Social credit company ni kampuni ya ukweli au magumashi?

Social credit company ni kampuni ya ukweli au magumashi?

Jamani naomba kufahamishwa zaidi kuhusu kampuni iitwayo SOCIAL CREDIT COMPANY ambayo imejinasibu kutoa mikopo kwako mtanzania yeyote kwa masharti nafuu kabisa!
Je hii kampuni ipo na kama yupo aliyefaidika NAYO anijuze tafadhali.
Ahsante sana.
 
Kutoa mikopo huna haja ya kibali cha BOT kwakuwa unatumia fedha zako mwenyewe.

Ukianza kukusanya pesa ya wananchi hapo ujue BOT inakuja fasta kukuchukulia hatua kali sana!!!!

Mbona wanakusanya hiyo ya kiingilio"?
Au BOT, M PESA NA TIGOPESA wanapata chao kuwadhulumu masikini was Tz?
 
Hawa ni 419

Msijaze hizo fomu hata kidgo!

Kuna viashiria vingi vinaonyesha kuwa ni matapeli na ama wanataka kuchukua details zako + accnt number ili wanunue vitu online au hiyo ada wanayoitaka, watu mia wakiwatumia....wana hela ndefu!

-fomu haina address, simu wala email au kuonyesha wapi walipo!
-kwanini watumie nembo ya taifa kama logo?
-Katika maelezo yao wameweka address na contacts, lakini number za simu ya meneja (landline) sio za mnazi mmoja, ni location ya posta! Mnazi mmoja (ninavyofahamu ingekuwa +255 22 218.... Location ya fax sio mnazi mmoja wala posta!
-Makosa ni mengi sana katika maelekezo yao n.k, lakini katika hali ya kawaida nani atakupa hela yake bila kukupima uwzo wako wa kulipa!

Hawa ni matapeli wakubwa sana!

na hata adress yao ya mtandaoni ina utata
 
nimesikia ali kiba alichukua mkopo kwa hawa jamaa kwa ajili ya kumalizia nyumba yake. Au naye ni mdau anafanya promo!

