36“Hakuna ajuaye siku wala saa, hata
malaika mbinguni hawajui wala Mwana, ila Baba
peke yake. 37Kama ilivyokuwa wakati wa Noa,
ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa
Adamu. 38Kwa maana siku zile kabla ya gharika,
watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na
kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia kwenye
safina, 39nao hawakujua lo lote mpaka gharika
ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo
itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu.
40“Watu wawili watakuwa shambani, mmoja
atatwaliwa, mwingine ataachwa. 41Wanawake
wawili watakuwa wanasaga pamoja, mmoja
atatwaliwa, mwingine ataachwa.
42“Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni
siku gani atakapokuja Bwana wenu. 43“Lakini
fahamuni hili kwamba: Kama mwenye nyumba
angelijua ni wakati gani wa usiku ambao mwivi
anakuja, angelikesha na asingeliiacha nyumba
yake kuvunjwa