afadhali hii ni kisoda....kuna mdau mwingine alishalalamika pia
yakwake ilikuwa sprite na ndani ina condom (salama) ukitafuta
post za nyuma utaipata
Hii ndio shida yetu Watanzania. Hivi inasaidia nini kwako binafsi na kwa sisi wenzio ukija hapa kunung'unika na kuishia hapa?
Hivi kweli kwa akili yako unaona mwenye kiwanda chake anaweza akawa amewaelekeza wafanyakazi wake waweke condom kwenye chupa ilhali anajua ya kuwa ubora ndio msingi wa biashara yake?
Kutopeleka ushahidi sehemu husika ni upumbavu usio na shaka. Wale waliopewa kazi pale kiwandani ni Watanzania wenzetu, ila kwa kutokuwa kwao makini wanaleta yote haya. Ikiwa leo mwekezaji ataamua kuleta hadi waosha chupa kutoka kwao South Africa nadhani wote tutapiga kelele na nafikiri sheria haimruhusu.
Tusiwe watu wa kunung'unika kama mapanya. Jambo limetokea do the needful. Kuja hapa kuletea gumzo ambalo kwa maoni yangu nafikiri ni sehemu ya udhaifu wa jamii yetu ni ujinga. Akitolewa muosha chupa pale akawekwa kuhindi tutanuna, lkn wakati huu ambapo tuna uwezo wa kumsaidia mwekezaji kuboresha tupo nyuma kazi umbea na majungu.
Juzi juzi hapa tulikuwa na malalamiko oooh tiGO imefanya hivi mara tiGo imezua hili. Kama sio ndugu zetu vilaza (Wanaojiita wataalam) wa IT ni nani wa kulaumiwa ikiwa server ipo down? Kama leo mwekezaji wa tiGO angeruhusiwa kuleta wazungu wenzake kusimamia system, unafikiri tuongea madudu ya kupiga simu halafu uje ujumbe kuwa huna salio la kutosha wakati una 1800?!
Mfano mwingine ni hapa hapa JF. Mara ngapi jitu linalalama tuuu kuwa limetukanwa wkt hapo pembeni kuna button ya Report Abuse, halibonyezi, liaona kulalamika ndio solution.
Haya mambo ya umbea mnayoyafanya hapa, hayaisaidii Tanzania kama Taifa. Coca Cola ikikosa soko kwa ujinga wamuosha chupa akisaidiwa na aliyeona kizibo na kuacha kutoa taarifa sehemu husika ili wanaofanya huu uzembe wachukuliwe hatua, kitakachotokea ni kwamba kampuni itashindwa kujiendesha na kiwanda kitafungwa. Kiwanda kikifungwa ndugu zetu wengi watakosa ajira, hata wale waliofanya kazi yao kwa uaminifu mkubwa. Sasa huu ni wakati wa nyie wenye ushahidi kuisaidia jamii yetu kuimarika kwa kurekebisha makosa.
Kukuta kizibo ndani ya chupa ya soda sio uvumbuzi wa mtu kujinadi as if ameunda mtambo. Jambo sahihi ni kuripoti ili mzembe aondolewe, na walio waaminifu wasipoteze ajira zao kwa kiwanda kufungwa.