Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

asante sana kaka. nitazipitia but ishu ni kwamba maswali yangu huku hakuna wa kuyajibu.
btw ukiwa umenunua hisa ndogo ina maana wewe ndo unakuwa kibaraka wa wenye hisa nyingi??

Sio kibaraka, ktk lugha rahisi tunasema utakula kwa urefu wa kamba yako, kwamba endapo kampuni ambayo umenunua hisa kwayo ikipata faida na kuamua kutoa gawio kwa wanahisa wake, basi kama wewe ni mmoja wao kiwango cha gawio utakachopata kitatokana na ukokotoaji unaotokana na hisa unazomiliki katika kampuni hio, kama ambavyo mchangiaji mmoja ameeleza hapo juu.

All in all biashara ya hisa hapa kwetu bado haina mwamko sana kama ilivo kwa wenzetu nchi zilizoendelea, na ndio maana wenzetu Marekani na Ulaya endapo soko la hisa likiyumba basi inapelekea pia kudorora kwa uchumi zao
 

asante sana kaka mdogo barikiwa.

leo sijamwona ukwelikitugani humu ndani.
 
Last edited by a moderator:

Ninapenda kukupongeza kwa kuuliza swali hili, ambalo kimsingi,limeweka uwanda wa kipekee kwa elimu ya biashara kwenye mtandao wa JF.

Usijione mnyonge,maana umefanya jambo ambalo wengi hawathubutu, japo wangependa.

Namshukuru Munisijo aliyetumia muda wake kuuelimisha umma. Maelezo yake ni ya kitaalam na sahihi.
 


a) Hisa ni nini?

Hisa ni sehemu ya mtaji wa Kampuni inayomilikiwa na mwanahisa, iliyo ndogo kabisa kutegemeana na mtaji wa kampuni husika. Makampuni hugawanya mitaji yao katika vipande yenye thamani sawa. Kila kipande huitwa hisa.

Mfano: Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 10,000, mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni.

Hisa ina sifa zifatazo

• Hisa ina thamani:
Inaweza kuuzwa na kununulika kutegemeana na makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji, au kwa kutegemea bei ya soko kwa makampuni yaliyosajiliwa kwenye Soko la Hisa.

• Hisa inaweza kukua thamani yake, au kupungua thamani yake:
Ikipanda thamani au bei yake, mmiliki wa hisa anapata faida; na ikishuka thamani au bei yake, mmiliki wa hisa anapata hasara.

• Hisa ndizo zinazounda MTAJI wa kampuni:
Kwahiyo, jumla ya hisa za kampuni ukizidisha na bei ya hisa, utapata mtaji wa kampuni ("paid up capital")kwa hisa zilizolipiwa au "Authorised shares capital" kwa hisa zilizoruhusiwa kisheria kulingana na MEMARTS za kampuni).

• Hisa inaweza ikazaa (Bonus shares), na vile vile inaweza ikafa (pale kampuni inapofilisika mtaji):
Hisa inahitaji kulindwa ili isije ikaporomoka thamani yake. Hii ndiyo sababu wanahisa au wamiliki wa hisa inabidi waajiri wataalamu watakaoweza kuiboresha ili izidi kuimarika na kupanda bei yake kila mara. (Yaani kuajiri timu ya menejimenti ya kampuni na kuteua Bodi yenye uelewa na sifa za kuendesha na kusimamia kampuni.

• Hisa inamilikiwa kisheria kama sehemu ya mali anayoweza kuwa nayo mtu yeyote kihalali.
Mtu anaponunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni.

b) Naweza kuzimiliki kivipi?? ni kimaanisha umri, na kiasi na wapi?? kwa masharti gani??
Unaweza kumili hisa kwa kuzinunua kupitia masoko ya fedha na mitaji.
Mtu yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 anaweza kununua hisa. Wazazi au walezi pia wanaweza kununua hisa kwa niaba ya watoto wao.
Unaweza kununua kiasi chochote cha hisa kulingana na uwezo wako kifedha. Unaweza kununua kuanzia hisa 100.

