Hakuna cha jazba, ndugu yangu.
Hii sheria mpya tunayoijadili ( na si historia) haitofautishi kiwango anacholipa asie raia wa Tanzania ( Mfilipino na wengine) na mtanzania bara. Wote wanatakiwa kulipa dola 5000 kwa mwaka kwa hekta. Sasa utasemaje kuwa hauwatengi kama wewe mwenyewe umewaweka kundi moja na hao wageni? Talk is cheap. Hatuwezi kuuenzi Muungano kwa maneno tu wakati tunafanya vingine kwa matendo!
Tangu lini mshirazi amekuwa ana asili ya Zanzibar kuliko mtanzania bara? Kwani wakina Seyyid Said walipokuja hawakukuta watu? Na hao watu walitokea wapi? Na nauliza hivi, si kwa jazba, bali kutaka kuelewa. Maana naona inaelekea huo uzanzibari ni haki ya washirazi na wengine ( wenye asili ya bara, ungazija n.k.) wanafanyiwa feva tu!
Unasemaje watanzania bara watamiliki ardhi wakati unawawekea viwango ambavyo ni usury!
Au unataka wakae huko kitwana maana kazi zote za maana mmeishasema wapewe upendeleo wazanzibari. Na huko tena watanzania bara wamewekwa kundi moja na wasio watanzania.
Hapana, Mkuu. Ni vitendo vyenu vinavyotuambia kuwa huu Muungano ni gelesha tu. Unathaminiwa mnapofaidika lakini mnapoweza mnautumia kuwakomoa watanzania bara!
Amandla....