SMZ yakana kufuja fedha kwa `mashangingi`

SMZ yakana kufuja fedha kwa `mashangingi`

Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema haijatumia fedha za umma kununulia magari ya kifahari maarufu kama mashangingi bali yamepatikana kupitia msamaha wa madeni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika Mtaa wa Vuga mjini Unguja jana.

Juma alisema SMZ baada ya kupata msamaha wa madeni kuna fedha zilipatikana na ndipo ikaamua kuondoa tatizo la huduma ya usafiri hasa kwa viongozi wa kitaifa kwa kununua magari hayo.

``Magari haya hatukununua kwa fedha mkononi bali tulinufaika na msamaha wa madeni na sehemu ya fedha zilizokuwa zipatikane tukashauriwa tunahitaji kitu gani ndipo tukapendekeza kuzitumia kwa kununua magari,`` alisema.

Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo waliamua kununulia matrekta ili kuboresha sekta ya kilimo visiwani hapa na kupambana na umaskini.

Waziri huyo bila kutaja thamani ya magari hayo alisema yaliyonunuliwa ni 80 aina ya Toyota Prado na Rav 4.

``Kwa sasa siwezi kusema yamegharimu kiasi gani naomba munipe muda hadi hapo baadaye, isipokuwa naweza kusema serikali ipo makini katika matumizi ya fedha za umma,`` alisema.

Alifafanua kuwa hali ya huduma ya usafiri kwa viongozi serikalini ilikuwa mbaya hasa kwa Kisiwa cha Pemba na Tanzania Bara ambako baadhi ya viongozi walikuwa wakilazimika kukodi teksi kwa ajili ya safari zao.

``Mfano gari langu lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani na ofisi ya Waziri Kiongozi Pemba haikuwa na gari hata moja na walilazimika kuazima Idara nyengine kwa ajili ya shughuli za kikazi``, alisema.

Tamko hilo la Serikali ya Zanzibar limekuja kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kuilalamikia SMZ kwa kufuja fedha kwa kununua mashangingi badala ya kutumia kuboresha huduma jamii ikiwamo afya na elimu.

SOURCE: Nipashe

Hawa SMZ waache ujinga; Kibu, Mwiba mko wapi? Yaani Zanzibar kuna haja ya kununua Prado? Kwa mwendo wa kwenda wapi, Dodoma? Visiwa vya Zanzibar hata wakinunua Suzuki Escudo zinawafaa sana. Yaani wameambukizwa ujinga wa Serikali ya CCM kuacha kujenga barabara ili wanunue Land Cruisers!
 
Magari anayozungumzia huyo Waziri ni vitendea kazi- hivyo ni neccessity na siyo luxury. Magari naamini kuwa ni vitendea kazi kama ilivyo simu, kalamu na vyenginevyo hivyo magari (yanayoendesheka) ni muhimu kwa Watendaji wa Serikali, ili Serikali ifanikishe majukumu yake. Kuhusu priorities kama za Elimu . Hiyo ina programme yake ya muda mrefu na mfupi. Hebu durusu alelezayo Mh. Waziri wa Elimu (Bw. Haroun) . Lipo hata la kuboresha Karume Tech. College iwe Chuo Kikuu cha Ufundi. Mipango yote hiyo inaratibiwa na ina mafedha yake kutoka ndani na kwa Wafadhili. Sasa itasimamiwa na kutekelezwa vipi ikiwa Bw. Haruna mwenyewe anategemea usafiri wa mkweche? Bw. Mkweli kuwa Mkweli na uone Ukweli.

Pakacha ustake kudanganya watu au kutetea matatizo ya serikali.
Sio magari yote ys SMZ yalikuwa ni mabovu, nyingi ya gari zilikuwa zinahitaji marekebisho ya madogomadogo. Tukiangalia kwa undani zaidi utagundua hizo gari zinapelekwa service uchochoroni, kinawekwa kifaa kibovu then dereva anapeleka risiti ya malipo ya kifaa kipya, sasa pakacha kwa ubwege huu wa msimamizi wa gari/dereva na hao anaokula nao unafikiri gari litakuwa zima kila siku?lazima litaia km ndani kuna panya!!!!

Halafu lazima tuwe wakweli hata km tunafanya kazi serikalini; saa 4 za usiku unakutana na gari la waziri kule forodhani au pale nyuma ya Afrika house hotel kisa anawapeleka watoto au mke wake kwenda kula mishkaki au urojo; je hayo ni matumizi mazuri ya rasilimali za nchi?wakati gari yake ameipaki barazani mwake?

N.B. Gari ya Harun Suleyman ni Prado ya cku nyingi tu tena ipo bomba sana, kama alishindwa kutekeleza majukumu yake ya kusimamia masuala ya elimu ipasavyo,huo utakuwa ni uzembe wake si kusingizia hakuwa na gari ya uhakika!!!!

Thnx
 
Zenj ni sehemu ndogo sana!

Magari kawaida tu yanatoshao...hivi toka Chanjaani kufika Macho Manne ..tunahitaji pajero?
 
Aljunior usiwe junior nawe. Kutokana na hilo tatizo la matengenezo ya uchochoroni ambayo yanakula fedha sana, ndiyo maana zinaletwa XTR Rav 4 sasa kuna uchochoro gani hiyo modern gari itatakiwa ikatiwe nati. Nati yake si itakuwa ile ile tu inayoweza kupatikana Shirika la Magari (ambalo litakuwa na package ya spare parts kutokana na ununuzi huo mkubwa). Kutokana na tatizo la kukutwa gari hizo unazosema usiku vichochoroni , ndio maana Hao viongozi sasa wanapewa SUV na sio saloon. si waweze kuonekana vizuri wakizitumia hizo gari vibaya? Al junuior Rav 4 XTR ni £19,000 tu na utaendesha miaka mitano hata tairi hujabadilisha. Achana na magari mabovu - na hilo tatizo la ubadhirifu wa gereji za vichochoroni litakufa kabisa. Kila ifanyacho Serikali sio kibaya Bwana. Kuna mengine ni mazuri tu na yana nia njema.
 
Zenj ni sehemu ndogo sana!

Magari kawaida tu yanatoshao...hivi toka Chanjaani kufika Macho Manne ..tunahitaji pajero?
Kumradhi yakhe sasa Waziri unataka afanye kazi zake kwa kutmia Citroen Berlingo, Renault Kangoo au Ki-Martiz. Acha utani Bwana.
 
Hawa SMZ waache ujinga; Kibu, Mwiba mko wapi? Yaani Zanzibar kuna haja ya kununua Prado? Kwa mwendo wa kwenda wapi, Dodoma? Visiwa vya Zanzibar hata wakinunua Suzuki Escudo zinawafaa sana. Yaani wameambukizwa ujinga wa Serikali ya CCM kuacha kujenga barabara ili wanunue Land Cruisers!
Acha kufuja watu Bwana. Na inabidi uwe na tabia ya kusoma mambo vizuri na kwa utuo. Wamesema kuwa wamenunua magari- kati ya hayo yapo machache (kama matano tu) ya aina ya Prado nayo ni kwa ajili ya shughuli zao wakiwa Bara (Si ndio hizo za kwenda Dodoma?) au wakiwa huko unataka wakubembelezeni nyinyi muwape lifti? Gari nyengine ni Toyota RAV 4 XTR. Sasa wewe unasema Suzuki Escudo. Hivi kweli unaelewa magari? Mimi nawapongeza kwa kufanya utafiti mzuri na kununua gari za kuaminika siyo mitumba kama iliyokuwa ikiletwa huko nyuma katika tawala zilzizopita.
 
Hivi hawawezi kusema kitu bila kuingiza Tanzania Bara? Sitashangaa wakibanwa wakija sema kuwa walinunua hayo mashangingi kutokana na shinikizo kutoka serikali ya Muungano!

