Hujakosea sana ila nataka kidogo kuweka sawa. OPEC hawapangi bei ila wao wanalinda maslahi yao kwa maana wana kiwango cha chini cha bei hawapendi kishuke sababu ndio inakuwa budget yao na wengi ni dola 60$ kwa pipa katika kupanda inakuwa hawaingilii sana soko sababu hata wao hawana akiba kubwa waliyobaki nayo ila ikishuka chini ya 60 huwa wanakata uzalishaji.Biashara ya oil ni cartel tupu, kuanzia wale wahuni wa OPEC mpaka waliopewa vibali kuagiza mafuta TZ,ukiwagusa lazima wakumalize na wana unlimited $$$ ni biashara ambayo imesababisha vifo na majanga makubwa sana kwa binadamu, hata Samia hana uwezo wa kugusa hiyo biashara, makampuni makubwa ya US na waarabu yanatengeneza billions na hakuna wa kunyanyua mdomo hata Biden kimya,lazima warudishe pesa yao maana mlipunguza kutumia mafuta wakati wa COVID mtalipa tuu sasa,
Sasa shida ni hapa kwetu maana kiuhalisia bei ya crude leo imeshuka kuliko miezi mitatu nyuma au kiasi kikubwa iko vile vile ni nini EWURA kuja kusema mafuta duniani yamepanda? yamepanda wapi?
leo brent iko 100$ bei ya juu mafuta mengine yako chini ya dola 100 sasa hawa EWURA watuambia dunia gani hiyo mafuta yamepanda?
Kilichotokea serikali inachukuwa tena kodi iliyojinasibu imesamehe. kwa ufupi kwa hawana pesa na hawataki kuongea ukweli.