Soko la Dunia mafuta yameshuka, Tanzania yamepanda. Nchi hii bora liende

Soko la Dunia mafuta yameshuka, Tanzania yamepanda. Nchi hii bora liende

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Kama una simu janja fuatilia bei ya mafuta duniani huko kwa wazalishaji, bei zimeshuka sana lakini Tanzania kila leo hadithi hazina kichwa wala miguu.

Kiuhalisia wameshindwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali na hapo bado tutarajie bei za ndani ya nchi kupanda zaidi na zaidi maana hawana pesa hivo ni kudandia vikodi vya hapa na pale bila ufanisi.

Waendelee kuupiga mwingi tena binafsi nawapongeza sana kwa kuupiga mwingi hadi unamwagikwa kabisa.
 
Biashara ya oil ni cartel tupu, kuanzia wale wahuni wa OPEC mpaka waliopewa vibali kuagiza mafuta TZ,ukiwagusa lazima wakumalize na wana unlimited $$$ ni biashara ambayo imesababisha vifo na majanga makubwa sana kwa binadamu, hata Samia hana uwezo wa kugusa hiyo biashara, makampuni makubwa ya US na waarabu yanatengeneza billions na hakuna wa kunyanyua mdomo hata Biden kimya,lazima warudishe pesa yao maana mlipunguza kutumia mafuta wakati wa COVID mtalipa tuu sasa,
 
Kama una simu janja fuatilia bei ya mafuta duniani huko kwa wazalishaji, bei zimeshuka sana lakini Tanzania kila leo hadithi hazina kichwa wala miguu...
Badala ya kulialia wewe mwanaume jiue commit suicide. Shida zote hizi zitaisha utakuwa huru milele.
 
SA wao naona uvumilivu umewashinda
20220803_065444.jpg
 
" nchi hii iliongozwa na mshamba sana na dikteta uchwara" alisikika mlevi mmoja.
Kamatia humo humo mama. Vita ya Urusi imeleta inflation duniani na sisi sio kisiwa.
Waambie wanaoongoza kila mtu ale urefu wa kamba yake, akipandisha mabega mzingue
 
Kila Nchi Duniani Wanalia Kupanda kwa Bei ya Nishati sio Marekani wala Nani,sisi ni nani Tusiathirike na huku tunanunua Sehemu moja.Juzi Biden kaenda Saudia Kuomba waongeze Uzalishaji ili ku create supply kubwa bei ishuke ndo utajua Nishati sasa hivi duniani ni Janga.Srilanka wao walikua hawana kabisa mafuta nchi imeshindwa Kuagiza sababu ya Bei Kuwa kubwa na ela hakuna.Hatukatai serikali inatakiwa kufanya jitihada Kuwapunguzia ugumu wananchi wake na kuwalinda dhidi ya Janga hili la Nishati.Serikali hadi sasa imeshachukua hatua ili kupunguza bei lakini Bado bei zinapanda Sababu mafuta aya chimbwi maganzo wala Nanjilinji huko ni lazima tuagize sasa Ukiagiza kunavitu vingi vinapelekea mafuta kupanda Bei ikiwepo Thaman ya Dola dhidi ya Shiling watu wanajua haya lakini bado wanapiga kelele kama hawajui.Vita yoyote Kubwa duniani lazima italeta athari kwa ulimwengu mzima na tunalijua hili. Ndio maana ukipiga kelele sasa hivi unaonekana wewe ni Gang na masalia wa mwendazake, Sasa tulieni mama afanye kazi mbona watu walitulia wakati yule Novice and Naive Dictator alipokua anaharibu nchi kwa kukajaga Katiba na kutaka Kujisimika wa Milele na hakua anajua analo fanya Iweje sasa mnajitia Makelele?!!Enyi wafiwa tulieni.Muacheni nae Mama afanye Kazi na kwa hakika Kazi anapiga na inaonekana.
 
Yes tuendelee kulalama kwenye key boards, ila bei ya crude 🛢 kwenye soko la dunia imeshuka na Zambia wameshashusha bei pia, tuelewe factor mbili muhimu kwa bei ya mafuta ni world market price na UTHAMANI WA LOCAL CURRENCY, SOMA HII 1ZWK=142TSH!!!
 
Back
Top Bottom