JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Hali ya soko la Kijichi lililopo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambalo lilijengwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Soko la Kijichi lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambalo lilijengwa kwa gharama kubwa lipo tupu na halitumiki.
Soko hilo lilijengwa kupitia mradi wa uboreshaji wa Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam (DMDP) kwa mkopo wa Benki ya Dunia (WB), ulizinduliwa Septemba 2019 ukihusisha uwepo wa miundombinu mbalimbali ikiwemo jengo kubwa la ghorofa ambalo lilikusudiwa kutumiwa kama ofisi na huduma mbalimbali zinazoenda sambamba maendeleo ya soko hilo.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la Jumatano, Agosti 21, 2019 lilieleza kuwa Mkopo huo wa Benki ya Dunia ulitumika kugharamia miradi ya soko hilo na mengine mawili ya Mbagala na Mkangarawe kwa thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.
Mradi huo ambao umetumia mamilioni ya shilingi, matarajio yaliyokuwepo yameyeyuka, soko lipo tupu na hakuna jambo lolote linaendelea ndani ya soko hilo.
Hata hivyo hali hiyo haikudumu zaidi ya miezi miwili, ambapo Watu wa mabasi walilalamika kisha kurejea eneo la Mbagala kama ilivyokuwa awali kabla ya kuhamishiwa Kijichi.
Inaelezwa kuwa baadhi ya viongozi hususani ngazi ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wamekuwa wakitembelea mradi huo, lakini hakuna kinachoendelea soko limebakia wazi bila kuingiza chochote chenye tija kwa Serikali hata kwa wananchi kama ilivyotarajiwa.
Inaelezwa na wakazi kwamba Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais, alifanya ziara kwenye mradi huo wa soko la Kijichi, ambapo alionesha kushangazwa na mradi huo kuwekwa kwenye eneo hilo, akisimamia hoja kwamba eneo limejitenga na jamii na akashauri daladala zinazoenda Kijichi zifike hadi sokoni ili angalau kuchochea mzunguko wa biashara.
Kulingana na mandhari iliyopo katikati eneo la karibu linalozunguka mradi huo, umezungukwa na makazi hasa ya watu wenye uwezo kiuchumi huku makazi mengi ya eneo hilo yakionekana kwa wingi yakiwa ndani ya fensi.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao awali walikuwa kwenye soko hilo wanadai watu wengi ambao wanazunguka eneo hilo walikuwa hawalitegemei zaidi kupata huduma.
Pia kuwategemea wanunuzi wengine ilikuwa jambo gumu kutokana na mwelekeo lilipo soko hilo, hali ambayo ilikuwa ikipelekea bidhaa zao mara kwa mara kuoza na kuwasababishia hasara kwenye mitaji yao ambayo walikuwa wamewekeza.
Kutokana na hali hiyo ilivyo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, hivi mamlaka husika zinafikira nini kuhusu mradi huo, ikizingatiwa pesa zilizotumika kufanikisha uwepo wa mradi huo ni za mkopo ambazo zinatakiwa kurejeshewa.
Hivi mwelekeo wa Mradi huo ni nini? Serikali imeamua kuuacha ufe, kama ni mkopo, fedha za kulipa madeni zinatoka wapi au ni kwenue miradi mingine ambapo walipa kodi wanakatwa fedha zao na kulipia mradi ambao umetelekezwa?
Majibu ya Serikali kuhusu Soko la Kijichi ~ Serikali yafikiria kubadili matumizi ya Miundombinu iliyojengwa kwaajili ya Soko la Kijichi (Temeke)