Soko la Hisa la Marekani litufumbue kitu Waafrika

Soko la Hisa la Marekani litufumbue kitu Waafrika

Joined
Jul 11, 2020
Posts
66
Reaction score
145
Soko la Hisa la Marekani na baadhi ya nchi zilizoendelea yako very flexible kiasi ambacho kampuni kushuka au kuongezeka net worth ndani ya masaa ni jambo la kawaida sana.

Chukulia mfano Corona ilivyoweza kufanya makampuni kama zoom kuinuka kwa kasi na hisa zake kupanda chati kwa kasi, au hivi karibuni tumeona namna ambavyo Elon Musk amepanda kwa siku moja.

Sensitivity hii ya Hisa ni moja kati ya kitu muhimu sana kwenye implementation ya Monetary Policy, lakini kwetu naona kuna shida nyingi sana, kwa mfano hisa za tz zimebaki kuwa na bei za kawaida.

Wakati huohuo CMSA inakiri kuwa na washiriki wachache huku tukiwa hatuoni juhudi za makusudi za CMSA kuhakikisha soko linachangamka na kuwa kama Marekani au kama Afrika Kusini tukizungumzia masoko yaliyochangamka kwa Afrika.

DSE wameanzisha hisa kiganjani ili watu waweze kutrade kama forex lakini marketing yao imekuwa mbovu huku products zikiwa limited, by the way yako mengi ya kujifunza kwenye soko la Hisa la Marekani na nchi nyingine zilizoendelea ikiwa tunataka Benki Kuu iwe na uwezo mkubwa wa ku-regulate uchumi.

Naenda Kusolve some more Mathematical Equations.
 
Vijana wanataka pesa ya chap chap hisa ni Long term investing labda utumie leverage products kama fx,Indice,Metals zina quickly return ipoo ila unatakiwa ujue namna ya kutrade profitable na risk management.
 
Chief sie bado Sana kwenye mambo hisa, hta mwamko wa wananchi bado upo chini saña

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Hapa kwetu makampuni yenyewe yanakatisha tamaa wawekezaji wa hisa,mfano ni Hawa Vodacom mwaka huu wameamua kutotoa gawio kwa wateja wao kwa kisingizio kwamba eti hawakupata faida,wakati ambapo mitandao yao ya simu na internet iko busy 24/7 .
 
Kwa ulicho adika hapa kwa mimi nisiyejua chochote nimeliona kama ni soko la giza maana kama nawekeza sehemu na sijui kupanda na kushuka kwa thamani ya hisa zangu kwa uwazi inaonyesha wazi kuwa makampuni yaweza kupika data ili tu yasitoe gawio kwa wenye hisa na wasilindwe
 
Makampuni ya bongo janja janja nyingi..mfano Nilikuwa nafuatilia mwenendo wa kampuni ya flan ambayo iko listed DSE lakini wao kila mwaka toka 2018 ni wanarecord loss tu.but kuna mdau akaniambia ni mbinu yao hiyo ili wasitoe gawio kwa wana hisa wao.
 
Kwa ulicho adika hapa kwa mimi nisiyejua chochote nimeliona kama ni soko la giza maana kama nawekeza sehemu na sijui kupanda na kushuka kwa thamani ya hisa zangu kwa uwazi inaonyesha wazi kuwa makampuni yaweza kupika data ili tu yasitoe gawio kwa wenye hisa na wasilindwe
Hilo linawezekana kabisa changa la macho likapitishwa.
 
Vijana wanataka pesa ya chap chap hisa ni Long term investing labda utumie leverage products kama fx,Indice,Metals zina quickly return ipoo ila unatakiwa ujue namna ya kutrade profitable na risk management.
Sijui unachoongelea hapa ni nini? Yani naona mauzauza tu. Ila mimi nachoamini ni kufanya kazi na uzalishaji mali hizi lugha zenu mnazonena Aisee.

Bora mkono kinywani.
 
Sijui unachoongelea hapa ni nini? Yani naona mauzauza tu. Ila mimi nachoamini ni kufanya kazi na uzalishaji mali hizi lugha zenu mnazonena Aisee.

Bora mkono kinywani.
Copenhagen tafuta na maarifa mapya wewe maisha umeona ni kubeba boksi tu..dunia inabadilika isije ikatokea unarudi bongo siku moja huku kichwani upo mweupe huelewi kitu kuhusu dunia inaendaje...itakuwa hakuna faida sasa kwako wewe kukaa Ulaya
 
Nimecheka Aisee tadpole
 
Back
Top Bottom