Soka la bongo na uchawi, Simba yapigwa faini kwa uchawi na vururgu

Soka la bongo na uchawi, Simba yapigwa faini kwa uchawi na vururgu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh. 500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Naye mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa kidole.

Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani na silaha kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Pia mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vilevile wamiliki wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wameandikiwa barua ya kufanya marekebisho ya vyumba vya wachezaji, kwa vile havina hewa ya kutosha.

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini kutokana na makosa mbalimbali ni Friends Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh. 200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi Morogoro (sh. 400,000) na Transit Camp (sh. 200,000).

Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro, John Tamba atapelekwa kwenye Kamati ya Maadili kutokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika mechi dhidi ya Burkina Faso.

Kiongozi wa Lipuli, Hamis Kiemba na wachezaji Boniface Sawaka, George Enock na Green Paul watapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kutokana na utovu wa nidhamu waliofanya kwenye mechi dhidi ya Kimondo.

Naye mchezaji Sangalau Nyamoka wa JKT Kanembwa aliyelalamikiwa uhalali wake na Polisi Tabora suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.

Credit: shaffihdauda.com
 
Hivyo vitendo vya ushirikina ni vipi? Isije ikawa Kamati ya Ligi ndiyo iliyorogwa kuona visivyokuwapo!
 
kabla ya yanga kufunga goli lake,katika match na alahly alikuja mtu kama mwandishi wa habari na kamera yake nyuma ya goli la Alahly, baada ya dakika kama 5 goli likafungwa, jamaa akaijisahau akaenda kushangilia na wafungaji wa yanga, baada ya kushangilia akaondoka eneo la tukio, huo nao tuuiteje
 
Hapo kwa mtazamo wang huyo aliona move ya goli akaenda kulipiga picha si umesema alikuwa na kamera?
 
Simba walozi wakubwa. Aibu kubwa sana hii
 
kabla ya yanga kufunga goli lake,katika match na alahly alikuja mtu kama mwandishi wa habari na kamera yake nyuma ya goli la Alahly, baada ya dakika kama 5 goli likafungwa, jamaa akaijisahau akaenda kushangilia na wafungaji wa yanga, baada ya kushangilia akaondoka eneo la tukio, huo nao tuuiteje

WACHAWI FC aka MIKIA FC aka wapiga ramli wa bunju...jamaa kwa mizizi na matunguli ni noma
 
Simba walozi wakubwa. Aibu kubwa sana hii

Wanga tu hao hawana lolote, za mwizi arobain wamekamatwa mchana kweupe wakiiwangia MBEYA CITY wakamloga na refa na refa na refa aliyechezesha mechi yao na mtibwa mpaka akatoa kadi nyekundu wakamtoa ufaham refa akawa anawabeba bila kulaga SIMBA hawajashinda bado
 
WACHAWI FC aka MIKIA FC aka wapiga ramli wa bunju...jamaa kwa mizizi na matunguli ni noma

"wameambukizwa na rage mzee wa mguu wa kuku, manake rage mchawi balaa"

nimemnukuu shabiki wa simba
 
kuna mshikaji m1 huwa anajisifu maskani kwamba eti naye alichangia ushindi wa nani mtani jembe sababu usiku wa kuamkia

game eti nae alienda kulala makaburini ili kufanikisha ule ushindi,jamani simba wanamambo!..
 
kwani ulikuwa hujui? Simba ndo zao hizo kuloga viwanja na kuloga timu pinzani
TFF wanashindwa kuheshimu kauli za vilabu kwamba huo si uchawi, ni Ufundi. Mbona ni utaratibu kuwa na madawati ya Ufundi kwenye timu?
 
Vitendo vya kishirikina ni vipi mbona habari haijakamilika?
 
Ni aibu kwa TFF ambayo inaamua kwa niaba ya selikari kuamini ushirikina Kumbukeni selikari haiamini uchawi
 
Ni aibu kwa TFF ambayo inaamua kwa niaba ya selikari kuamini ushirikina Kumbukeni selikari haiamini uchawi

Ni aibu zaidi kwa klabu kubwa kama Simba kujihusisha na vitendo vya ushirikina.
 
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh. 500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Naye mshambuliaji wa Simba, Amisi Ta
 
Back
Top Bottom