Maiti, Mkuu ninachokisema nakielewa vizuri sana.
Umri ambao wazazi wamekulea ni mchache sana ukilinganisha na umri ambao utakuja kuishi bila wazazi.
Hivyo wazazi umeishi nao kwa muda mchache tu. Muda mwingi utakuwa peke yako na utajilea mwenyewe.
"Njia bora ya kuondokana na uwoga ni kufanya kile unachokiogopa"
Usipeleke lawama kwa wazazi, utajikuta upo hapo hapo,azima ujue kwamba wazazi walikosea kukulea vile, na hapo sasa baada ya kusema walikosea sasa ujiulize je upo tayari kuishi kwa matokeo ya makosa yao? NO HAUPO TAYARI.
Sasa anza kuchukua hatua muda huu, huu ndio muda wako wa kuweka lawama pembeni na kuangalia namna gani utalitatua tatizo hilo pasi na kuwalaumu wazazi, kwani UKILAUMU SANA WENGINE INAKUFAYA UJIONE WEWE NI MSAFI SANA.
Njia ya kwanza ambayo itaweza kukutoa katika janga hili ni kwanzakuwapa wazazi UDHURU kwamba walikuwa na nia njema huenda walikosea katika matendo yao.sasa wahukumu kwa ile nia yao njema na sio yale matendo yao.
Kwani lau wangelikuwa hawana nia njema ingekuwa UMESHAKUFA ZAMANI WEWE.
Kwanini upo mpaka sasa hivi? Kwa sababu yao,hawakukutilia sumu wala kukupangia njama za kukuuwa bali walijitahidi kukufikisha hapo ulipo.
Tatizo ni wewe sio wazazi, wao wameshamaliza kazi yao na sasauko wewe ndo muamuzi nani uwe.
Unadhani ukiwa ndani ya shimo alafu ukawa unandelea kulichimba utafanikiwa? Hapana bai acha kuchima himo ukiwa shimoni.
Acha kuongeza lawama kwa wazazi wakati bado upo katika matatizo yako na unahitaji kuyatatua kwa namna yeyote ile.