kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,521
- 2,747
Wakuu heshima mbele, nimewiwa kuandika hii sredi baada ya kufuatilia historia ya muanzilishi na mmiliki wa limbe leaf baadae Tukuyu stars Ramnik Patel, kwa ufadhili wa huyu mhindi Tukuyu stars ilikuwa bingwa mwaka 1986, ikashuka daraja 1987, Ramnik akapambana akairudisha ligi kuu mwaka 1988 na kuikabidhi kwa mkuu wa wilaya wa kipindi hicho baadae ikapotea kimya kimya, hawa watanzania wenzetu wamekuwa wafadhili wa soka letu tangu enzi na enzi, wengi wetu tunawafahamu Manji kwa upande wa yanga na familia ya akina Dewji kwa upande wa simba, naomba tuweke rekodi sawa katika uzi huu kwa kuwakumbuka wengine ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa soka letu, tuwakumbuke tuwaenzi, mie nimeanza na Ramnik Patel Kaka wa Tukuyu stars banyampala, wana koma kumanya......RIP KAKA.