Soko la Dunia mafuta yameshuka, Tanzania yamepanda. Nchi hii bora liende

Hujakosea sana ila nataka kidogo kuweka sawa. OPEC hawapangi bei ila wao wanalinda maslahi yao kwa maana wana kiwango cha chini cha bei hawapendi kishuke sababu ndio inakuwa budget yao na wengi ni dola 60$ kwa pipa katika kupanda inakuwa hawaingilii sana soko sababu hata wao hawana akiba kubwa waliyobaki nayo ila ikishuka chini ya 60 huwa wanakata uzalishaji.

Sasa shida ni hapa kwetu maana kiuhalisia bei ya crude leo imeshuka kuliko miezi mitatu nyuma au kiasi kikubwa iko vile vile ni nini EWURA kuja kusema mafuta duniani yamepanda? yamepanda wapi?

leo brent iko 100$ bei ya juu mafuta mengine yako chini ya dola 100 sasa hawa EWURA watuambia dunia gani hiyo mafuta yamepanda?

Kilichotokea serikali inachukuwa tena kodi iliyojinasibu imesamehe. kwa ufupi kwa hawana pesa na hawataki kuongea ukweli.
 
Hi serikali inaenda kufeli vibaya kila siku ma mikopo huku wananchi wanateseka na mfumuko wa bei kila siku vitu vinapanda waliopewa dhamana wanajinuifaisha na Mali za umma hamna lolote wanalofanya kenge hawa
 
Mi nashangaa sana sana watu kutetea huu upuuzi, bei imepanda ya vitu kabla vita haijaanza, mwanzoni 2022 hali ilikuwa mbaya na watu walifungua nyuzi humu za malalamiko kuhusu gharama za maisha kuwa juu, leo hii mtu anakuja kusema eti ni hali ya dunia nzima.

Hakuna mtu kakataa kwa kinachoendelea duniani, lakini uongozi usio makini na kujali maisha ya watu wake umeongezea hali kuwa mbaya zaidi, 60% ni serikali, 40% ni vita inayoendelea.

Tuweke vichwa viwe free, tutoe ushabiki wa Jpm na chuki zisizo na msingi, tuwe neutral, tuache chuki kwa SSH, tuache u team na unafiki, tukiacha vyote hivyo utagundua SSH nchi imemshinda toka mapema, serikalini hali ni mbaya pesa hakuna, hii miradi sijui itakuaje.

Team JPM na Team SSH haisaidii wanaoumia ni ndugu, jamaa na marafiki, babu zako walioko vijijini na wananchi wasio na kipato cha kueleweka.
 
Mtu akipaza sauti gharama za maisha kupanda kuna watu wanaanza siasa, yaani kila jambo siasa siasa siasa, inakera sana.
 
Sasa huko duniani wameshashusha tayari, tatizo lipo Tanzania
 
Kuna kipindi Makamba alienda uarabuni tukaambiwa, waarabu watatuuzia mafuta kwa Bei poa. Kiko wapi ?
Hivi tangu Makamba aingie Kuna unafuu wowote katika Bei ya mafuta au sekta ya nishati?
Sasa wanini kuendelea naye?
 
Watu wa hivyo ni wapuuzi sana, just because it is safe wt them now wanaona wacha mambo yaende hivyo hivyo. Mungu huwalipa hao wanafki, wala haitachukua muda.
 
Watanzania ndio viumbe wazembe zaidi.. Tutapiga kelele mtandaoni,vijiwe vya kahawa, kwenye daladala wiki moja, kisha jii suala limepita.
Wewe umechukua hatua gani kwenye suala kama hili?
 
Inategemea yaliyopo yaliagizwa lini.
 
Umewaza vyema, kabisa nakuunga mkona 100%
Bi mkubwa nchi imemshinda huo ndio ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…