Soko huria ndiyo sababu kubwa inayofanya nchi za Kiafrika zisiendelee

Shukrani, nitamfuatilia. Inaonekana tunayofundishwa kwenye formal education na yanayofanya kazi duniani ni mambo tofauti kabisa. Nilivyosoma tu Bad Samaritan nikaona jinsi ambavyo situation yetu ni hopeless.
Sasa Kuna jamaa hapo naona kakomaa na soko huria;inabidi kushika tama tu.


Kuna Aina zaiidi ya 8 za chumi;A,B,C,D,I,M,N,K.

Sasa chumi ya Neo classical Economics ambayo ndio imeshika mpini katika nyakati hizi pamoja na vyuo na shule uchumi ndio inasambaza fleva hizi za sokohuria,demokrasia ,Haki za binadamu na fleva kibao.


Neo classic economic miaka ya 70s -80s ndio ilianza kupata nguvu kubwa Sana mpaka hivi sasa.


Pamoja na mapungufu ya mwalimu kambarage nyerere katika kuendesha uchumi wa Tanganyika/Tanzania ;ambaye mzee Lee yuan Kew Waziri mkuu wa zamani wa singapore alimuelezea Kama MTU asiyejua hata abc Za uchumi/simple economic katika interview PBS USA 2001...lakini mzee huyu katika Kitabu chake cha From third world to first world Singapore ndani ya Ku rasa 370 Alisema

"Nyerere was the Africa leader I most respected"

Anahoja nzinto na zilizoshiba kuhusu Soko huria;IMF & world Bank , ni jambo lakufatilia interview za mwalimu na hotuba zake..
 
Mimi ujinga wa kufunga mkanda wasiniambie wkt wao viongozi wanakula kiyoyozi Cha V8,huku wakinywa Hennessy.Siko tayari kwa Hilo,kila mtu apambane na hali yake.
Hahahahahahah kufunga mkanda tutafunga kwenye siti za gari tu ila kimaisha kila mtu apambane kivyake😅
 
Si kweli.
Afrika ni masikini sababu Ina viongozi masikini wa fikra
 
Viongozi wenyewe wakiwa wazalendo wanaondolewa kama Gadafi, Sankara nk.
 
Soko huria tumeshindwa litumia tusitafute visingizio kuhalalisha uvivu wetu.
 
Wa hovyo yupoje
Hao mnao walalamikia kila siku.
Wameshindwa kuwafanya muwe kama ulaya.
 
Si rahisi kwa viongozi wa nchi karibu hamsini wote kuwa maskini wa fikra.
Kwann sasa hali za uchumi za nchi karibu zote za afrika ufanana.
Angalau kidogo nchi za kiafrica ya waarabu wao Wana nafuu kidogo mfano Libya, tunisia Misri Morocco Mauritania Mauritius Algeria.
Nilifanya research sababu ya mfumo wa uongozi wa dini ya kiislamu unakataza mtawaliwa kuwatendea mabaya wataliwa hofu ya kwamba siku ya mwisho utaulizwa angalau kidogo imepunguza wizi,rushwa, ufisadi, ukabila,nk.
Wananchi wa hizo nchi angalau wanamudu kupata basic needs tofauti na hizi nchi za kiafrica za weusi.Mambo ya hovyo hovyo mfano uswahilini,slams, umasikini vijijini unakuta karibu nchi zote za afrika ya weusi.
 
Sisi waafrika ndio tunashindwa watumia weupe Ili tuendelee, huwezi ukaendelea bila kushirikiana na watu wa magharibi nchi zote zilizofungua milango au shirikiana nao zimeendelea zingine tulikuwa nazo sawa au achana kidogo kiuchumi.
Malasyia, Philippines, singapore,falme za emirates, china, vietnam.
 
Tunaweza lima chochote na kuuza popote duniani bila kizuizi chochote maadamu tu tumeet standard.
Na sio hii ya kubikiri matunda hayo tuuziane sisi wenyewe.Kubikiri matunda ni kitendo cha kuchuma matunda mabichi machanga na kuyalazimisha kuiva kwa lazima Ili yaingie sokoni.
 
Mauritania ni nchi maskini afadhali yetu. Na hii Mauritius asilimia kubwa ni wakatoliki na wahindu. Nafikiri sababu kubwa ya nchi za kaskazini kuwa vizuri ni Geography yao. Wapo karibu na Ulaya na wanaaccess ya hilo soko kwa urahisi. Na hawa wamekuwa na muingiliano na Ulaya kwa maelfu ya miaka. Tena maendeleo yao yalitakiwa kuwa level ya nchi za Ulaya. Nchi kama Morocco inapokea watalii zaidi ya 10m kwa mwaka, huku sisi hatufiki hata 1.5m. Na kingine ni kuwa wengine, kama Libya na Algeria wana rasilimali nyingi sana za mafuta na gesi.
 
Kwa raslimali nchi za afrika ya weusi ndizo zinaongoza kwa madini,gasi,mafuta,mito,ardhi zenye rutuba,nguvu Kazi ya kutosha,hali nzuri ya hewa.
Shida ipo kwenye maendeleo ya fikra.
 
Hata mwafrika mmoja mmoja aliyefanikiwa ni ngumu Sana kuwasaidia wengine nao wafanikiwe,hii wenzetu weupe wote ufanya kujitolea kwa jamii,mfano kujenga shule,visima,kusomesha,nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…