hivi mkopo wa nyumba unatolea dakika 45 au siku mbli?labda hazungumzii hwa jamaa
 
NIMEONA ninawajibika kuwataarifu kuhusu kuwepo kwa vijana wa Kitanzania ambao wamejiingiza katika mtandao wa kitapeli ambapo wamekuwa wanatangaza kuwa wanatoa mikopo kupitia Kampuni wanayoiita SOCIAL CREDIT COMPANY. Ili kufanikisha mipango yao wana-hack kurasa za facebook za watu mbalimbali ambao ni maarufu na zile zenye traffic kubwa. Wakifanikiwa wanamwondoa mwenye akaunti kwa kufuta USER NAME na PASSWORD yake na kuimiliki hiyo page. Kinachofuatia hapo ni kuanza kuposti taarifa za ushawishi kwa kutumia jina lako kuwa wewe mwenye akaunti unaijua hiyo kampuni hivyo unawatoa hofu jamaa zako.Kuna jamaa zangu ambao facebook page yao ilikuwa hacked na kwa sababu kidogo niko kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano nikaanza kuwafuatilia hawa jamaa na kuwataka wenye page watumie neutralizing strategy kwa kuwatumia watu waliokuwa wanaingia mara kwa mara kwenye hiyo page kutuma taarifa za kuitahadharisha jamii juu ya utapeli huu. Ingawa bado wanaishiilia hiyo page lakini zile posti waliziondoa. Tatizo hili pia liliwapata Airtel kama wiki moja iliyopita, hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa kupitia kiupindi chao cha Power Breafast.
HATUA ZAIDI TULIZOCHUKUA:
Ukisoma kiambatanishi, matapeli hawa wanadai kuwa wana ofisi Mnazi Mmoja na wametoa namba zao za simu na email address. Hivyo vyote ni vya uongo. Aidha, cha kushangaza wamefanikiwa kuandikisha namba za simu za mikononi za mtu wanayemwita Mhasibu wao anajulikana kama MR. ANTHONY SHILLIYE LUCAS. Huyu ameandikisha namba ya MPESA 0756 310 988 kwa jina la ANTHONY SHILLIYE na TIGOPESA 0714 254 735 kwa jina la ANTHONY LUCAS.
Tumetoa taarifa TIGO na VODACOM huku tukiamini kabisa kuwa tutapata ushirikiano wa kumjua mtu anayetumiwa fedha lakini ushirikiano umekuwa mdogo. Pia tumewataarifu TCRA ambao wameahidi kufuatilia kwa sababu huu ni WIZI wa MTANDAO. Hata hivyo mahali pa kuanzia ilikuwa ni kwenye hizi namba za simu kwavile tunaamini usajili wa hizo namba una viambatanisho. Pia kupata taaarifa za wale wote ambao wamekuwa wanawasiliana na hizi namba.
Website yao (SOCIAL CREDIT COMPANY) haina kitu zaidi ya hilo tangazo lililoko kwenye attachment ya email hii.
Watanzania wengi waliokumbana na tangazo hilo wamekuwa wanahangaika kutaka kujua ukweli wa Kampuni hii ambayo inadai kufahamika na taasisi nyingi muhimu nchini lakini hakuna. Bado watu wanaibiwa na hili linathibitishwa na post zilizo kwenye hii page ambayo wameifungua wakijifanya ni Wema Sepetu : https://www.facebook.com/wema.sepetu.946?fref=ts.
Kama haitoshi pia wamefungua akaunti ya AirTel Tanzania (https://www.facebook.com/pages/Airtel-Tanzania/438820529559726) ambayo sio akaunti sahihi ya Kampuni ya Simu. Hapo tumekuta post ambayo ipo katika Kiambatanisho kwenye email hii. Utaona Post ati kutoka AirTel wakimtaka Mteja ajaze Fomu.
Tukizingatia umuhimu wa vyombo vya habari katika mustakabhali wa nchi, ninaamini hii habari mnaweza kuitumia kutafuta ukweli wa nini hizi Kampuni za Simu zinajua kuhusu hili? Kwanini hazijoitokezi hadharani kueleza wanachokijua baada ya kupata malalamiko mengi?
Aidha, kwavile huyu mtu anachukua fedha kwa maajenti wa MPESA, TIGOPESA na AirTel Money ina maana hawawezi kusaidia kujua sehemu anayochukulia fedha? Je, kwa kutumia GPS hawawezi kujua huyu jamaa simu zake zinapatikana maeneo gani? Anawasiliana na watu gani? Pia ni IP Address gani anayoitumia kutuma hizo message zake? TCRA ni lazima walijue hili kwani liko katika eneo lao. Asanteni na samahani kwa kuwachukulia muda wenu mrefu. Ninatumaini mtalipa uzito hili suala ili wananchi wasiendelee kuibiwa na wajanja wachache.
Zaidi soma taarifa za utapeli wao hapo chini:-
www.socialcompany.wapka.mobi
FINANCIAL SERVICES
Secure Online Application
WALIO MTANDAONI (13)
________________________________________
JAZA FOMU
________________________________________
SOCIAL CREDIT COMPANY ni Taasisi ya kifedha inayohusika na utoaji mikopo nafuu na isiyokua na riba kupitia mfuko maalum uitwao Social Credit & Loans kwa dhumuni la kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa nchini Tanzania kwa kuwapatia mikopo ya pesa kwa lengo la kumuinua kiuchumi mtanzania na kumletea maendeleo ili aweze kujikimu kimaisha kwa dhana yakinifu kutaka kutokomeza umasikini.
