GE2025 Sms za kukumbusha kupiga kura: Je, ni kuhamasisha au kero kwa wananchi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Katika siku za hivi karibuni, simu za Watanzania zimefurika na ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaosema: “Kura yako ina thamani, kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, hakikisha unapiga kura tarehe 27.11.2024 kumchagua kiongozi unayemtaka kwenye Kijiji, Kitongoji au Mtaa wako.”
Screenshot_20250930_213044_Messages.jpg

Kwa wengine, ujumbe huu ni mwaliko wa kizalendo unaokumbusha wajibu wa kiraia. Hata hivyo, kwa idadi kubwa ya wananchi, SMS hizi zimeibua hofu na maswali mazito. Wengi wanashangaa: “Ni nani anayetoa namba zetu? Kwa nini tusumbuliwe kana kwamba hatujui kuwa kuna uchaguzi?”
images (75).jpeg

Hali hii inaleta mjadala wa faragha ya mtu binafsi dhidi ya haki ya taifa kuhamasisha ushiriki wa kidemokrasia. Ni kweli, kura ni haki na pia ni wajibu. Lakini je, kuikumbusha jamii kwa mafuriko ya jumbe wa simu ndiko kunakoongeza hamasa, au kunazaa kinyume chake kwa kuwafanya baadhi kujisikia wamekwenda bila hiari yao?
images (72).jpeg

Hata hivyo, ukweli unabaki pale pale: kura ni ya mtu binafsi, na ushiriki wa kila mwananchi ni hiari yake. Na kama mtu hataki kwenda kupiga kura hakuja kiwango cha sms ambazo zitatumwa zinaweza kumfanya mtu aende kupiga kura.
images (71).jpeg

Nyie watu wa mitandao, Halotel, Vodafone, Airtel na wengine acheni kutuma sms, watu wanafahamu kuwa kuna uchaguzi.
 
Hizo huwa tunapokea mara moja tu unapiga na block!
 
Katika siku za hivi karibuni, simu za Watanzania zimefurika na ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaosema: “Kura yako ina thamani, kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, hakikisha unapiga kura tarehe 27.11.2024 kumchagua kiongozi unayemtaka kwenye Kijiji, Kitongoji au Mtaa wako.”
View attachment 3481427
Kwa wengine, ujumbe huu ni mwaliko wa kizalendo unaokumbusha wajibu wa kiraia. Hata hivyo, kwa idadi kubwa ya wananchi, SMS hizi zimeibua hofu na maswali mazito. Wengi wanashangaa: “Ni nani anayetoa namba zetu? Kwa nini tusumbuliwe kana kwamba hatujui kuwa kuna uchaguzi?”
View attachment 3481428
Hali hii inaleta mjadala wa faragha ya mtu binafsi dhidi ya haki ya taifa kuhamasisha ushiriki wa kidemokrasia. Ni kweli, kura ni haki na pia ni wajibu. Lakini je, kuikumbusha jamii kwa mafuriko ya jumbe wa simu ndiko kunakoongeza hamasa, au kunazaa kinyume chake kwa kuwafanya baadhi kujisikia wamekwenda bila hiari yao?
View attachment 3481429
Hata hivyo, ukweli unabaki pale pale: kura ni ya mtu binafsi, na ushiriki wa kila mwananchi ni hiari yake. Na kama mtu hataki kwenda kupiga kura hakuja kiwango cha sms ambazo zitatumwa zinaweza kumfanya mtu aende kupiga kura.
View attachment 3481430
Nyie watu wa mitandao, Halotel, Vodafone, Airtel na wengine acheni kutuma sms, watu wanafahamu kuwa kuna uchaguzi.
Do this instead block 🚫 them
Screenshot_20250925_144300_Messages.jpg
 
Kwangu ni kero..
Unakuwa umekaa unasubiri msg ya muamala, unafungua simu mambo ya KURA na TAKUKURU.
 
NI KERO KUBWA MNO KWANGU. Nimeandika kwa msisitizo kabisa.
 
Kimeumana huko 😃 😀 😄
Sikiliza HOMEBOY akitoa somo
 
Back
Top Bottom