Snoop Dogg na Mike Tyson waingia ubia kuwekeza kwenye kilimo cha bangi

Snoop Dogg na Mike Tyson waingia ubia kuwekeza kwenye kilimo cha bangi

GTA

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
878
Reaction score
651
miketysonsnoopdogg.jpeg
Mwanandondi huyo mambaye kwa sasa amefungua shamba la ukubwa wa ekari 40, kwa ajili ya kilimo cha bangi, amejiweka karibu na mwanamuziki Snoop ambaye nae tayari anafanya shughuli za uzalishaji wa bangi, ili kujifunza namna sahihi ya kuendesha kilimo hicho na kupewa ushauri wa aina sahihi ya bangi anayotakiwa kulima.

Chanzo kimoja kimeeleza kuwa Snoop amemtafuta Tyson na kumpa maelekezo ya aina ipi ya bangi anayopaswa kulima.

Alikuwa amewekeza kiasi cha dola za marekani milioni 25 kwenye bangi hata kabla ya jimbo la Carlifonia halijaruhusu matumizi yake, kwa hiyo anajua kwa undani uzalishaji wake.

Snoop ambaye anataka kufungua maduka ya bangi aliwahi kulieleza gazeti la Daily Star la nchini Marekani kuwa, anaamini kuwa uwekezaji kwenye bangi unaweza kumaliza migogoro yote duniani.

Alisema Ninahisi kwamba watu wengi wanavyozidi kuitumia ndivyo amani inavyozidi kuongezeka.
Jack-in-the-Box-8-Lightened.jpg
Habari zimeeleza kuwa Snoop ameungana na mghahawa wa Jack in the Box kuwapa wateja wake ofa ya bangi
 
Bangi ikiruhusiwa Tz Kama kilimo/zao la biashara,watu wengi watalima bangi matokeo yake kutakuwepo na uhaba was chakula nchini...nishawahi kushuhudia watu wakiuza na kununua bangi iliyokaushwa na kisadolini (kitini) kimoja kilikuwa kinauzwa Tsh 50,000/=
Kama mkulima akipata visadolini 300 kwa msimu mmoja anaweza kutengeneza fedha nyingi sana,lkn tusisahau kuwa INA madhara kiafya!
 
Niliwahi sikia Kijana mmoja akisema hapendi huo Mmea utajwe vibaya, kwakuwa hauna shida wala tatizo lolote ila Watumiaji wa Mmea huo ndo wenye matatizo..,
Nilikuwa sijamwelea ila hivi sasa kama kuna kapicha Fulani kanakuja hivi!!!
 
Niliwahi sikia Kijana mmoja akisema hapendi huo Mmea utajwe vibaya, kwakuwa hauna shida wala tatizo lolote ila Watumiaji wa Mmea huo ndo wenye matatizo..,
Nilikuwa sijamwelea ila hivi sasa kama kuna kapicha Fulani kanakuja hivi!!!
aah kapicha kapi mkuu
 
Back
Top Bottom