Taasisi ya Social Credit Company imeanzishwa mwaka 2003 ikiwa kama tawi zawa lisilojitegemea nakua kampuni binafsi iliyoingia ubia na Bank ya NBC (National Bank of Commerce) kwa makubaliano ya mikataba ya muda. Social Credit Company imemaliza mikataba rasmi na Bank ya NBC hivyo imeanza rasmi kujitegemea na kuunda mfuko huu wa Social Credit & Loans.
Social Credit Company imeanza hatua za kutaka kusambaza matawi yake mikoa yote nchini Tanzania ili kila mtanzania aweze kupata huduma za mikopo kwa ukaribu, kwasasa Social Credit Company ina matawi matatu makuu katika mikoa mitatu (3) Dar es salaam, Kigoma na Dodoma ina jumla ya wafanyakazi 45 katika matawi tajwa kila mkoa.
MTANZANIA ATAWEZAJE KUPATA MKOPO?
Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania bila ya kuwepo na ubaguzi wa aina yoyote huduma zetu ni stahiki kwa kila mtanzania ambae ni mjasiriamali,mtumishi wa serekalini au mfanyakazi wa kampuni binafsi wote wanastahili kujiunga na kuwa washirika wetu na tutawapatia mikopo.
Wakati tukiwa katika maandalizi ya kusambaza matawi yetu katika kipindi hiki inamlazimu mteja wetu ambae anahitaji mkopo kuweza kujiunga kwa kujaza fomu ya maombi ya mkopo na kujiunga kupitia Online katika tovuti hii kwa kujaza fomu yetu na kulipia ada ya ushirika kiasi cha Tshs. 45,000 (elfu arobaini na tano) kupitia Mobile Banking M-PESA na TIGOPESA Baada ya mteja kujaza fomu yetu na kulipia ada Tshs. 45,000 fomu yake itapokelewa na bodi kuu ya utoaji mikopo pia malipo yake yatapokelewa na Muhasibu MR. ANTHONY SHILLIYE LUCAS baada ya hapo maombi yake ya mkopo yataidhinishwa na atapatiwa mkopo wake wa pesa ndani ya dakika 45.
SIFA ZA KUJIUNGA UWE MSHIRIKA UPATE MKOPO
Sifa kuu za mwanachama anaetakiwa kujiunga aweze kupata mkopo nikama zifuatazo:-
(i) UWE MUAMINIFU
(ii) UWE NA AKILI TIMAMU
(iii) UWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 AU ZAIDI
(iv) UWE MTANZANIA
(v) UWE NA KITAMBULISHO KIMOJA WAPO KATI YA HIVI MPIGA KURA, BANK, CHUO, LESENI YA BIASHARA, LESENI YA GARI au KITAMBULISHO CHA KAZI
KWANINI TUNATOA MIKOPO NAFUU YENYE MASHARTI RAHISI?
Watanzania wengi wanaweza kujiuliza kwanini Social Credit Company inatoa mikopo kwa watanzania yenye masharti rahisi sana tofauti na asasi zingine walizozizoea kama bank na nyinginezo!? Sababu kuu ya kuweka masharti rahisi ni kutaka kumsaidia kila mtanzania kuweza kupata mikopo bila kumuwekea vikwazo vigumu ambavyo vitakatisha ndoto zake na kumfanya awe dhaifu katika maendeleo yake kwa kukosa mkopo kutokana na vigezo vyetu kua vigumu ikiwa dhamira yetu kuu ni kutaka kumsaidia kila mtanzania hivyo hakuna sababu yakuweka ugumu wa upatikanaji wa mikopo.
KWANINI TUNATOA MIKOPO ISIYOKU NA RIBA?
Mikopo hii haina riba kutokana na faida kuu mbili tuzipatazo kutoka katika kampuni za simu pindi mteja anapojaza fomu na kulipia ada kwa tigopesa au mpesa kuna asilimia fulani zinaingia katika kampuni yetu kupitia mitandao ya simu VODACOM na TIGO pindi mteja anapotuma pesa. pia ada zinazolipiwa na wateja wetu baada ya kujaza fomu Tshs.45,000 inaingia katika mfuko wa Social Credit Company hivyo tunafaidika kwa asilimia kubwa kipato kinajitosheleza bila kuchukua riba
MTEJA ATAUPOKEA MKOPO WAKE MUDA GANI? BAADA YA KUJAZA FOMU NA KULIPIA ADA
Mikopo yetu haicheleweshwi kwa mteja wetu atakae jiunga kwa kujaza fomu na kulipia ada kiasi cha Tshs.45,000 atapatiwa mkopo wake wa pesa ndani ya muda muafaka
Social Company imeondoa urasimu ili kumuwezesha mteja wetu kupata mkopo wake ndani ya dakika 45 baada ya maombi yake ya mkopo kuidhinishwa.
MTEJA ANARUHUSIWA KUKOPA KUANZIA SHILINGI NGAPI?
Mteja anaruhusiwa kuomba mkopo kuanzia Tshs. 200,000 (LAKI MBILI) Mwisho wa kukopa ni Tshs. 10,000,000 (MILLION KUMI)
MTEJA ATAPOKEA VIPI MKOPO WAKE BAADA YA KUJAZA FOMU NA KULIPIA ADA?
Katika fomu ya kujiunga kuna kipengele kinamtaka mteja ajaze njia itakayokua rahisi kwake kupokea mkopo wake kuna M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY au Bank inategemea na kiasi cha mkopo mteja atakacho omba. Mkopo kuanzia Laki Mbili mpaka Million Tatu mkopo wake utatumwa kupitia M-Pesa, Tigopesa au Airtel Money. Kuanzia shilingi Million Nne mpaka Million Kumi mteja atatumiwa mkopo wake kwa njia ya Bank katika akaunti yake. Hivyo mteja atatakiwa kujaza namba ya M-Pesa, Tigopesa au Airtel Money katika fomu ili mkopo wake utumwe kwa njia ya Mobile Banking pia mteja anaweza kuandika akaunti namba zake za Bank ili apokee pesa zake kupitia Bank. Mara baada ya mteja kujaza fomu na kulipia ada elfu45 atapewa taarifa pindi tukishamtumia pesa zake.
