SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi


And that is the pwoint ,msitutishe na kuzama wacha tuzame kwani sisi tutakuwa sio wa kwanza ,lakini kutuzalilisha hilo halikubaliki.
 
better leave Zanzibar total autonomy to the Zanzibar President. That will be the best for both Tanganyika and Zanzibar.
That will be the best for both Tanzania (siyoTanganyika) and Zanzibar. Na hivi ndivyo Muungano kama tunazungumzia ule wa 1964 ulivyotaka iwe. Isipokuwa kuna mambo (machache) yameainishwa kuwa yatakuwa katika milki ya Jamhuri ya Muungano (Rais wa Jamhuri ya Muungano.) Sasa nani katufikisha hapa tulipo sijui. Hivyo, wanaodai hiyo autonomy nafikiri wanataka turudi katika azma yetu ya awali na siyo kuelekea katika mawazo ya ndotoni.
 
vile vile WaTanzania Bara huwa hatuelezi vizuri kwa nini hatukubaliani na kwa Wazanzibar kuwa na total Autonomy; sisi hufikiria tu kuwa ati ni kujitenga. There are issues to compromise, hawa watu wamekuwa chini ya muungano since 1964 na hamna mafanikio waliyoyapata ila ni kudidimia tu. Better to have a referundum; labda Tanzania ikubali on only one issue; on Muungano on defence with a Senior General for Zanzibar who have to be under a comand of the Chief Of the Defence of URT. Other issues give them autonomy what to practice including those policies which influence social political and economic development. Sometimes we have to agree, the smaller the better and easier to organize.
 
As long as CoAF ni raisi wa Muungano,

Mambo madogo madogo ya Visiwani basi waamue huko2 visiwani!
 
Hapana, ni sahihi kabisa kwani wanatutafuta wabara bila sababu. Waende wakagombane wao kwa wao nyumbani kwao, wakishapatana warudi tuungane. Wakiridhia huko visiwani, wawelezaji wa kipemba nao walipe $5,000 kwa kila hekari ya ardhi Tanzania Bara

Sasa wapemba walipe $5000 kwa kila hekari ya ardhi Tanzania Bara kutumia sheria ya nchi gani? Tanzania Bara au JMT?, tangu lini umesikia kuna nchi inaitwa Tanzania Bara, hapa tunarudi pale pale - Serikali ya Tanganyika irudishwe na iyashughulikie masuala kama haya, sasa ugumu uko wapi jamani?, au munawataka kuwafanyia wazenji "change bin change"? - weshashituka wapemba wamekaza makalio sasa.
 

Wewe, munabembeleza kwa sababu munajua munaweza kufaidika baadae na rasilimali zilizopo offshore Zanzibar hivyo lengo ni kuibembeleza Zanzibar na kuivunja nguvu kidogo kidogo mpaka ikubali kuwa mkoa, sasa angalia uhamiaji wa watanganyika kwenda Zanzibar - is it just a coincidence au ndio mbinu za kuongeza idadi ya wazanzibara ambao huko mbele watakuja kusaidia kupunguza kasi ya hisia za kizanzibari?, siwezi kuiita hii mbinu ethnic cleansing lakini naweza kusema ni ethnic neutralization, wapemba waliopo Buguruni hawafikii hata 1% ya wadanganyika wakati wazanzibara waliohamia zanzibar baada ya kuondolewa hati za kusafiri wanaweza kufikia hata 10% ya wazanzibari, tembea zanzibar na utashangaa, wamejazana kweli kila unakopita unaisikia accent ya kibara utadhani upo Manzese, halafu wengine sasa wamekuwa na kiburi cha hata kuwabughudhi wazawa asilia, angalieni hapa tunaweza kuja kuwa na Rwanda nyengine Zanzibar kati ya wazanzibari na wazanzibara.
 

Kasome historia na utajua asili ya wazanzibari. Kila mtu pale visiwani ni muhamiaji na kutokana na uhamiaji huu ndio Uzanzibari umekuja, asilimia kubwa ya Wazanzibari wala hawajui asili yao imetokea wapi, umetokea mchanganyiko mkubwa tu na huu ndio uzanzibari, kama una rafiki yako mzanzibari hebu muulize yeye kabila gani? asilimia kubwa ya wazanzibari halisi hawajui haya mambo ya makabila. Uzanzibari ulivyo ni kwamba unamkusanya kila mtu ambae ana mizizi ya kifamilia kule huyu anaweza akawa mndengereko, mzaramu, msukuma,muarabu, mshirazi, muhindi etc na wala haumbagui mtu. Usitake kuleta siasa za Pan Africanism za 1960s ambazo ndio zimetuleta hapa, kama unahisi watu wenye asili ya kiafrika tu ndio wenye haki zaidi Zanzibar basi kwanini usiende Kenya kudai haki zako as well?, au hata Comoro?, kama si huu muungano ungeliweza hata kutoa kauli kama unayotoa leo? Zanzibar ni ya wazanzibari na wenyewe wanajuana.
 

Na nyinyi mumezidi mbona Wazanzibari hawalalamiki wanapowekewa vikwazo kama hivi, kwanini gari zinazosajiliwa Zanzibar zinachukuliwa kama gari zilizosajiliwa nchi nyengine na zikiingia Bara basi zinalipa kila kitu kama gari za Kenya au Uganda. Kwa nini wanalipa kodi bandarini Dar wakiingiza mizigo yao na kwanini wanasachiwa mizigo yao kama wanavuka mpaka kuingia nchi nyengine? au ndio vile tena mkuki kwa nguruwe?. Waacheni na wao wakupeni taste of your own medicine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…