Du ivo huwezi kunyamaza kila inapotajwa Tanzania Bara? Hisia zitakupotowa. Tanzania Bara SMZ ina ofisi zake na hutumia gari zake na hilo ndilo lililosababishwa kutajwa Tanzania Bara na si kwa sababu nyengine
 
Acha kufuja watu Bwana. Na inabidi uwe na tabia ya kusoma mambo vizuri na kwa utuo. Wamesema kuwa wamenunua magari- kati ya hayo yapo machache (kama matano tu) ya aina ya Prado nayo ni kwa ajili ya shughuli zao wakiwa Bara (Si ndio hizo za kwenda Dodoma?) au wakiwa huko unataka wakubembelezeni nyinyi muwape lifti? Gari nyengine ni Toyota RAV 4 XTR. Sasa wewe unasema Suzuki Escudo. Hivi kweli unaelewa magari? Mimi nawapongeza kwa kufanya utafiti mzuri na kununua gari za kuaminika siyo mitumba kama iliyokuwa ikiletwa huko nyuma katika tawala zilzizopita.

Asante Mkuu. Lakini unapajua Dodoma weye? Mimi magari nayajua vizuri na ninayo! Labda huwa hawaishii Dodoma, wanafika hadi Kigoma, barabara ya Dar- Dodoma hata Corolla Limited inaenda tena bila shida yoyote. Kama wanaenda hadi Shinyanga au Kigoma basi Prado inafaa sana lakini kama ni Dodoma tu, I doubt.
 
Hivi ukisamehewa madeni unalipwa feza ? Jamani aliefahamu hebu anifahamishe hapa kwenye mahesabu ya wakubwa ?

Kama niliona kuwa waliulizwa wanataka kitu gani na wakaamuwa magari. Pengine kama ni mlipaji mzuri inawezekana ukawa umeshaanza kulilipa lile deni na Bwana akaamuwa akusamehe deni zima bila shaka hicho ulichokianza kulipa unaweza ukaulizwa upewe nini kwani fedha isiyo na mpango maalum inajulikana kwetu itarudi mifukoni mwa watu.
 
Mwiba,
Unaona RAHA YA KUUWA MUUNGANO? Umepiga kelele wee jinsi tunavyowaibia na kusema sisi Wabara tulivyo wa ovyo. Sasa hata hii hamkujua kama siyo CHADEMA. Kama mnafikiri Muungano ukifa basi UFISADI utaisha Zenji, kwa kweli mlie. Kwa hili swla NAIPONGEZA SMS kwa kuonyesha waziwazi kuwa UFISADI hauna Ubara wala U-Zanzibar.
Nashindwa kujua kwa nini wasingelinunua RAV4 80 na Prado 4. Halafu magari hayo yote ni lazima yanunuliwe kwa mpigo? Ili yaishe yote? Hapo utakuta wamenunua Matrekta 3 ili kusema tumenunua magari na matrekta. Duu, uchaguzi unakaribia. Wakiuziana kwa bei chee, na baadaye wayauze kwa bei juu, zitatosha kwenda kiwandani na kushonesha T-SHIRT za kijani na mashati yenye alama ya JEMBE NA NYUNDO.
Na hapo subirini MAFUTA yapatikane. Wataanza kununua hadi ndege/helkopita za serikali kwani kuja Dar kuna foleni kubwa sana BAHARINI.

CCM kule haina utaratibu wa kuchangiwa kwa fedha za ufisadi, hizo ni fedha za vigogo tu. Michango ya shughuli za CCM inatoka serikalini na wafanyabiashara wanaotaka kupata baraka ya kuendelea na biashara visiwani,
 
Kama niliona kuwa waliulizwa wanataka kitu gani na wakaamuwa magari. Pengine kama ni mlipaji mzuri inawezekana ukawa umeshaanza kulilipa lile deni na Bwana akaamuwa akusamehe deni zima bila shaka hicho ulichokianza kulipa unaweza ukaulizwa upewe nini kwani fedha isiyo na mpango maalum inajulikana kwetu itarudi mifukoni mwa watu.

