Mkuu kwa style yako ambayo unashawishi watu kwa kuona uzembe mkubwa hivyo kukaa kimya na kukimbilia kiwandani kuripoti mie naona haitoshi,alivyofanya huyu kuitangaza na kuipiga picha ni sawa kabisa.
Nyie kila siku mnatangaza product zenu kwenye tv mabango etc kuwa zina ubora kumbe mnakuwa wazembe mnaachia kondom na matakataka mengine ndani halafu mnafunga watanzania midomo wasitangaze,hiyo ni sawasawa na mgomo pale muhimbili watu wanakufa ovyo halafu unafunga mdomo watu,wanaharakati na waandishi kupigia kelele,huo ni uzembe wa hali ya juu kama zingekua nchi za wenzetu ni issue kubwa sana hiyo sio nyepesinyepesi kama ulivyoichukulia.
Suala lingine ambaloo umeliongelea hapo mie kwangu naona ni la kipumbavu,uzembe wa management yenu ya kusimamia wafanyakazi kwa makini kwa kufuata procedure zilizopo ndio utufumbe mdomo eti ni kutetea ajira ya watz wenzetu kwa hiyo tuendelee kunywa uchafu?Naomba sana usichukulie umasikini wetu sisi watanzania kama mtaji wa kutulisha uchafu eti tuogope kufukuzwa kazi.
Kwanza wewe utakua sio mtanzania kama ni mtz basi utakua ni kibaraka wa hao makaburu manake unaonekana unawalamba miguu sana mara oo tigo mzungu kilichobaki kwako ni kuwaabudu.
Jamani watanzania wenzangu nasema tunaweza tusijizaraulishe wala tusikubali kuzarauliwa na vibaraka wa wazungu.
Mie ni mpenzi mkubwa sana wa soda ya cocacola,Napenda kuchukua nafasi hii kuiomba serikali kupitia mashirika yake ya viwango kufanya suprise visit katika kiwanda hicho cha soda angalao twice a monthy ili kuweza kuthibitisha ubora wa vinywaji wanavyotengeneza.
Sitakulaumu kwa kuwa am not responsible for your thinking capacity. Mimi si mmiliki wala si mfanyakazi wa Coca-Cola, naomba usome taratibu na uelewe nilichomaanisha kabla hujasapoti jambo la kijinga la huyu mtoa mada.
1. Nilisema kuwa, si nia ya mfanyabiashara kusambaza bidhaa chafu kwa kuwa anajua mustakabali wa mtaji wake upo ktk ubora wa bidhaa anazouza kwa hiyo ni dhahiri hata yeye angefurahi kuona tatizo hilo linapata ufumbuzi. Je, kwa kusema hapa JF unasaidia nini ktk juhudi za kumbaini aliyesababisha uchafu kubaki ktk chupa?
2. Niliposema ajira, nilimaanisha hivi: Coca-Cola imeajiri zaidi ya watu 800 (mathalan), na kati ya hao wapo ambao wanafanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa, lkn kwa bahati mbaya yupo mmoja au wawili wenye tabia hii ya uzembe. Nilichomaanisha mimi ni kuwa, kama itabakia tabia hi ya kipuuzi ya kupiga kelele bila kuchukua hatua, basi kitakachotokea ni kwamba watu wataacha kutumia bidhaa na hapo ajira za hata wale walio waaminifu napo zitakuwa mashakani. Cha muhimu kufanyika ni kufikisha jambo hili panapohusika ili uchunguzi ufanywe na aliyehusika achukuliwe hatua kwa kusababisha athari kwa afya za watu.
3. Nikukumbushe kuwa ni sheria za Tanzania ndio zinafanya mtu awe huru kufanya makosa na kuendelea kuwepo kazini. Ikiwa wewe leo umeona hili na unaacha kuchukua hatua badala yake unaanzisha mahubiri, lengo ni kumkomoa mwenye kiiwanda au kurekebisha jamii yetu? Hivi kweli huna akili hata kidogo kiasi uone kuwa si lengo la mwekezaji ila ni tabia zetu?
4. Unaposema unadhalilishwa kama Mtanzania, ina maana wewe ulitaka niseme kuwa kama Mlinzi ameacha geti wazi mali zikaibiwa hilo ni kosa la Managing Director kwa hiyo anatakiwa akomolewe au?
5. Upumbavu ni mzigo ndugu yangu. Wewe unaona mimi nawalamba miguu wazungu kwa kuwa tu nimehimiza watu wawajibike na kuwa waaminifu kwa mikataba yao. Unajua maana ya ajira? Au unafikiri kuna mwekezaji ambaye huwekeza kwa lengo la kukuajiri wewe na sio kupata faida?
Nimalizie kwa kukwambia kuwa mimi sio wa level yako ya kufikiri. Nimezingatia mambo haya kabla sijasema lolote juu ya hii mada:
1. Upo uwezekano yanayosemwa ni uzushi kwa lengo la kuharibu biashara za watu wengine. Kama kuna ukweli wa hili kwa nini kuna ugumu wa kulifikisha kwenye vyombo husika ili kiwanda kichukuliwe hatua? Wewe ukibakwa au kuibiwa, utaenda polisi au utakuja JF kubwabwaja?
2. Si mara ya kwanza kwa watu kufanyiana kampeni chafu kushindania soko. Kama kweli jambo hili ni dhahiri, nini kinawazuia waliokutana na mikasa hii wasiende kwenye dola?
3. Coca-Cola ni mwekezaji, anawekeza ili afanye biashara kwa hiyo msingi pekee wa kuwepo hapa ni biashara kwa hiyo sidhani kama management inaweza kuona posibility ya jambo kama hilo halafu ikae kimya.
Ubongo sifuri, lugha sifuri: Suprise visits, Angalau na Twice a month.
Na kumbe unajua kuwa kuna mashirika ya viwango sasa juu ya nini kesi kama hii isipelekwe huko badala ya kupiga kelele za kidemudemu hapa.