Una kuku idadi gani? Unaweza kujaza lori moja zima? Kama huwezi ni afadhali ukaanza kwa kuwauzia wachuuzi wanaochukua kuku mikoani kuleta Dar? Nina imani italipa hata kama faida haitakuwa kubwa sana. Pole pole utajifunza masoko yalipo kutoka kwa hao hao wateja wako. Ukiwa na taarifa za kutosha ndiyo unaweza kuamua kama italipa kuleta mwenyewe Dar. Vinginevyo funga safari njoo Dar zungukia masoko ongea na wahusika ili uweze kufanya uamuzi sahihi. Soko lipo ila linahitaji mbinu ya kuliingia.Wadau habari!kwa wale ndugu zangu wenye uzoefu na soko la kuku wakienyeji katika masoko ya Dsm hasa Shekilango,Manzese,Tabata na Kisutu,naomba wanijuze kama kuna uwezekano wa kupata soko la kuuza kuku hao wa kienyeji katika masoko hayo,kama uwezekano upo je ni njia gani stahiki naweza tumia kuwapata wahusika stahiki kwa maana ya wanunuzi katika masoko hayo!!mimi nipo Mkoani na nilikua nataka kuanza kuuza kuku hao Dsm!asanteni sana!
Na mimi Milo mkoani ninakuku hao wa kienyej em tusubirie watchman wake watujuze!!
Wakienyeji aina gani? Chotara au pure kienyeji? Uko mkoa gani?Hawa nacte hata mm siwaelewi kabisa.
Wadau habari!kwa wale ndugu zangu wenye uzoefu na soko la kuku wakienyeji katika masoko ya Dsm hasa Shekilango,Manzese,Tabata na Kisutu,
Naomba wanijuze kama kuna uwezekano wa kupata soko la kuuza kuku hao wa kienyeji katika masoko hayo,kama uwezekano upo je ni njia gani stahiki naweza tumia kuwapata wahusika stahiki kwa maana ya wanunuzi katika masoko hayo!!
Mimi nipo Mkoani na nilikua nataka kuanza kuuza kuku hao Dsm!
Asanteni sana!