Soko la Afrika Mashariki.

Soko la Afrika Mashariki.

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
1,382
Reaction score
513
Ni wazi kua sasa imebidi tufungamanishe nguvu zetu kama wakazi wa Afrika Mashariki, ili kujikimu na mwenendo wa kiuchumi, tamaduni hata kisiasa katika ukanda wetu huu. Jana ikiwa siku ya jumapili tarehe 20, nilifika sehemu ambayo hua nafuata huduma ya kinyozi maarufu mjini kama Barber Shop,

Hapa kuna kitu kimeuteka ufahamu wangu na ndio maana nikaamua niiweke hii mbele ya jukwaa, huduma hii iko sehemu nyingi mjini na ni ya kawaida kabisa, ila kilicho cha ajabu katika hii sehemu ni watoaji wa huduma na wala sio huduma yenyewe. Huyu bwana anaetoa huduma hii nimekua nikimfuata toka ofisi moja hadi nyingine, kutokana na aina ya kazi yake na pengine akitafuta maslahi zaidi. Jana tukapata wasaa wakubadilishana mawili matatu kwani idadi ya wateja haikua kubwa, katika mazungumzo yetu nikagundua huyu bwana sio mtanzania, na hapa ndipo palipoipelekea picha nzima ya soko la afrika mashariki.

Watanzania wenzangu haitachukua muda mrefu kabla ya kugundua huduma na mtoa huduma ni kipi bora. Aliyeko ofisini, au popote pale sio kwamba unatumikia bakuli la bwana fulani hapana, unatoa huduma, na malipo unayopata ni kipimo tosha cha huduma unayotoa. Niwatakie siku njema.
 
Lengo la story yako ni nini kutuonyesha kwamba tunapaswa kuchangamkia fursa za soko la Africa mashariki?
 
Mkuu hapa sijakusoma kabisa
Mkuu, ni hivii nilikua naangalia hiyo scenario ya tukio lenyewe kwani mm ndio nilikua muhusika mkuu, Watanzania swala la kuuza huduma hatupo, wengi wetu tunafikiria kumtumikia kafiri, kumbe sio kweli maana huyo kinyozi ninaemuongelea amejijengea clientele kubwa na wote tunamfuta kila anapohamia saloon mpya kutokana na huduma yake. KUUZA HUDUMA NI ZAIDI YA MTAJI WA HELA. Ni hayo tu mkuu!
 
Lengo la story yako ni nini kutuonyesha kwamba tunapaswa kuchangamkia fursa za soko la Africa mashariki?
Haswaa mkuu, ila ndio hivyo kunakuchangamka, na zaidi. Maana lazima tuwe na approach ya namna tunavyozichangamkia fursa hizi, hasa katika swala zima la Service Industy.
 
Haswaa mkuu, ila ndio hivyo kunakuchangamka, na zaidi. Maana lazima tuwe na approach ya namna tunavyozichangamkia fursa hizi, hasa katika swala zima la Service Industy.

kwenye red kwa nini isiwe customer care?
 
Mkuu, ni hivii nilikua naangalia hiyo scenario ya tukio lenyewe kwani mm ndio nilikua muhusika mkuu, Watanzania swala la kuuza huduma hatupo, wengi wetu tunafikiria kumtumikia kafiri, kumbe sio kweli maana huyo kinyozi ninaemuongelea amejijengea clientele kubwa na wote tunamfuta kila anapohamia saloon mpya kutokana na huduma yake. KUUZA HUDUMA NI ZAIDI YA MTAJI WA HELA. Ni hayo tu mkuu!

Mkuu sio kitu cha kuuliza, Watnzania katika swala zima La service tuko nyuma sana, wewe jaribu kutembelea Baadhi ya Maeneo mfano mahoteli, Baa, Maduka na kwingineko uone huduma zilivyo za kijinga, Unaweza fika Dukani Mhudumu anaongea na wewe wakati huo anabonyeza bonyeza simu,

Wewe unazani ni kwa nini wawekezaji wengi wanakuja na wafanya kazi wao? ni mambo kama haya
 
kwenye red kwa nini isiwe customer care?
Mkuu, customer care ni sehemu ndogo tu ya keki nzima ya Service Industry, kwa mfano karani wa mahesabu anatoa huduma ila hakutani na mteja uso kwa uso. Nilikua naangalia zaidi kwenye uadilifu na after service ili kujenga loyalty na watu unaowauzia huduma yako!
 
Back
Top Bottom