- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii,
"Soda ya Sprite (ya baridi) tunayoambiwa kusukutua nayo mdomoni baada ya kung'oa jino huwa ni tiba ya kweli ya maumivu au ni imani?"
"Soda ya Sprite (ya baridi) tunayoambiwa kusukutua nayo mdomoni baada ya kung'oa jino huwa ni tiba ya kweli ya maumivu au ni imani?"
- Tunachokijua
- Meno/Jino yanaweza kung'olewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuoza sana kwa jino, magonjwa ya fizi au mahitaji ya kurekebisha mpangilio wa meno (orthodontic)
Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X amechapisha taarifa katika muundo wa swali kuuliza iwapo unywaji wa soda aina ya sprite ya baridi inaweza kuwa tiba kwa mtu aliyeng'oa jino?
Uhalisia wa madai hayo
Vyanzo mbalimbali vya afya vimeeleza kuwa baada ya kungo'oa meno miongoni mwa vyakula ama vinywaji ambavyo vinapaswa kuepukwa ni pamoja na soda pamoja na vinywaji vingine vyenye gesi.
Tovuti ya kituo cha tiba ya meno Dallas Marekani kupitia makala yao wameeleza kuwa ni muhimu kuwa makini na mpangilio wa mlo baada ya kung'oa meno ikiwemo kutotumia baadhi ya vinywaji na chakula ili kuepuka kuchelewesha kupona, kuongeza maumivu au hatari ya maambukizi.
Tovuti ya omah dentists inaeleza kuwa mtu aliyeng'oa meno anapaswa kuepuka vinywaji vyote vyenye gesi ikiwamo soda ili kutovuruga uthabiti wa damu iliyoganda katika eneo lenye kidonda.
Wanaendelea kueleza kuwa kunywa soda ama vinywaji vingine vyenye gesi kunaweza kusababisha madhara, kuchelewesha mchakato wa kupona, na kuongeza usumbufu.
Tovuti ya Dr. Mgordon inaeleza kuwa vyakula na vinywaji ambavyo vinapaswa kuepukwa ni soda na vinywaji vingine vyenye gesi, vyakula ama vinywaji vya moto, vyakula vyenye viungo vingi, vyakula vigumu au vya kutafuna tafuna.
JamiiCheck imewasiliana na
Dkt. Majaliwa Mzungu kutoka Mkoani Health Center ambaye ameeleza kuwa;
Hakuna kitu kama hicho, hizo ni imani ambazo kisayansi hazina ukweli na hakuna Wataalamu wanaofanya hivyo.