Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Yaambiwa hiyo ni kazi ya Bunge
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza kuondoa suala la mafuta ya petroli na gesi asilia kwenye orodha ya mambo ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imesema hawana uwezo wa kuchukua hatua hizo.
Kauli ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, bungeni jana akijibu swali dogo la Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Malima alisema SMZ haiwezi kufikia uamuzi huo kinyemela bila kujadiliwa na Bunge. Zitto alitaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu uamuzi wa SMZ wa kuondoa suala la mafuta yani petroli na gesi asilia kama ilivyotangazwa kwenye Baraza la Wawakilishi na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari jana.
Malima akitoa kauli hiyo inayotafsiriwa kama mwanzo wa mvutano wa serikali hizo, jana wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF, walionyesha furaha yao kwa hatua iliyochukuliwa na SMZ, kuondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano.
Msimamo wa SMZ ulitolewa juzi na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2009/10 katika Baraza la Wawakilishi.
Akieleza furaha yake kwa uamuzi wa SMZ, Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, Ali Suleiman Ali, alisema Baraza la Mapinduzi Zanzibar, linastahili kupongezwa kwa uamuzi liliouchukua kwa vile suala hilo limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu na wananchi kupitia wawakilishi wao.
Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Ali Denge Makame, alisema Waziri Mansour amefanyakazi kubwa kutetea maslahi ya Zanzibar katika suala la mafuta na gesi asilia na anastahili kuitwa dume la mbegu.
Naye Mwakilishi wa Chonga, Abdallah Juma Abdallah, alisema kwa kuwa eneo la Tundaua Kisiwani Pemba ndio lenye dalili ya kuwepo mafuta serikali inapaswa kuanza kuchukua hatua za awali kutengeneza miundombinu ya barabara na maji kabla ya kuanza kukaribisha wawekezaji katika sekta hiyo kwa ajili ya utafiti na uchimbaji.
Hata hivyo, Mwakilishi wa Kitope, Makame Mshimba Mbarouk, alisema hivi sasa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watapumua kwa vile wananchi walikuwa wakiwauliza kila mara kuhusu suala la mafuta.
Mwakilishi wa Mkanyageni, Haji Faki Shaali, alisema hatua iliyofikiwa na Baraza la Mapinduzi, inastahili kuungwa mkono na wajumbe wote kwa vile suala la mafuta na gesi asilia litasaidia kutatua kero nyingi za umasikini zinazowakabili wananchi wake.
Awali Malima alisema Wizara yake imesikia azma ya SMZ na kwa sasa inasubiri taarifa yake ya maandishi na kuiwasilisha katika Bunge hilo ili ijadiliwe kwa kina kwa kuwa chombo hicho ndicho chenye mamlaka ya kutoa uamuzi huo.
Hata hivyo, baada ya swali la Zitto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, aliomba mwongozo wa Spika kwa madai kuwa kile alichoeleza kwamba ni upotoshaji mkubwa uliofanywa na Zitto alipokuwa akiuliza maswali yake.
Katika maelezo yake, Marmo alisema: Zitto ametoa matamshi mawili mazito ambayo yanaupotosha umma, sio kweli kwamba mwaka 1968 hakukuwa na Katiba ya Jamhuri, upotoshaji wa pili alioufanya mheshimiwa Zitto ni ule wa kusema kwamba kwenye Katiba kuna jambo limenyofolewa, naomba mwongozo wako mheshimiwa Spika kwa kumtaka Zitto afute kauli zake.
Hata hivyo, Spika Samuel Sitta, aliokoa jahazi kwa kueleza kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kunyofoa kitu kwenye Katiba isipokuwa Bunge na kumtaka Zitto awe makini katika matamshi yake.
Hakuna Mtanzania anayeweza kunyofoa kitu kwenye Katiba bila Bunge mheshimiwa Zitto uwe makini na kauli zako, yote uliyosema leo ni sifuri na ninakusamehe kwa sababu mwaka 1968 hukuwa umezaliwa, alisema.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Magogoni (CUF), Vuai Abdallah Khamis, alihoji faida ambayo imepatikana kutokana na uchimbaji wa gesi asilia na kuhoji pia kiasi cha faida ambacho kimepelekwa Zanzibar. Akimjibu, Malima alisema hadi Aprili mwaka huu, gesi asilia yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 149.7 imezalishwa kutoka Songo Songo na Mnazi Bay.
Alifafanua kuwa tangu matumizi ya gesi asilia yalipoanza, serikali imeingiza kiasi cha Sh. bilioni 50.8.
Aliongeza kwamba mapato hayo yamekuwa yakiingizwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina ambao unagharimia kazi za Serikali ya Muungano.
:: IPPMEDIA