Unatuambia kuwa kama wanadaiwa milioni 50 dola za kimarekani na kwa bahati nzuri madeni yakasamehewa ,wakati wanasamehewa walikuwa wameshalipa dola 25 milioni ,kwa maelezo yako nilivyoyafahamu kuwa unaposamehewa hata zile ulizokwisha lipa unarudishiwa au nimefahamu sivyo ?

Basi kuna watu hapo mwanzo walikuwa wakitia ndani fedha ,itabidi tutazame yale mdeni yote tuosamehewa miaka ya nyuma tokea akina Mwinyi ,fedha iliyosamehewa waliifanyia nini ? Kama ndivyo usamehevu wenyewe ulivyo,inaonyesha wazungu wamesituka kurudisha kitita na badala yake wamekuja na mpya ,kiasi jamaa waagize magari.
 
Nchi itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno,

Waziri anasema kuwa pesa ni za madeni yaliyosamehewa hivyo sio za wananchi ila ni misamaha, kumbe waliposamehewa waliletewa cash na wao wakaona wakanunue mashangingi?

Kuna haja waliopo kwenye Baraza la wawakilishi na haswa CUF kuhoji kama hizo zilikuwa kwenye bajeti ya serikali ama laa na kama hazikuwepo hilo fungu wamelichota wapi? je? walipanga kulipa madeni kiasi gani kwenye bajeti ya mwaka huu?na ni madeni gani?
 
Ndugu yangu unafahamu mantiki ya maintenance, unafahamu nini uchakavu. Jee unafahamu kuwa ku-maintain gari chakafu ni bora kununua mpya ukaachana na chakafu.Jee una fahamu kuwa life-span ya magari (hasa haya yanayotengenezwa siku hizi) ni miaka isiyozidi mitano. Jee unajua hayo magari anayozongumzia Mh. Hamza yana umri gani? (wa uchakavu) Na hata hayo mashangingi wanayopanda Mawaziri na makatibu Wakuu (Toyota Crecida nyeupe na za bluu zilizonunuliwa tokea wakati wa awamu ya kwanza ya Salmin) zina umri gani?. Unajua kuwa Toyota Company sasa hata Crecida hawatengenezi tena. Usilaumu tu angalia pande zote.

Rafiki yangu PAKACHA nakubaliana na wewe kuwa kuna umuhimu wa kununua hayo magari LAKINI ipo haja ya kusema utumbo aliousema Waziri? Unaposema pesa za Umma una maana gani? hivyo msaada ulioletwa kwa ajili ya Umma si wao?
Hakukuwa na sababu ya kupinga kuwa pesa ni ya umma au la bali kuwafahamisha Wananchi sababu za uamuzi wa kutumia pesa za umma kwa masilaha ya umma. Kwa hesabu ndogo tu huko kwenu magari ya mawaziri yanaweza kupakia hata watu wa chini kama mimi, hakuna ubaguzi, hiyo si faida.
Viongozi wenu wawe makini na kuacha kukurupuka kujibu maneno ya wapinzani for the sake of kujibu tu. Hebu jaribuni kugawa hayo mashangingi kwa vyama vyote ikiwa na upinzani kama watayakataa eti hizo pesa zingekwenda kwenye Elimu. Mbona wanapiga keklele kwa ruzuku hawasemi ruzuku iende kwenye elimu?
 
