Soccer Arena: The Way Forward

Soccer Arena: The Way Forward

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
Tumekuwa tukishuhudia michezo mbalimbali ikifanyika kwenye sub standard sports arena katika nchi yetu. Na hii inatokana na labda kutokuwa na financial resources au ni utashi tu wa wahusika wetu. Kwa mfano sasa hivi utaona wasanii wetu wanavyo hangaika kwenye campaign za uchaguzi wakizunguuka nchi nzima ili kuhamasisha watu na hasa vijana wajitokeze kwa wingi kwenye campaign hizo. Pamoja na jitihada zao bado hawajajengewa kumbi mbalimbali za kuonesha sanaa zao( Performing Art Centers or Stages) mara chaguzi zinapokwisha.

Kama tatizo ni meagre financial resources, yapo mashirika ya uMma yenye uwezo mkubwa kifedha yangewekeza kwenye sports erena hizi na kuwa kama vitega uchumi vyao na kututoa kwenye aibu hii ya kuwa na viwanja vibovu na hasa kwenye mpira, mchezo ambao hupendwa na watu wengi. Na hapa napenda kuipongeza Azam kwa kuonyesha mfano mzuri wa uwekezaji kwenye sector ya michezo pale walipojenga Azam Complex pale Chamazi.

Makampuni ya uchimbaji madini kama Geita Gold Mines na Mwadui Diamond Mines yangebanwa kwenye kipengengele cha Cooperate Social Responsibility kufanikisha hili na sio kutuachia mashimo tu.
Mashirika ya umma NSSF, TPDC, BBC e.t.c. nayo yangeweza kuwekeza kwenye jambo hili kama sehemu sehemu ya vitega uchimi vyao. Halmashauri mbalimbali vilevile zingewekeza kupitia mikopo ya riba nafuu yenye udhamini wa serikali.

Kwa wenzetu viwanja vingi vya michezo humilikiwa na makampuni makubwa kama ilivyo kwenye mchezo wa basketball ambapo katika Jiji la Los Angeles, kampuni Stapples humiliki uwanja huo. Ukienda Sacramento kampuni ya Arco na Dallas ni kampuni ya American Airlines. Na michezo mingine ni hivyo hivyo. Kwenye kabumbu, uzuri wa mchezo hutegemea sana na kiwanja chenyewe na hapa naongelea pitch.
 
Back
Top Bottom