwana!!!!???? Ni hayo tu mkuu.
 
Back
Top Bottom