KWANINI MTEJA ANAJIUNGA ONLINE KATIKA MTANDAO?
Tumeanzisha utaratibu huu wa kujiunga online kupitia katika mtandao kulingana na sababu kubwa ya upungufu au ukosefu wa matawi yetu kuto-enea katika mikoa yote Tanzania hivyo tumemrahisishia kila mtanzania ambae yupo mkoani na hakuna tawi letu na anahitaji kujiunga ili awe mshirika aweze kupata mkopo iwe njia rahisi kujiunga Online kupitia katika mtandao huu kwa kujaza fomu yetu na kulipia ada Tshs.45,000 kupitia M-PESA au TIGOPESA na tutaipokea fomu yake na tutampatia mkopo bila tatizo.
MTEJA ANAE HITAJI KUFIKA KATIKA OFISI ZETU ATATUPATAJE? (Mawasiliano)
Contacts Details
UHURU STREET
SCC MNAZI MMOJA BRANCH
1st FLOOR
P.O.BOX 9282
MENEJA: +255 22 2135823
FAX: +255 22 2163448
Email: info@socialcompany.co.tz
AINA ZA MIKOPO TUNAYOITOA KWA WATEJA
1. BIASHARA
Mikopo ya biashara tunaitoa kwa wajasiriamali / wafanya biashara
2. MAENDELEO
Mkopo wa maendeleo unatolewa kwa wateja wote ambao wanahitaji kufanya maendeleo binafsi kama kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja au vitu vya samani aidha ukarabati wa nyumba
3. ELIMU
Mkopo wa elimu unatolewa kwa wanafunzi walio vyuoni kwa dhumuni la kuwasaidia kulipia karo mashuleni au kwa mahitaji binafsi ya elimu
JINSI YA KUREJESHA MKOPO
Mteja mara baada ya kujiunga kwa kujaza fomu na kulipia ada tukampatia mkopo atatakiwa kukaa miezi miwili bila kufanya marejesho na baada ya hapo ndio atatakiwa kuanza kufanya malipo ya mkopo wake KWA MFANO: Mteja kajaza fomu leo Tarehe 3 mwezi wa 5 na akalipia ada tukamtumia mkopo wake basi atatakiwa kuanza kurejesha mkopo kuanzia Tarehe 3 mwezi wa 7. Miezi miwili atakaa bila kulipia na baada ya hapo mteja ataanza kua anarejesha malipo ya mkopo wake kupitia namba yetu ya Vodacom kupitia M-PESA
NAMBA ZA KULIPIA ADA YA KUJIUNGA NA MAREJESHO YA MKOPO
Mteja akishajaza fomu atatakiwa kulipia Tshs. 45,000 Elfu arobaini na tano kupitia M-Pesa katika namba: 0756 310 988 au TIGOPESA katika namba 0714 254 735 ni muhimu kulipia na pia kwa wateja wa AIRTEL MONEY mnaweza kulipia toka katika akaunti za Airtel Money kuja Tigopesa au M-Pesa katika hizo namba zetu za Muhasibu wa kampuni ya Social Credit Company na pesa itatufikia. Hakikisha unapotuma pesa katika namba ya M-PESA jina litatokea ANTHONY SHILIYE pia kwa TIGOPESA hakikisha jina linatokea ANTHONY LUCAS ni majina ya muhasibu ambae ndie anaepokea malipo ya ada na marejesho pia kwa marejesho ya mkopo zinatumika namba hizo hizo
MAREJESHO YA MKOPO
Mteja atatakiwa kurejesha kiasi chochote kile cha pesa kuanzia Tshs. 100,000 Laki moja kila mwezi mpaka deni lake litakapo kwisha haijalishi mteja atakua analipia shilingi ngapi ila kima cha chini kianzie Tshs. 100,000 mteja anaruhusiwa kuwa analipia laki moja au zaidi ya laki moja kulingana na uwezo wake kinachotakiwa aweze kukamilisha malipo ya mkopo wake na marejesho yote yasivuke miezi 160.
JIUNGE SASA UPATE MKOPO WA HARAKA NA NAFUU
Kujiunga ni rahisi mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na atapatiwa mkopo. Unachotakiwa kufanya bofya katika Link / Kimvuli hapa chini kilichoandikwa JAZA FOMU HAPA utaiona fomu ya kujiunga ijaze fomu yote kisha itume kwetu baada ya hapo unatakiwa kulipia ada Tshs. 45,000 kupitia M-PESA katika namba 0756 310 988 au TIGOPESA katika namba 0714 254 735 pia kwa wateja wa Airtel mnaweza kulipia toka katika akaunti zenu kuja katika namba zetu hizo na tutapokea malipo yenu.
ANGALIZO: Ni muhimu kulipia Tshs.45,000 ili kuchangia mfuko wa Social Company na mikopo itatolewa kwa wale ambao watajaza fomu na kulipia ada pekee
Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania, wajasiriamali na wasiokua wajasiriamali pia wafanyakazi wa makampuni binafsi na watumishi serekalini wanaruhusiwa kujiunga na watapatiwa mikopo.
Bofya katika hii Link ifuatayo iliyoandikwa JAZA FOMU HAPA uweze kujiunga kwa kuijaza fomu na ulipie ada Tshs.45,000 tukupatie mkopo. Baada ya kujaza fomu na kulipia ada utapokea mkopo wako ndani ya dakika 45.
 
