Makaayamawe
JF-Expert Member
- Feb 21, 2009
- 341
- 9
SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi
Na Salma Said, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mkakati mpya wa kuwataka wawekezaji na watu wenye asili ya Tanzania Bara kusajiliwa na kuanza kulipa kodi ya ardhi ya dola za Marekani 5000 (Sh6.5 milioni), kila mwaka kwa kila hekta moja ya ardhi.
Hata hivyo, SMZ ilisema mwekezaji mwenye asili ya Zanzibar atapaswa kulipa dola 500 (Sh650,000).
Mpango huo umetangazwa jana na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Mohammed Hashim Ismail kufuatia bodi hiyo kupewa uwakala wa kusimamia na kukusanya kodi ya ardhi.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992, Mzanzibari tu ndiye mwenye haki ya kumiliki ardhi, lakini wageni wote wanapaswa kukodishwa wakiwemo watu wenye asili ya Tanzania Bara.
Hatua hii itatuwezesha pia kuwafahamu wamiliki wote wakubwa na wadogo wadogo wa vipande vyote vya ardhi hapa Zanzibar pamoja na wale ambao wanatajwa kuhodhi maeneo kinyume na utaratibu, alisema kamishna huyo.
Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwatambua wasiokuwa Wazanzibari na kuishauri serikali kuchukua hatua zinazofaa.
Kamishna huyo alisema viwango vya malipo vitapitiwa upya ili viende na wakati na kuishauri serikali juu ya hatua sinazostahili kuchukuliwa.
Alisema ardhi ni suala muhimu katika kupambana na umasikini na kukuza uchumi wa Zanzibar, ndio maana serikali imeamua kuhakiki upya viwanja vya makazi kupitia mradi wa SMOLE.
Kamishna huyo alisema kupitia mradi huo taarifa zote zitaingizwa katika mfumo wa kompyuta ili kuweza kuwatambua watu wote waliokodishwa ardhi.
Hashim Ismail alisema kwamba bodi ya mapato imeanza kujitayarisha kwa ajili kukusanya fedha hizo pamoja na kuwatambua waliopewa ardhi kinyume cha sheria. Hata hivyo zoezi hilo linatarajiwa kuibua mjadala mkubwa kutokana na ukweli kwamba, inachochea ubaguzi kati ya Watanzania Bara na Wazanzibari hivyo kuendelea kuudhoofisha muungano.

Last edited by a moderator: