Soko la DRC huwa tunagawana na Tanzania pasu

Kwa mahesabu ya kichekechea, hawana shilingi sawa, lakini kwa wabobezi wa hisabati na takwimu za kiuchumi huwa wana uwezo wa kuona na kudadavua nambari kwa kutumia akili za kujiongeza. Sasa inategemea na mwisho wa uwezo wako kifikra...hehehehe
Hapa Mkuu tunatafuta tafsiri ya neno "Pasu" pengine umesahau
 
Cha msingi ni infrastructure/miundo mbinu na kwa Sasa Kenya iko sawa sio mambo na route ama distance. Mjaribu kuikwamua SGR yenu from Kibaha angalau mfikishe Morogoro (200km). SGR Kenya ni km600 na tayari inafanya Kazi so tayari tumefupisha umbali kwa mkongomani.
 
Hapa Mkuu tunatafuta tafsiri ya neno "Pasu" pengine umesahau
Tz na DRC ni majirani ila Kenya na DRC sio majirani ila mizigo yao mingi inapitia Mombasa. Nilitegemea 100% ipitie Tz kwa kuwa border ni moja ila Infrastructure ya Tz ni poor.
 
Hamtafanya lolote Tanzania na Kongo biashara yake itakuwa kubwa sana, SGR ikikamilika.

Refer mazungumzo ya Rais Magufuri na Felix pale magogoni
Maneno ya wanasiasa wasikutie tumbo joto...je wafanyibiashara wataweza...au uzalishaji wenu wa bidhaa ni kiasi gani
 
Last december nilitembelea nilivyokuwa likizo, niliona mabasi na malori mengi sana yakitoka Dar - Lubumbashi.
Route ipo ndio, ila ni ndefu sana na ina challenge ya security...hasa hicho kipande cha kutoka kasumbelesa hadi Lubumbashi.

Kigoma port ikifanyiwa maboresho ni njia Fupi zaidi. Au SGR ipite Kigali tu eastern Congo hapo ndio mambo yatakuwa rahisi zaidi.
 
Hapa Mkuu tunatafuta tafsiri ya neno "Pasu" pengine umesahau

Hivi tafsiri ya neno 'relativity' kwa kiswahili nini, naomba msaada kwa yeyote. Kapige darasa nadharia ya relativity....
 
Hiyo takwimu ya hizo dollar ni kwa formal sector ambazo zipo regulated na mamlaka husika mipakani na kikodi, huku kusema mtaenda sambamba kwenye soko la DRC na Tanzania ni kujidanganya

Tanzania ndio inalisha Eastern Congo almost yote kuanzia mahindi, mchele na nafaka zote, nikija kwenye dagaa sasa ndio usiongee, pale mwaloni kirumba kuna semitrela zaidi ya 100 kwa giza zinapeleka dagaa DRC almost yote, hizi ni biashara za mabilioni ya shilling ambazo mara nyingi haziwi regulated na authorities kama za viwandani na bandarini

Ikumbukwe tu Tanzania ina njia zaidi ya 8 za kuingilia DRC, cheki hii

Nikajua unasema SGR yenu imefika Congo..hahaha kwani ni wapi bongo infrastructure sio nzuri? Barabara za lami zipo hadi Congo direct, kuna reli ya kati hadi kigoma port.

Subiri kipande cha isaka Kigali kianze, Wewe baki na maneno ya kibaha. We won't fail as you guys.
 
Tz na DRC ni majirani ila Kenya na DRC sio majirani ila mizigo yao mingi inapitia Mombasa. Nilitegemea 100% ipitie Tz kwa kuwa border ni moja ila Infrastructure ya Tz ni poor.
Takwimu zipi mmeizidi Tanzania kwenye mzigo wa DRC? Sio unatapika tu hapa mataputapu ya kwa mama nginyii bila mpango, leta facts.
 
Tz na DRC ni majirani ila Kenya na DRC sio majirani ila mizigo yao mingi inapitia Mombasa. Nilitegemea 100% ipitie Tz kwa kuwa border ni moja ila Infrastructure ya Tz ni poor.
Hii ni kweli mizigo ilipita Mombasa ila sio mingi Kama Unavyosema hapa. Na hilo limeshafanyiwa utatuzi na rais wa Congo alienda bandarini pale na kuona mashine mpya za kuongeza uwezo wa kupakua mizigo. Two times ya uwezo wa sasa. Hivyo kaeni mkao wa kutoa chozi.