Mbona wanakusanya hiyo ya kiingilio"?
Au BOT, M PESA NA TIGOPESA wanapata chao kuwadhulumu masikini was Tz?

Hayo ya kiingilio watajuana wenyewe. Hata ukienda Bar kuangalia mpira unalipa kiingilio.

BOT wao wanahusika tu iwapo taasisi inafungua milango inajidai kuweka pesa za wananchi.

Ukiandika bango unaweka pesa za wananchi kama walivyofanya Desi, unapokea deposits hapo ndio utajua BOT ni nani.
 
Ina maana kama ni matapeli Police hawajaliona hili?, au ndo Tz shamba la bibi kama kawaida.
 
Hawa ni matapeli.nA mwanachofanya wanahack account za hawa wasanii then wanapost wnavyotaka wao
 
Aasante sana kaka kkwa kutujuuza sasa ambao walishaliwa wanafanyaje tunawasaidiaje hawa
 
Ridhiwani Kikwete
MATATIZO MAKUBWA
YAMKUMBA MSANII DIAMOND
PLATNUM BAADA YA KUTOA
KASHFA KWA MSANII ALIKIBA.
Baada ya msanii Diamond kumtolea
kashfa msanii alikiba alivyo jiunga
na Taasisi inayotoa mikopo SOCIAL
CREDIT COMPANY. Kampuni ya
SOCIAL CREDIT COMPANY
imeamua kumfungulia mashtaka
msanii DIAMOND kwa kashfa hizo
kupitia taasisi hii. Siri iliyokuwepo
nikwamba baada ya msanii Diamond
kupost zile kashfa na ishu kua kubwa
aliwahi kuifuta post yake katika
ukurasa wa Tweetter ili kupoteza
u ya
SOCIAL CREDIT COMPANY
ilikua imepata ushahidi na kuhifadhi
hiyo post kama picha.
shahidi bila kujua kama taasisi
MENEJA WA SOCIAL CREDIT
COMPANY AMEZUNGUMZA NA
VYOMBO VYA HABARI NA
KUSEMA HAYA YAFUATAYO:
: “Kitendo alichokifanya
msanii Diamond kumkashifu msanii
mwenzake Alikiba sio kitu kizuri na
uongozi wa Social Credit Company
hatujapendezwa kabisa na tukio hilo,
tumeamua kulichukulia
ni
msanii au sio msanii sasa kwanini
Diamond atoe kashfa kwa
mwenzake? Sisi hatubagui mtu,
kwetu wote nisawa mtu yoyote
anaetaka mkopo anaweza kutembelea
ofisi zetu akajiunga akapewa mkopo
au akajiunga online kupitia tovuti
yetu hii hapa
#MENEJA
umakini
suala hili la msanii Diamond kwa
kumfungulia mashtaka ili iwe
fundisho kwake na kwa wengine ili
kukomesha hizi tabia za kuwakashifu
wenzao na sababu kuu ya sisi
kumshitaki ni baada ya yeye kuamua
kuingiza jina la kampuni yetu katika
post yake na akawahi kuifuta
akidhani hatujaipata. Kiukweli
SOCIAL CREDIT COMPANY
hatuna ubaguzi mtanzania yoyote
anaruhusiwa kujiunga na taasisi yetu
na akapatiwa mkopo haijalishi
http://socialcredit-
company.wapka.mobi akajiunga na
akapewa mkopo.
CHANZO CHA
HABARI #MILLARD_AYO
 
