social networking...

social networking...

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
...mnh, Mwenzenu 'mshamba!'

Hizi social networking mbona ni kasheshe wajameni!...Facebook, Hi5, Twitter sijui Bebo nk...

Utakuta wanoalalama kwanini 'rafiki' anataka kum- add tena baada ya kum- delete!

Wengine unakuta status zao 'married', ...within days anabadilisha unakuta 'separated'...mara -'complicated relationship'...

Ni kweli tumefikia kuweka maisha yetu hadharani kiasi hiki, au ndio speed za maisha zinapitiliza IQ zetu?

Heri yetu wa miaka ya 47 na zile autograph... Ukishapewa u saini, unabandika kapicha ka Bruce lee, James Bond au Jackson 5,...unaandika uyapendayo kisha unamrudishia mwenye buku, ...akiliacha liingie vumbi au liliwe na panya shauri yake... sio miaka hii mambo yanasomwa hadharani kuanzia Tokyo mpaka Miami!

au ndio maendeleo yenyewe haya?

Mtu akiku delete hadharani, au 'mchuchu wako' akikupiga kibuti hadharani namna hii utamuelewaje?
 
Mbu kusema kweli maisha yetu siku hizi yamekuwa maisha ya dunia meaning its not a private life anymore but global life- na ndio maana tunasikia habari nyingi za ndoa za watu n.k. kwa sababu yale maadili yetu ya kutunza siri hayapo tena!
 
mbu ......dunia ya sasa hakuna kitu SIRI! vyote vinamwagwa hadharani tu...kuanzia najisikia lonely, nimepata mpenzi mpaka jana nili enjoy vya kutosha na mume wa mtu!
 
Mbu, hakuna watu wanaojali utamaduni wao kama Wachina na Wajapan. Tena wameu-maintain na kuutunza kuliko hata sisi Waafrika. Lakini cha ajabu - wamekuwa mstari wa mbele kuendeleza teknolojia na kuiendeleza. We now live in global village, tutake tusitake maisha yetu taratibu yataanza kujulikana kwa wengi kuliko ilivyokuwa zamani. Kamwe hatutashindana na wimbi hili la mabadiliko na kusema kuwa tumelishinda.

Kwa upande mwingine, huu uwazi na utandawazi pamoja na mabaya yake au mazuri yake yote tunayoyasikia unashabihiana vipi na matamaio yetu kimaisha? Je, tumekaa na kujiuliza uzuri na ubaya wa maisha yetu ya kisiri siri na kulinganisha tofauti kifaida inayoweza kuwepo au kuletwa tukiwa wawazi zaidi katika maisha yetu? Je, tunapoamua kuficha ficha mambo yanayotukabiri na yanayohusisha wenzetu kimaisha na mahusiano tunamficha nani, nafsi zetu au za wengine? Je, huu ni utamaduni wetu wa asili au ni hali iliyojijenga na kuendelezwa tu hivyo kuonekana ni utamaduni? Utamaduni unajengwa vipi, na upi uliobora kwa maendeleo yetu katika mambo ya mahusiano?!
 
Mbu kusema kweli maisha yetu siku hizi yamekuwa maisha ya dunia meaning its not a private life anymore but global life- na ndio maana tunasikia habari nyingi za ndoa za watu n.k. kwa sababu yale maadili yetu ya kutunza siri hayapo tena!

Kutunza siri na kuficha ficha mambo, haswa maovu, kwa kiwango kikubwa mimi naamini ndiko huku kumeendeleza na kueneza maambukizi ya ukimwi kwa waafrika kuliko kwingineko.
 
Jamani inafika mahali zinaboa sana.Kuna wakati nilijiunga na forum fulani ili inisaidie ku-imporve English skills hasa speaking kwa nia ya kuchati na skype,lakini niliboreka kwa siku moja.kila ukiingia kila mmoja anauliza marital status,na kutafuta mahusiano ya mapenzi badala ya lengo muhimu la kujifunza.
 
Napenda UWAZI na ukweli to me no P.
 
migogoro tupu hii nayo inachangia sana kuharibu mahusiano ya watu
 
mbu ......dunia ya sasa hakuna kitu SIRI! vyote vinamwagwa hadharani tu...kuanzia najisikia lonely, nimepata mpenzi mpaka jana nili enjoy vya kutosha na mume wa mtu!

mie hapa hata sisemi kabisa
 
Jamani inafika mahali zinaboa sana.Kuna wakati nilijiunga na forum fulani ili inisaidie ku-imporve English skills hasa speaking kwa nia ya kuchati na skype,lakini niliboreka kwa siku moja.kila ukiingia kila mmoja anauliza marital status,na kutafuta mahusiano ya mapenzi badala ya lengo muhimu la kujifunza.
ZD, kwa kweli inategemea na kile unachoamua kuandika na jinsi unavyoamua watu wakuchukulie kimaandishi. Kwamfano, hapa hapa JF, kuna akina dada na akina mama ambao sijaona wakiletewa kebehi na tahfurani za kimapenzi kutoka kwa wakorofi wa JF licha ya kujulikana kimajina au kimaandishi kuwa ni wanawake.

Hata hivyo Mbu anaongelea zaidi social networking sites au standalone applications. Hizi ziko geared kwenye kujua status ya mtu na kile akifanyacho kwa wakati huo au yale yamzingirayo yeye kama yeye, kimaihusiano, kikazi, n.k.
 
well said steve
 
mbu ......dunia ya sasa hakuna kitu SIRI! vyote vinamwagwa hadharani tu...kuanzia najisikia lonely, nimepata mpenzi mpaka jana nili enjoy vya kutosha na mume wa mtu![/QUOTE]

cjui kama nimekuelewa vizuri mrembo wangu......
 
hivi COMPLICATED maana yake nini??
 
hivi COMPLICATED maana yake nini??
hizi ni relation zilizoingiliwa!inapofika muda unatakiwa urudi nyumbani unatamani kufa!hiyo nyumba unaiona chungu.huyo mume/mke unamuona shetani
 
duh. si nchezo.
 
...bahati mbaya 'kizazi kipya' wanaona hayo ndio maisha. Yaani huna haja kujua mtu kaamkaje, kila siku ana post kila kilichopita, kilichopo, na kitachofuatia...

Yaani unakuta hasa (wanawake) wanajiweka soo vulnerable kwa predators wanaowinda 'mlo' kama huo. Cha ajabu kile 'wanachoshindwa' kukiongea nyumbani utakikuta baada ya masaa machache online (akiwa kazini)...

Mbaya zaidi, kuna wale wenye IQ ndogo ambao 'wakianza' ku cheat tu utaona mabadiliko kwenye status zao, na comments za ajabu ajabu zikifuatiwa kisha kufutwa baada ya siku chache, hawajui INBOX hawa?

...Almuradi kitimu timu mambo hadharani!
 
Ndio maana mimi sipo huko kwenye mafacebook yenu na matwitter yenu.
 
Back
Top Bottom