Soka la bongo na ufadhili wa watanzania wenzetu wenye asili ya Asia

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
Wakuu heshima mbele, nimewiwa kuandika hii sredi baada ya kufuatilia historia ya muanzilishi na mmiliki wa limbe leaf baadae Tukuyu stars Ramnik Patel, kwa ufadhili wa huyu mhindi Tukuyu stars ilikuwa bingwa mwaka 1986, ikashuka daraja 1987, Ramnik akapambana akairudisha ligi kuu mwaka 1988 na kuikabidhi kwa mkuu wa wilaya wa kipindi hicho baadae ikapotea kimya kimya, hawa watanzania wenzetu wamekuwa wafadhili wa soka letu tangu enzi na enzi, wengi wetu tunawafahamu Manji kwa upande wa yanga na familia ya akina Dewji kwa upande wa simba, naomba tuweke rekodi sawa katika uzi huu kwa kuwakumbuka wengine ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa soka letu, tuwakumbuke tuwaenzi, mie nimeanza na Ramnik Patel Kaka wa Tukuyu stars banyampala, wana koma kumanya......RIP KAKA.
 
Azam ni wamiliki wake wana asili ya uarab

Simba mmiliki wake ni muhindi

Wadhamini wa mbao gf truck ni kampuni ua wahindi

Stand united inadhaminiwa na maji ya kampuni ya jambo ambayo mmiliki wake ni mwarabu

Tujiulize hivi hamna mswahili yoyote mwenye hela ya kudhamini timu mojawapo ya ligi kuu au ndyo ile kasumba ya ubinafsi ndyo imeshika kasi?
 
Mkuu ndio hoja niliyotaka tushirikishane hapa, hawa wenzetu wamekuwa mstari wa mbele sana katika kulibeba soka letu, ni muhimu tuwakumbuke na kuwaenzi.
 
Mkuu tuulize wenye lugha yetu hatuna banyampala tuna BHANYAMBALA...KOMA KUMWANYA
 
Mkuu tuulize wenye lugha yetu hatuna banyampala tuna BHANYAMBALA...KOMA KUMWANYA
Nashukuru kwa marekebisho mkuu, tuendelee kuweka rekodi zetu sawa kwa kupeana yale tusiyoyajua kuhusu hawa wenzetu.
 
Nashukuru kwa marekebisho mkuu, tuendelee kuweka rekodi zetu sawa kwa kupeana yale tusiyoyajua kuhusu hawa wenzetu.
Katika uhalisia wake michezo ni morale na morale inabustiwa na fedha hawa wenzetu baniani wanamwaga fedha za kutosha kwenye michezo yote sio soka tu nenda gymkhana yote Ile ni wao tu njoo motor racing countrywide ni wao...kwa uchache wametushika si tu kwenye michezo hata sekta nyinginezo ingawa ni waoga kuwekeza kwenye real Estate sector nadhani bado ule mzimu wa Idi Amini kuwatimua wenzao haujawatoka...wahindi hoiyee
 
Nilikuwa inspired kuandika haya baada ya kusikiliza mahojiano ya Ramnik namna alivyoamua kuwasaidia vijana wa mtaani kwake mwaka 1982 ambao baadae ndio ikaja kuwa Tukuyu stars, hawa wenzetu wana moyo wa kipekee kabisa, most of them have passion with football and other games as you have mentioned above, bado wametushika kwenye golf, swimming, racing za magari na pikipiki nk, kiukweli hawa watu wanazaliwa wanamichezo, nafikiri ni kwenye riadha tu ndio hatuwaoni sana hapa nchini.
 
Nilikuwa inspired kuandika haya baada ya kusikiliza mahojiano ya Ramnic
 
Wazawa tajiri ni Mengi tu...wengine wana fedha kidogo za kutosha familia zao
 
Wazawa tajiri ni Mengi tu...wengine wana fedha kidogo za kutosha familia zao
Sidhani, nafikiri wapo waswahili wenzetu wengi tu wenye cash labda hawajaona umuhimu wa kuwekeza kwenye soka, lakini kusema ki bongo bongo mzawa mwenye cash ni Mengi tu utakuwa wakosea mkuu japo sina facts za kusapoti hoja yangu.
 
Waswahili mbona wengi tu, kuna akina Zamunda wa African Lyon, James Bwire Aliance, timu zote za jeshi, akina Mwigulu, nk.
 
Yanga alikuwepo muhindi Abasi gulamali na Simba alikuwepo Azim dewji enzi zile.
 
alikuwepo Panone kabla yake alikuwa Kajumlo tatizo kwenye mpira kuna walaji wengi wakishagundua wanajitoa ulaji plus majungu
 
SSB sio mzawa? Ali Mafruki?
Naongelea top ten ya 2018..Bakhresa hana asili ya Tanzania kwao Oman ila ana makaratasi ya Tanzania(passport)... Mfuruki sio tajiri ana hela ya kusomesha watoto ng'ambo
 
alikuwepo Panone kabla yake alikuwa Kajumlo tatizo kwenye mpira kuna walaji wengi wakishagundua wanajitoa ulaji plus majungu
Hivi Merey Barabuu wa Moro United na ni mzawa mwenye asili ya Asia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…