Ridhiwani Kikwete
MATATIZO MAKUBWA
YAMKUMBA MSANII DIAMOND
PLATNUM BAADA YA KUTOA
KASHFA KWA MSANII ALIKIBA.
Baada ya msanii Diamond kumtolea
kashfa msanii alikiba alivyo jiunga
na Taasisi inayotoa mikopo SOCIAL
CREDIT COMPANY. Kampuni ya
SOCIAL CREDIT COMPANY
imeamua kumfungulia mashtaka
msanii DIAMOND kwa kashfa hizo
kupitia taasisi hii. Siri iliyokuwepo
nikwamba baada ya msanii Diamond
kupost zile kashfa na ishu kua kubwa
aliwahi kuifuta post yake katika
ukurasa wa Tweetter ili kupoteza
u ya
SOCIAL CREDIT COMPANY
ilikua imepata ushahidi na kuhifadhi
hiyo post kama picha.
shahidi bila kujua kama taasisi
MENEJA WA SOCIAL CREDIT
COMPANY AMEZUNGUMZA NA
VYOMBO VYA HABARI NA
KUSEMA HAYA YAFUATAYO:
: “Kitendo alichokifanya
msanii Diamond kumkashifu msanii
mwenzake Alikiba sio kitu kizuri na
uongozi wa Social Credit Company
hatujapendezwa kabisa na tukio hilo,
tumeamua kulichukulia
ni
msanii au sio msanii sasa kwanini
Diamond atoe kashfa kwa
mwenzake? Sisi hatubagui mtu,
kwetu wote nisawa mtu yoyote
anaetaka mkopo anaweza kutembelea
ofisi zetu akajiunga akapewa mkopo
au akajiunga online kupitia tovuti
yetu hii hapa
#MENEJA
umakini
suala hili la msanii Diamond kwa
kumfungulia mashtaka ili iwe
fundisho kwake na kwa wengine ili
kukomesha hizi tabia za kuwakashifu
wenzao na sababu kuu ya sisi
kumshitaki ni baada ya yeye kuamua
kuingiza jina la kampuni yetu katika
post yake na akawahi kuifuta
akidhani hatujaipata. Kiukweli
SOCIAL CREDIT COMPANY
hatuna ubaguzi mtanzania yoyote
anaruhusiwa kujiunga na taasisi yetu
na akapatiwa mkopo haijalishi
http://socialcredit-
company.wapka.mobi akajiunga na
akapewa mkopo.
CHANZO CHA
HABARI #MILLARD_AYO
 
Hiyo Company magumashi nilijazaga fomu yao kwa maelezo ambayo kias cha mkopo nilicho omba isingekuwa rahisi kukubaliwa lkn nika ambiwa mkopo wang umepitishwa kinachotakiwa ni2me ada 125000/=. Nikash2kia dili ila haikunipashida kwakua ktk maelezo yao walidai wanatawi DAR, DOM na KGM nikaona sio kes nikawaandikia text wanipe maelekezo tawi lao lilipo KGM ili niwatembelee, wakanipigia cm et wenyewe wapo Kigamboni dah! Yaani wakawa wanapingana na maelezo yao nikash2ka nikala pin. Hivyo hawana uthibitisho wa uhakika km ifuatavyo:
-Ada yao inabadilika badilika
-Kunawa2 wana wa2mia FB kujifanya wameshapokea mkopo
-Nilionge na VodaCom juu ya uthibitisho wao kuhusiana na upitishaji wa hela kwao sikupata uthibitisho.
 
Back
Top Bottom