Aljunior usiwe junior nawe. Kutokana na hilo tatizo la matengenezo ya uchochoroni ambayo yanakula fedha sana, ndiyo maana zinaletwa XTR Rav 4 sasa kuna uchochoro gani hiyo modern gari itatakiwa ikatiwe nati. Nati yake si itakuwa ile ile tu inayoweza kupatikana Shirika la Magari (ambalo litakuwa na package ya spare parts kutokana na ununuzi huo mkubwa). Kutokana na tatizo la kukutwa gari hizo unazosema usiku vichochoroni , ndio maana Hao viongozi sasa wanapewa SUV na sio saloon. si waweze kuonekana vizuri wakizitumia hizo gari vibaya? Al junuior Rav 4 XTR ni £19,000 tu na utaendesha miaka mitano hata tairi hujabadilisha. Achana na magari mabovu - na hilo tatizo la ubadhirifu wa gereji za vichochoroni litakufa kabisa. Kila ifanyacho Serikali sio kibaya Bwana. Kuna mengine ni mazuri tu na yana nia njema.

Pakacha

Inaonekana hujui unachotetea, hizo rav 4 xtr hamna kitu kabisa kwa mazingira ya znz. Barabara nyingi km si zote ni mashimo matupu, ukiangalia structure ya hizo gari haziwezi kuhimili mikikimikiki ya barabara za huku, ukiangalia chasis zipo chini sn.
Pakacha unashindwa hata na wanawake hawa? wiki 2 zilizopita nilikwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya magharibi (DC West) kule Mwera. Mheshimiwa amepata hiyo rav 4, sasa ktk mazungumzo ya kina mama ktk ile ofisi wakaanza kusema kwa ununuzi wa aina ile za gari serikali imechemsha!!! na hasa kuwapa wakuu wa wilaya na mikoa, kwani mazingira yetu ya huku haziwezi kuhimili, zitaharibika kwa haraka, wakasema ni bora hata wangeletewa Defender new model ingekuwa ni bora zaidi. Hawa ni kina mama na kwa kuwaagalia hawana hata elimu ya chuo kikuu km uliyonayo wewe ambae huna mtazamo wa ndani zaidi uanaangalia ncha ya pua yako ilipoishia.

Kwa magari hayo nakupa sn ikizidi ni miaka 2 km zitadumu.

N.B. Simaanishi km wanawake hawana upeo mpana wa fikra (samahani)
 
Unatuambia kuwa kama wanadaiwa milioni 50 dola za kimarekani na kwa bahati nzuri madeni yakasamehewa ,wakati wanasamehewa walikuwa wameshalipa dola 25 milioni ,kwa maelezo yako nilivyoyafahamu kuwa unaposamehewa hata zile ulizokwisha lipa unarudishiwa au nimefahamu sivyo ?

Basi kuna watu hapo mwanzo walikuwa wakitia ndani fedha ,itabidi tutazame yale mdeni yote tuosamehewa miaka ya nyuma tokea akina Mwinyi ,fedha iliyosamehewa waliifanyia nini ? Kama ndivyo usamehevu wenyewe ulivyo,inaonyesha wazungu wamesituka kurudisha kitita na badala yake wamekuja na mpya ,kiasi jamaa waagize magari.

Hiyo inawezekana na ndio maana wakubwa wakaamuwa warejeshe kwa kufanya kitu cha miradi kwani ikrejeshwa feza hakuna anayesema imerejeshwa kiasi gani. Sasa kwa kuona Vigogo wasikose kabisa ndio wakaamuwa waletewe magari na baada ya kipindi kifupi magari hayo wataweza kujiuzia kwa bei ya chee, si dili hilo?
 
Du ivo huwezi kunyamaza kila inapotajwa Tanzania Bara? Hisia zitakupotowa. Tanzania Bara SMZ ina ofisi zake na hutumia gari zake na hilo ndilo lililosababishwa kutajwa Tanzania Bara na si kwa sababu nyengine

Unashangaa nini? Sijawahi kuficha kuwa mimi ni chogo. Mwenzako Kibunango ameisha nijibu. Na nilimshukuru kwa kunifahamisha. Hakukuwa na haja ya wewe kurudia jibu lake.
 
Unashangaa nini? Sijawahi kuficha kuwa mimi ni chogo. Mwenzako Kibunango ameisha nijibu. Na nilimshukuru kwa kunifahamisha. Hakukuwa na haja ya wewe kurudia jibu lake.

Usikasirike YAGHE! Hiyo inatokana na namna tunavyoingia kwenye mtandao. Hata hivyo unapoingia ukumbini na silaha ndipo unapokaribisha mapambano. Hata kama ulijibiwa lakini aliekujibu hakukueleza kuwa jizuie na hisia katika majadiliano kuwa Chogo au mdebwedo kusitufanye tusitumie busara.
 
Pakacha

Inaonekana hujui unachotetea, hizo rav 4 xtr hamna kitu kabisa kwa mazingira ya znz. Barabara nyingi km si zote ni mashimo matupu, ukiangalia structure ya hizo gari haziwezi kuhimili mikikimikiki ya barabara za huku, ukiangalia chasis zipo chini sn.
Pakacha unashindwa hata na wanawake hawa? wiki 2 zilizopita nilikwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya magharibi (DC West) kule Mwera. Mheshimiwa amepata hiyo rav 4, sasa ktk mazungumzo ya kina mama ktk ile ofisi wakaanza kusema kwa ununuzi wa aina ile za gari serikali imechemsha!!! na hasa kuwapa wakuu wa wilaya na mikoa, kwani mazingira yetu ya huku haziwezi kuhimili, zitaharibika kwa haraka, wakasema ni bora hata wangeletewa Defender new model ingekuwa ni bora zaidi. Hawa ni kina mama na kwa kuwaagalia hawana hata elimu ya chuo kikuu km uliyonayo wewe ambae huna mtazamo wa ndani zaidi uanaangalia ncha ya pua yako ilipoishia.

Kwa magari hayo nakupa sn ikizidi ni miaka 2 km zitadumu.

N.B. Simaanishi km wanawake hawana upeo mpana wa fikra (samahani)
Duh. Kushindwa na wanawake ni fakhari kwangu mimi. Kwani hata dada zangu wamenipita katika kila hali na nafurahia jambo hilo. Nenda katika website za Land Rover UK - English - Home, www. toyota.co.uk, na www. whichcar?. co.uk na fanya comparison. Lakini usidharau wanawake na kupinga ukweli kwamba wanaendelea kuwa (kuwa bora) mbele yetu sisi wanaume wenye majivuno kama wewe.
 
Wakuu, mtanisamehe lakini nashindwa kabisa kuelewa mnachozungumza hapa..
kuna watu wanadai kuwa kusamehewa madeni ni pamoja na kurudishiwa fedha ambazo umekwisha lipa ktk deni..
Hivi kweli mnafahamu misaada (aids) inavyotolewa na hata kuitwa DENI na likafikia kusamehewa kama deni..
Ebu nambieni mathlan Wachina wametupa msaada ya billioni 1 ktk ujenzi wa uwanja wa Aman na tumewahi kulipa millioni 500 interest pekee ni millioni 350, unafikiri kweli tukisamehewa deni tutarudishiwa millioni 500 na uwanja wa Aman tumeupata bure..Nani anakudanganyeni jamani!

Na hata tukifikiria hivyo, hizo millioni 500 zilizolipwa mwanzo zilitoka wapi?..Hivi ktk accounting utaweza vipi kimahesabu kufuta hilo deni ktk kitabu cha madeni bila kuweka transaction inayohusiana na matumizi ikiwa fedha hizi sio za wananchi..
Mwiba mkuu tumeibiwa, tunaposema afadhali ya mkoloni ni kutokana na mambo kama haya!.. Hata huyo Sultan hakuwafanya ujinga wa kiuchumi kama huu..Ukombozi wa kifikra wakati unadidimizwa kiuchumi ni utumwa mbaya zaidi sawa na ule wa kutengwa..
 
Kwa ushauri wa fasta, ilikuwa ni bora hao SMZ kununua vespa na batavuzi. Maanake pale stone town barabara ni nyembamba mno kwa magari kupita. Aidha ilikuwa ni vema kwao kumpa tenda tena Raza awaletee magari, kama alivyowahi kufanya katika awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom