SoC02 Soko la Fedha za Kigeni

SoC02 Soko la Fedha za Kigeni

Stories of Change - 2022 Competition

Germini

New Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Soko la fedha za kigeni linaweza kuwapa fursa nzuri wafanyabiashara katika zote maishani.Inaewezekana kabisa kupata matunda mazuri ya uwekezaji wako na kufanikiwa kugeuza biashara hii katika kazi ya wakati wote (full time job) au kama vitega uchumi vingine tu. Fursa ya kugeuza faida hutokana na mabadiliko au kushuka kwa thamani ya sarafu hivyo mtu yoyote anaweza kujifunza na kushugulika nayo kupitia vifaa vya mtandaoni kama simu,kompyuta au kupitia mshauri mwenye uzoefu zaidi kwani kila kitu huitaji ujuzi ili kukifanya vema.

Ukweli ni kwamba biashara hii kama biashara nyingine hubeba hatari za kifedha( financial risk) na ni muhimu kwa mfanyabiashara kuzifahamu hatari hizi ili kulinda mtaji wake kwa kujifunza njia za kuepuka au kupambana nazo na bila ya ivo hupelekea mmoja kupata hasara za kifedha na kuona biashara hii ya uongo na kitapeli. Kwa kuchukua muda kujifunza na kuelewa jinsi gani masoko yanavofanya kazi na kufahamiana na elimu ya kutosha kuhusu masoko kutaongeza nafasi ya kufanikiwa zaidi katika biashara hii.

Kuna vitabu na rasimali nyingi ambazo zinaweza kumsaidia mfanyabiashara katika kujifunza na kupata uzoefu katika biashara hii.

Soko la kigeni ni jukwaa ambalo sarafu ya nchi moja inaweza kubadilishwa katika sarafu ya nchi nyingine mfano USD kwenda TZS au GBP kwenda JPY.Thamani ya sarafu duniani habdilika kila wakati kutokana na sababu mbalimbali na hasa utulivu wa kiuchumi (economic stability) wa nchi hizo husika na mabadiliko haya ndiyo huleta fursa ya kutengeneza kipato. Pale uchumi wa nchi unapokua imara thamani ya sarafu hupanda vivyo hivyo uchumi unapo dorora thamini nayo hushuka. Hivyo ni muhimu mfanyabiashara kuelewa jinsi gani mabadiliko haya hotokea ili aweze kunufaika.

Soko la kigeni lina ukubwa mpana karibu na karibu fedha yenye thamani ya trillioni 6.6 (USD) huuzwa kila siku na hivyo kulifanya kuwa soko kubwa la fedha kuliko yote duniani. Kati ya kiasi icho asilimia 5.5 huchangiwa na wafanyabiashara wadogo katika soko hili


images.png

kumb:www.investopedia.com

Thamani hii huwakilisha shughuli nyingi ambazo zinahitaji kubadili sarafu. Biashara amabzo huhusisha manunuzi ya nje ya nchi au kuhusisha wanunuzi wa kigeni au wateja na mabenki ya kimataifa yanayohamisha au kushughulika na usambazaji wa fedha duniani huweza kufanya hivyo kupitia masoko haya ya kigeni (forex).

Kama mfanyabiashara wa masoko ya kigeni ni muhimu kuzingatia muda wa kuingia sokoni. Muda sahihi ni pale ambapo kuna kiasi kikubwa cha shughuli ( high transaction volume) au shughuli kubwa za kimasoko na mara nyingi huwa katikati ya wiki au pale masoko yanapoingiliana hivyo kuongeza nafasi za kufanikiwa kuliko kutumia soko moja tu.

Kwa mfanyabiashara mgeni ni muhimu kuwa na wakala( broker) ambae atakupa akaunti yenye nyenzo zote na vifaa vya muhimu ili uweze kuelewa na kufanyia mazoezi mikakati yako ya kifedha ili kuhakikisha mafanikio katika biashara hii.

Vitu vya msingi wakati wa kuchagua wakala ni pamoja na kibali kutoka serikalini ,vigezo na masharti na maoni ya wateja juu ya wakala uyo.Baada ya ufunguzi wa akaunti ni muhimu mfanyabiashara kuzingatia mfumo wake katika soko ambao utamuongoza kuingia au kutoka sokoni kwa kuzingatia usimamizi sahihi wa hatari za kifedha.Ukweli mmoja wapo katika biashara hii ni kwamba hakuna usanidi kamili(perfect setup) au mkakati wa uchawi au uhakika ambao utakupa matokeo sahihi kila wakati.

Wakati nakala na tovuti mbalimbali mtandaoni huchapisha kuhusu usanidi wenye faida ya uhakika ukweli ni kwamba hakuna uhakika wa asilimia zote hivyo basi ni muhimu mfanyabiashara kuhakikisha faida ni kubwa kuliko hasara.

Masoko sio tu harakati za nambari bali ni maonyesho ya nguvu ya asali ya mwanadamu na ya washiriki wa soko hilo na hubadilika kila mara. Kuna wakati mfanyabiashara hujikuta katika upande mbaya wa soko, hichi sio kitu kibaya kwani ni vema kujifunza kutokana na makosa na kuyatumia kuongeza nafasi ya maamuzi yajayo kuwa ya mafanikio zaidi .Hivyo kuelewa biashara hii kwa watu wengi kunaweza kupelekea mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika nchi yetu🇹🇿.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom