JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kwenye soko hilo maeneo ya biashara ni matupu hakuna wafanyabiashara, vizimba vipo wazi hakuna shughuli za kibiashara zilizokusudiwa ambazo zinaendelea kwenye soko hilo.
Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa tovuti ya Manispaa ya Kinondoni awali ilieleza tija mbalimbali zinapatikana kwenye soko hilo, ambazo ni pamoja fursa za urasimishaji kwa wafanyabiashara,
Ajira na kujiajiri, Fursa za usafirishaji mizigo na abiria,Fursa za elimu ya biashara.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwenye tovuti ya Manispaa ya Kinondoni Soko la Bwawani ni mradi ambao umetekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kwa (Package 6) kwa gharama ya fedha za kitanzania shilingi bilioni 1.
Basi kama mamlaka zimeshindwa kusimamia soko hilo la Bwawani ufanyike mchakato wa wazi ili miundombinu iliyopo itumike kwenye shughuli nyingine za kiuchumi ambazo zinaweza kuingiza mapato kuliko kinachoendelea kwa sasa, tutakuja kulipishwa mikopo ambayo haijaleta tija kutokana na uzembe wa Watu wachache ambao wamepewa dhamana kwa kushindwa kuwajibika na kuwa wabunifu.