Mwanahisa
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 1,382
- 513
Ni wazi kua sasa imebidi tufungamanishe nguvu zetu kama wakazi wa Afrika Mashariki, ili kujikimu na mwenendo wa kiuchumi, tamaduni hata kisiasa katika ukanda wetu huu. Jana ikiwa siku ya jumapili tarehe 20, nilifika sehemu ambayo hua nafuata huduma ya kinyozi maarufu mjini kama Barber Shop,
Hapa kuna kitu kimeuteka ufahamu wangu na ndio maana nikaamua niiweke hii mbele ya jukwaa, huduma hii iko sehemu nyingi mjini na ni ya kawaida kabisa, ila kilicho cha ajabu katika hii sehemu ni watoaji wa huduma na wala sio huduma yenyewe. Huyu bwana anaetoa huduma hii nimekua nikimfuata toka ofisi moja hadi nyingine, kutokana na aina ya kazi yake na pengine akitafuta maslahi zaidi. Jana tukapata wasaa wakubadilishana mawili matatu kwani idadi ya wateja haikua kubwa, katika mazungumzo yetu nikagundua huyu bwana sio mtanzania, na hapa ndipo palipoipelekea picha nzima ya soko la afrika mashariki.
Watanzania wenzangu haitachukua muda mrefu kabla ya kugundua huduma na mtoa huduma ni kipi bora. Aliyeko ofisini, au popote pale sio kwamba unatumikia bakuli la bwana fulani hapana, unatoa huduma, na malipo unayopata ni kipimo tosha cha huduma unayotoa. Niwatakie siku njema.