Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Sofa bed inafaa sana pale hali ya uchumi inapokuwa na changamoto na unalazimika kupanga chumba kimoja. Unaamka asubuhi unaangalia vitu vyote unavyomiliki. Kuna kitanda, jiko, ndoo ya kuogea na ndoo ya maji ya kupikia.
Kuna wale wanaosoma mchana anahitaji kuwa na meza ya kusomea na wengine hupata wageni kwa discussion. Wengine wanaishi chumba kimoja na wanafanya biashara, wateja wanafuata bidhaa nyumbani.
Mchana unatoa godoro unakunja kitanda na kuweka mito ya kukaa. Watu wanaotumia sofa bed wanaongezeka.