SoC03 Soka huzuni mpaka burudani

SoC03 Soka huzuni mpaka burudani

Stories of Change - 2023 Competition

web developer

New Member
Joined
Feb 21, 2017
Posts
3
Reaction score
1
Mwaka 1993 kwenye Fainali ya CAF Kwa Sasa Shirikisho kwenye uwanja wa  Uhuru timu ya  Simba ilipoteza Kwa kupigwa magoli mawili dhidi ya Stella Club d'Adjame ya Ivory Coast, hali iliyopelekea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo Mh. Ally Hassan Mwinyi (Mzee wa ruksa) kutokwa na maneno yasemayo Tanzania katika mpira wa miguu ni kichwa cha mwendawazimu, ambapo kauli hiyo aliifuta rasmi mwaka 2018.

Kwangu mimi naona kauli hiyo Mzee wa Ruksa asingeifuta kwani si Simba, Yanga wala Timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) zilizo tuletea Makombe yanayohusisha mashindano ya bara la Afrika wala Dunia.

Naomba niongelee hii timu ya wote yaani Timu ya Taifa (Taifa Stars), kwangu mimi uwajibikaji wa timu yetu hii naona unachangamoto kubwa kwa sababu mbinu tulizo zitumia tukashindwa mara kadha wa kadha ndio hizo hizo tunazo endelea nazo namaanisha sisi kazi yetu ni kubadili walimu (makocha) na kufanya hamasa zaidi kwa upande wa mashabiki ili hali mzizi wa tatizo bado viongozi wetu hawawajibiki nao.

Inauma na inahuzunisha, Mashabiki tunahamu na shauku kubwa ya kuhakikisha tunaishangilia Timu ya Taifa 'Taifa Stars' lakini Matokeo huwa yana tunyong'onyesha, ila hatukati tamaa na hatutakata tamaa milele kuishabikia Timu yetu Taifa Stars.

Tanzania tuna mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu kwa wanaume kuanzia Ligi kuu na zile ligi za vijana chini ya umri wa miaka 20 na 17, haitoshi mashuleni tuna UMISETA na UMITASHUMTA lakini bado mafanikio yake au mchango wake kwa Timu ya Taifa na zile timu za Taifa za vijana ni madogo/mdogo sana na hii hali husababishwa na uwajibikaji wa kiwango cha chini kwa viongozi wanaohusika na masuala ya mpira wa miguu nchini.

Sio hivyo tu, Inaonekana mahusiano ya kiutendaji baina ya wizara ya michezo na wizara ya elimu bado sio bunifu, kwani miongoni mwa jukumu la utawa bora ni ushirikishaji namaanisha viongozi wa wizara ya elimu na michezo bado hazina mshikamano wa uwajibikaji kwa kuzingatia wanasahau maisha ya wengi yaani watanzania bado hatuna furaha na matokeo ya michezo kwa timu yetu pendwa Taifa Stars.

lakini haki na usawa bado ni changamoto kwa viongozi wetu wanao simamia masuala ya mpira wa miguu kwani kuna vipaji vingi vimejificha vijijini na mijini na vinazidi kupotea huku wakiacha historia kwenye ligi za ng'ombe na mbuzi kwa ufundi wao wa kulisakata kabumbu na sio historia kwa nchi.

Haitoshi, wachezaji wetu wa ndani wakipambana kuifikisha timu Ligi Kuu huwa wanashushwa thamani kwani watasugua benchi na mwishoe watarudi kwenye ndondo cup. Kukosa kwao namba inapelekea kuua vipaji vyao pia na inayoathirika ni Taifa Stars na sisi tuliowatazama safari yao kuanzia mpira wa makaratasi mpaka Ligi Kuu, hali inayo ondoa hamasa ya safari ya kuchezea timu kubwa na Taifa kwa vijana wengine.