Ile delay sababu ya handling na charges kisa meli zinashindwa ku offload on time limekwisha.
 
Tz na DRC ni majirani ila Kenya na DRC sio majirani ila mizigo yao mingi inapitia Mombasa. Nilitegemea 100% ipitie Tz kwa kuwa border ni moja ila Infrastructure ya Tz ni poor.

Le me use the Kenya's common phrase. This is verbal dysentery.
 
A
Acha kuwaza bila kuwa realistic, Tz. haitegemei ziwa tu kuingia Kongo tuna mpaka wa kuingilia Zambia na ndio maarufu na upo wa kupitia Burundi na wa Rwanda.
 
Miundombinu ya kuishambulia DRC
 
Takwimu zipi mmeizidi Tanzania kwenye mzigo wa DRC? Sio unatapika tu hapa mataputapu ya kwa mama nginyii bila mpango, leta facts.
Tz imesafirisha mizigo worth $153million , Kenya $150 million na ujue Tz shares a 500km border with DRC. Unyinge wenu ni kutokubali mapungufu yenu, nakwqmbia Kama ni Kenya ingekuwa inashre mpaka na DRC na Rwanda 100% ya mizigo yao yote ingekuwa inapitia Kenya.
Kama infrastructure ni nzuri MBONA hata mizigo ya Rwanda inapitia Kenya? Mbona mizigo ya Kongo inapitia Kenya?
 
Hizo ni preference baina ya mteja na mteja kuamua apitishe mzigo wake wapi. Sio kwamba wanapitishia Mombasa kisa ubovu wa miundombinu. Na ni kwamba automation bandari ya Dar ilikuwa chini kidogo. Ila saiv efficiency imeongezeka two times hivyo mjipange
 
Huyu si bado mgeni ndio kachukua madaraka hawajui vizuri WAKORA wanaokuchekea kijino pembe kumbe wanakuweka sawa wakuibie!!! sijajua dhahabu ya mwarabu kama imerudishwa ama bado anasubiri kuanza kutimiza azma yake ya kuwakata vichwa atakaokutana nao?? yetu macho....Mugabe ndio anawajua vizuri watu hawa na aliwapiga marufuku kukanyaga nchini mwake........ila nafikiri kashabadilisha gia hewani baada ya kupata taarifa sahihi.....alipochaguliwa tuu ...kiguu na njia wa jamaa anayemiliki ardhi kibepari kwa docrine ya (WILLFU BUYER and WILLFUL PURCHASER),,, Akapewa somo wee alipotaka kuingia kingi juzi tu aka NGASTUKA KABISA na kujisalimisha kwa MZEE WA HAPA KAZI TUU. Kama ilivyokuwa kwenye snario ya bomba la mafuta la HOIMA.Tehe....Tehe.....Tehe!!! usiombe mtu aliyekuwa amesinzia halafu unachukua hiyo nafasi kujinufaisha siku akiamka HAWEZI KUFUMBA HATA JICHO MOJA...Anakaba kila kona.....1. Sasa hivi tumerudisha milki ya mlima wetu......2.Tumezungushia uzia na tunauza madini yetu tena yameandikwa made in Bongo........3. Wamejua sasa serengeti ni yetu..... 4. Hata milki ya lugha adhimu ambayo zamani walipotoshwa kwa misamiati ya uongo sasa wametambua chenyewe halisi ni cha bongo na hawataki tena waalimu wapotoshaji...eti nimekuja kwa mulango nikatokea kwa dirisha...ile maneno...mnanielewa lakini?
 
Hivi tafsiri ya neno 'relativity' kwa kiswahili nini, naomba msaada kwa yeyote. Kapige darasa nadharia ya relativity....
Relativity = Uhusianifu

Lakini hakuna uhusianifu wa 10 na 10.2
 
Tz na DRC ni majirani ila Kenya na DRC sio majirani ila mizigo yao mingi inapitia Mombasa. Nilitegemea 100% ipitie Tz kwa kuwa border ni moja ila Infrastructure ya Tz ni poor.
Tanzania hatuna poor infrastructure ila tuna poor infrastructure in Kigoma region na huu ndio mkoa unaopakana na DRC kwa kiwango kikubwa.

Sasa hivi tumedhamiria buda tunaboresha bandari, those thieves wa bandarini tumefukuza wote na waliobaki they're on the track

Hatutaki ubabaishaji tena,mizigo ya wakongo 95% kama si 100% itapita Dar port SGR ikikamilika Isaka-Kigali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…