c) Nitapata faida gani kwenye umiliki wa hizo hisa??
Faida ya kuwekeza kwenye hisa ni:
• Kwa ujumla dhamana za fedha (hisa na hatifungani) ni rasilimali ambazo zinagawanyika kwa urahisi. Kutokana na urahisi huo, dhamana zinaweza kuwekwa rehani kwa ajili ya kupata mkopo kutoka taasisi za fedha.
• Wawekezaji kwenye hisa wanapata gawio ikiwa kampuni imetengeneza faida.
• Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa.
Ongezeko la thamani ni tofauti ya bei ya kununulia hisa na bei ya kuuzia. Ikiwa bei ya kuuza ni ndogo kuliko bei ya kununulia, mwanahisa anapata hasara.

d) Je nitapataje gawiwo langu kwenye umiliki wa hisa?

• Ni juu ya mwekezaji kuwasiliana na kampuni aliyowekeza na kutoa habari muhimu kama vile anwani ya posta pamoja na akaunti ya benki.

• Kama malipo yatalipwa kwa kupitia njia ya posta basi utapata Hawala ya Posta kupitia anwani yako, na kama malipo yanafanyika kupitia kwenye akaunti ya benki basi utapata hundi au pesa zitaingizwa kwenye akaunti yako.

• Ni muhimu kutoa taarifa iwapo anwani au akaunti yako itabadilika. Kampuni nyingi zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa zinatoa gawio mara mbili kwa mwaka.

e) Hasara zipatikanazo kwa ununuzi wa hisa.
- Uwekezaji kwenye hisa hauna uhakika wa gawio kwa sababu gawio linategemea faida ya kampuni.
- Bei ya hisa sokoni inaweza kushuka na hivyo mwanahisa akapata hasara endapo ataziuza hisa zake kwa bei ya chini kuliko bei aliyonunulia.

f) Nitaijuaje bei ya hisa ama kuna hisa zinauzwa?

Utajua bei ya hisa kwa kufuatilia taarifa za vyombo vya habari kama magazeti (yanayochapisha habari za uchumi), televisheni na hata kwa kuuliza madali wa Soko la Hisa la DSM na washauri wa masuala ya uwekezaji (investment advisors).

g) Kwa maisha ya kitanzania is this bussiness valid and does it pay??
Yes, the business is valid ("viable" if you meant that) and it pays if you have invested in profit making companies the like of TBL, TCCL, Twiga and Tanga Cements etc.
 
dah! mwaJ ibarikiwe siku ulipojiunga jf mweeeh!

mbona ntakusumbua sana sasa?? nataka niingie kwenye hii biashara.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin
vilevile naomba niongezee maana wadau wamejb maswali karibia yote kwa ufasaha,lazima uwe macho na mfuatiliaji wa taarifa za soko la hisa hasa wakati kampuni inapofungua mwaka au kipindi cha biashara (start of financial year)na kuanza kuuza hisa zake na wakati wa kufunga mahesabu (end of financial year)

mfano wanaanza kufungua biashara mwezi wa1, mara nyingi bei ya hisa inakua chini mfano wanauza kwa sh100 na inapofika mwezi wa6 unakuta biashara imechanganya ,yani kampuni imepata faida na hisa zinapanda thamani kufika sh 600, kwa makampuni mengine unaweza kukuta faida inaanza kushuka kutokana na sababu mbalimbali ila mojawapo kubwa ni kudorora kwa biashara zao na wanaanza kufanya matumizi kuliko kuingiza kipato, kadri matumizi yatakavyoongezeka kuliko mapato ndivyo faida au thamani ya hisa inavyoshuka

ukiona kitu kama hicho nakushauri ufanye maamuzi ya kuuza hisa zako kabla haujapata hasara, mfano thamani ya hisa zimeshuka kutoka sh600 mpaka sh400 na ukichunguza mwenendo wa kampuni hawaonyeshi dalili ya kupata mauzo zaidi, huo ni wkati muafaka wa kuuza hisa zako ili usipate hasara bali ufaidi faida yako ya sh 300 kutokana na uwekezaji wako wa sh 100
mi napendelea kuuza wakati napojua thamani ya hisa ipo kwenye maturity stage na kwenda kununua kwenye kampuni nyingine ambayo najua wapo kwenye growth stage
 
Kw ushauri wangu kanunue hisa za vinywaji kama bia keani mara ya mwisho ilikuwa 1800 saiv nimecheki ni around 2000 na bia zina panda bei kila siku. TCC

UKIENDA DSE hawata kuzia hisa indtead uta ambiwauendw kwamabroker wako jengo hilo hilo
 
Oooh naona hii mambo ilinipita,
ok tuanze na kusema kuhusui kuinvest kwa watu ama kikindi cha watu.its very risk kama wewe sio parttaker ktk day to day activities na hakuna chombo chochote cha kuregulate, nilishapigwa pesa nyingi kwa namna hiyo.

Kununua share nunua kwa kampuni ambayo ni audited na imesajiliwa na DSE ambapo huwa ni lazima wawe audited 3 years before kabla ya kuwa registered dse.uzuri wa kuinvest kwa kampuni ambazo zipo listed DSE ni kuwa zipo wazi ktk mapato na matumizi tofauti na ambayo sio listed wanaweza kucheat.

Swali la pili kuinvest ktk vishughuli vidogovidogo je utaweza kusimamia ama utakaa kuona pesa yako ikiisha hvhv tu, matajiri wengi huweka pesa zao ktk kampuni ambapo huwa wanaangalia
1.management
2.audited
3.iwe profitable in long run
suala la msingoi kabla huijainvest pesa yako popote hakikisha unapata knowledge zaidi.

Ukiwa na large cash, reinvest ktk biashara iliyokupatia hiyo pesa.



 
Last edited by a moderator:
Also cha msingi na muhimu before investing ktk shares, jifunze kusoma financial statement ya kampuni ambapo huwa zinatolewa after every quarter.

ili ujue mapato na matumizi ilipotoka na inapoenda then utapata picha halisi also uangalie na competitors anafanya nini.
 
Ni makampuni 17 tu yako registered Dar Stock Exchange! Mbaya zaidi hakuna hata kampuni moja ya simu kuanzia TTCL na mengineyo.

KUna siri inafichwa hapa. Wabunge wetu jamani mlivalie njuga hili.
 

kweli mkuu yaan hata mvuto haina,information chache
 
Wanabodi,
Wale wenye acess na ITV, watch live jinsi Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Bw. Magabe Maasa akifafanua fursa za Watanzania kugeuka, mamilionea na mabilionea overningt kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Fuatana nami.

Karibu.

Pasco
 
DSE waanzisha Soko la Kukuza Ujasiliamali, (Enterprize Growth Market-EGM).

ili kuwawezesha wajasiliamali wadogo na wa kati (SME's), wanaruhusiwa kujisajili soko la hisa la Dar es Salaam ili kuuza hisa na kupata mitaji!.
 
DSE waanzisha Soko la Kukuza Ujasiliamali, (Enterprize Growth Market-EGM). ili kuwawezesha wajasiliamali wadogo na wa kati (SME's), wanaruhusiwa kujisajili soko la hisa la Dar es Salaam ili kuuza hisa na kupata mitaji!.
Hii nimeipenda, je hao SME's wanapaswa kujiunga kwanza na kituo cha uwekezaji kama vile TIC au vinginevyo?
 
Bwana Magabe, anafafanua kuwa lengo la kufungua soko hilo dogo lenye masharti nafuu, ili Watanzania wengi zaidi wenye vipato vidogo na vya kati, waweza kupata fursa za kutajirika kupitia soko la hisa la Dar es Salaam.
 
Amesema jinsi ya kampuni kujiunga na soko hilo la EGM, wamelegeza masharti ya kujiunga, ambapo hapo zamani, ili kampuni isajiliwe, ilipaswa kwanza iwe imefanya biashara kwa zaidi ya miaka 5!, pili lazima kampuni ionyeshe kuwa imekuwa ikitengeneza faida.

Kujiunga na EGM hakuna sharti la muda, au kutengeneza faida, yaani kampuni unaweza kuianzisha leo, na leo leo ukaisajili soko la hisa la Dar es Salaam, na kuuza hisa, unapata mtaji, unafanya biashara!. Hivyo lile sharti la kuonyesha faida au la kuwa lazima kwanza uwe ulifanya biashara halipo!.

Yaani uinaanzisha biashara leo, unajisajili DSE leo, unauza shares leo, unapata mtaji leo, ndipo unaanza biashara kesho!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…