Ili tuwe na furaha kama raia wa Argentina walivyo furahi kwa kupata ubingwa wa kombe la Dunia mwaka 2022, au tufurahi basi kwa kufika hata hatua Moroko iliyofikia kwenye kombe la Dunia mwaka 2022, au tufurahi nasi kwa kuwa bingwa wa AFCON au bingwa wa CHAN basi mabadiliko yanahitajika. Kuwa bingwa kuna raha yake jamani lakini haya yote tunayopitia ni kwa sababu viongozi wetu wanakosa ubunifu katika utendaji wao wa kazi, kwani bila ubunifu kila siku tutahuzunika na pengine tutazidi kutokwa na machozi kwa upendo tulio nao kwa nchi yetu.

Nikikumbuka baadhi ya maneno bora kutoka kwa Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alituhasa kwa kusema ukikosoa basi uje na mikakati au tiba ili nchi yetu izidi kuendelea, kutokana na maneno hayo sina budi kuweka wazi mitazamo yangu juu ya soka la Tanzania ili nasi baada ya miaka kumi au kumi na tano tujivunie kwa kuwa na kikosi bora cha Taifa Stars kitakachobeba makombe.

Kitu muhimu katika maendeleo ni mahitaji na siku zote huwa hayatoshi lakini kama viongozi wetu watakua waadilifu basi uchache huohuo utaleta faraja kwetu watanzania.

Kwanza tuwekeze katika kupata walimu bora wa mpira wa miguu na waende kuzihudumia kata zote nchini, pia tuwe na maafisa weledi wa michezo kwa ngazi ya wilaya, mikoa na Taifa. Pia kila kata ijenge uwanja wa mpira wa miguu wa gharama nafuu lakini kiwe bora kwa mazoezi na mashindano.

Wizara nayo ijenge viwanda vya kuzalisha vifaa vya michezo na itenge bajeti ya kupeleka vifaa hivyo ngazi za kata.

Serikali pia ilazimishe vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya ualimu yaongeze mafunzo ya walimu wa mpira wa miguu kwa kipekee na walimu hao wakihitimu wasambazwe kata zote nchini na kuwapa majukumu yenye tija kwa nchi ikiwepo aunde timu ya kata na kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindao yaani atafute vipaji na aviboreshe kwa ubora sahihi, nae afisa michezo wilaya aendeshe ligi za timu za kata na kupitia hao hao walimu kwenye vikao nao wachague timu ya wilaya na moja wao kama mwalimu wa wilaya, afisa michezo mkoa nae aendeshe ligi za kushindanisha wilaya na mwishoe kupitia vikao na hao walimu wa wilaya watoe timu ya mkoa na mwalimu wa kuwaongoza huku ngazi ya Taifa waandae ligi ya kushindanisha Mikoa na watoke na timu ya Taifa na Makocha kutoka kwa hao hao walimu ili waiboreshe timu ya Taifa.

Ifanyike ivyoivyo kuwapata walimu wa magolikipa na viungo na iwe ni muendelezo.

Ili tuwe bora zaidi chama cha mpira nchini kitafute mechi za kirafiki kila mwaka angalau 7 mpaka pale tutapofikia malengo yetu.

Ili hayo yaweze kufanyikiwa uwajibikaji wa kila mmoja unahitajika na uongozi ulio bora zaidi na unaofuata sheria bila kusahau misingi ya haki na usawa.

Hakuna mkate mgumu ndani ya chai, sio nasema mimi ni uhalisia namaanisha tukiamua kuwajibika katika mpira wa miguu na uongozi ukasimama imara basi tutegemee furaha tele kutoka kwetu wenyewe.

Tujue pia wachezaji wetu watapanda thamani, wataingia mikataba na timu kubwa na umasikini kwao na familia zao utaondoka na Taifa tutapanda katika viwango vya soka duniani.

Pia mashirika ya umma na binafsi ya vyombo vya habari yaweke nguvu yake kutangaza mechi zote kuanzia hata ngazi za mikoa.

Ninaimani na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ni sikivu na yenye macho ya mbali kuwa wakiona wazo hili watalitilia maanani.

Yaani itakuwa ni muunganiko wa shangwe na kelele za furaha kuanzia vijijini mpaka mijini ndani ya Tanzania.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom