Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Lengo la mjadala huu ni kupanua uelewa juu ya nafasi ya mitandao ya kijamii kwenye siasa za Tanzania na duniani kwa ujumla kwenye zama hizi katika kujenga au kubomoa.
Aidha, mijadala unalenga kuchambua ni kundi gani linafanya nini huku mitandaoni, kwa nini linafanya linavyofanya, nini kinachotegemewa kutokea katika mazingira fulani fulani na nani anapaswa kufanya au kutofanya nini kwenye mazingira yetu ya Tanzania na ili iwe nini.
Katika mada hii, tutajadili kwa kina maeneo yafuatayo
1. Wanaofanya siasa mtandaoni ni kina nani hasa?
2. Malengo ya wanaofanya siasa za mitandaoni ni yapi?
3. Tafiti zinasemaje kuhusu siasa za mitandaoni na muelekeo wa siasa za dunia (Social media politics Vs actual field politics)
4. Nguvu ya mitandao ya kijamii kwenye siasa ni kubwa kwa kiasi gani? na hiyo maana yake ni nini?
5. Huko duniani wanafanya nini na ili iwe nini?
6. Hapa kwetu tanafanya nini na kwa nini na hatma yake ni nini?
7. Uzandiki mitandaoni na kwa nini?
8. Nani anapaswa kufanya nini na ili iwe nini?
9. Vikwazo ni nini kwenye kuchukuwa hatua sahihi na ni vipi tunaweza kuvivuka.
10. Ni nini kitatokea kama ikiachwa ‘nature’ iamue.