Social credit company ni kampuni ya ukweli au magumashi?

Social credit company ni kampuni ya ukweli au magumashi?

MAMBO 7 MUHIMU ILI MWAKA 2015 UWE WA MAFANIKIO KWAKO
Ikiwa leo ni siku ya 8 tangu mwaka 2015 uanze.inawezekana bado uko na malengo ya mwaka jana na hukufanikiwa kuyafikia,au bado hujapanga malengo yako ya mwaka 2015.inawezekana bado hujatambua kama siku 8 tayari zimeshapita na hazitajirudia maishani mwako.tunaishi mara moja na wakati uliopo ndio unacheza movie ya maisha yako,hakuna muda mwingine tena..
Haitakuwa na maana kwako kusherekea mwaka mpya na ukaingia kwa furaha halafu ukaendelea kubaki yuleyule, haiwezekani. Umefika ni wakati wa kubadili akili yako na kuwa na mitizamo mipya, inayoona fursa mpya na itakayokuongoza pia katika ushindi wa mafanikio unayoyataka. Je, unataka mwaka 2015 uwe wa historia na mafanikio makubwa kwako? Kama nia hiyo unayo na una uchungu wa mafanikio, hakikisha unafanya mambo haya:

1. ANZA KUBADILI MTAZAMO WAKO KUHUSU MAISHA HARAKA SANA
Kitu kipya kwako unachotakiwa kuhakikisha kukifanya ni kubadili mtazamo huo ulio nao kuhusu maisha. Anza kufikiri tofauti na ulivyokuwa ukifikiri mwaka jana, acha kuogopa vitu ambavyo kwako huwezi kuvitawala, acha kuwaza hasi sana badala yake anza kufikiri chanya katika kila Nyanja ya maisha yako. Kama utaendelea kuwa Yule Yule wa siku zote mabadiliko ya mwaka hayawezi kukusaidia kitu, utakuwa tu kama ni utoto kufurahia mabadiliko ya namba bila ya wewe kubadilika.

2. ANZA KUISHI KWA MALENGO MAKUBWA

Kama wewe ulikuwa ni mtu wa kujiwekea malengo kidogo katika maisha yako, anza sasa kujiwekea malengo makubwa. Wewe si mtu wa kawaida tambua vipaji vyako ya kuwa wewe ni nani? Kisha anza kuvitumia ili kufanikisha malengo makubwa uliyonayo katika maisha yako. Hauna haja tena ya kulaumu wala kulalamika kama ambavyo umekuwa ukifanya mara kwa mara, ni wakati wako sasa wa kuishi kwa malengo uliyojiwekea na kuyafuata.

3. ANZA KUJIFUNZA KILA SIKU
Hili ni jukumu ambalo unatakiwa kuwa nalo kila siku bila kuliacha. Ukiwa ni mtu wa kujifunza kila siku vitu vipya hasa kupitia vitabu, utakuwa unakua kila siku kiakili na baada ya muda utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na changamoto kuliko unavyofikiri. Hautakuwa na mafanikio makubwa sana kama wewe hautaanza jukumu hili la kujifunza kikamilifu kila siku mwaka huu. Tenga muda maalumu wa kujisomea kila siku utaona matokeo yake.

4. ANZA KUTUMIA UWEZO MKUBWA ULIONAO
Hata kama kuna wakati unapitia kwenye majaribu na pengine unashindwa kuona matumaini yaliyo mbele yako lakini, tambua kitu hiki muhimu kwako kuwa una uwezo mkubwa wa kukufanya kuwa tajiri ambao huutumia. Kwa kulijua hilo anza kufikiri kama mtu aliyefanikiwa hata kama mfukoni hauna kitu na acha kujiona hufai kama ambavyo umekuwa ukijiona kwa muda mrefu sasa, huu sasa ni mwaka wa mafanikio kwako, tumia uwezo mkubwa ulionao kufikia mafanikio makubwa unayotaka.

5. ANZA KUWA WEWE KAMA WEWE
Kujaribu kuwa kama mtu mwingine katika maisha yako ni unapoteza muda wako bure. Jifunze kuwa wewe kama wewe, acha biashara ya kukurupuka na kuiga malengo ya watu wengine. Hiyo itakurudisha nyuma sana kimbia mbio zako wewe mwenyewe na ipo siku utakuwa mshindi. Kama kwa miaka yote umekuwa ukiishi kwa kuiga maisha ya watu wengine, kwa mwaka 2015 achana na hayo mazoea. Ni muda wa kuishi maisha mapya na kutegemea kuona mabadiliko makubwa, kikubwa chukua hatua.

6. ANZA KUISHI MAISHA KWAKUWA NA WATU SAHIHI.
Wakati wa kuishi maisha na watu ambao wanakukatisha tamaa, wanakurudisha nyuma umeshapita. Jipange sasa kwa mwaka huu unaoanza kuwa na watu sahihi watakaoweza kukusaidia kutimiza malengo yako kwa urahisi. Jifunze kwao kisha na wewe uchukue hatua ya kubadilisha maisha yako. Unapokuwa na watu sahihi inakusaidia kujifunza vitu vingi vinavyobadili maisha yako na utaona malengo yako yakitumia kuliko ambavyo ungekuwa na watu ambao sio msaada kwako.

7. ANZA KUFURAHIA MAISHA YAKO.
Kwa vyovyote vile unavyoishi, jifunze kuyafurahia maisha yako. Hata kama upo kwenye shida nyingi namna gani yafurahie tu maisha yako. Hakuna muda au wakati utakaokuja useme sasa huu ni wakati wa kuyafurahia maisha hakuna. Kwa mwaka 2015 jifunze kuyafurahia maisha yako kwa kuishi leo kama leo na kuachana na hofu zinazokunyima furaha. Ukiweza hili utamudu kuwa na amani na furaha na hiyo itakusaidia kujenga mafanikio makubwa yaliyo mbele yako.

MPENDWA ACHA KUISHI MAISHA YALE YALE ULIYOKUWA UKIISHI MIAKA YOTE, Hayatakufikisha popote zaidi ya kukurudisha nyuma. Jitafakari mwenyewe mienendo yako uliyonayo na kisha jiulize je, inakufikisha kwenye mafanikio unayotaka? Au kuna mahali utaishia kukwama. Ukishapata jibu, chukua hatua za kufanya kile kitachokusaidia kukufanikisha, ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi mambo haya muhimu uliyojifunza sasa.
UKIPENDA KUJIFUNZA ZAIDI KUPITIA NA UNA MALENGO MAKUBWA USISITE INBOX OR WHATSAPP 0752997088
 
Back
Top Bottom