Soko la kuku wa kienyeji

Soko la kuku wa kienyeji

Asha Mahd

Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Natumaini wote wazima,mimi ni muuzaji wa kuku wa kienyeji toka Singida na Dodoma na naifanyia biashara hiyo Dodoma kwa sasa. Natamani biashara yangu niilete Dar Es Salaam na tatizo sina soko. Wadau naombeni maoni/ushauri na maelekezo.
Thanks
 
Natumaini wote wazima,mimi ni muuzaji wa kuku wa kienyeji toka singida na dodoma na naifanyia biashara hiyo dodoma kwa sasa.natamani biashara yangu niilete Dar Es Salaam na tatizo sina soko.wadau naombeni maoni/ushauri na maelekezo.
Thanks
Je unaweza ku-supply kuku wangapi kwa mwezi? Maana kila siku watu wanaomba tender za ku-supply vitu, wakipata kazi, baada ya siku moja mzigo hana, inakuwa kasheshe tena kuanza kuokoteza.
 
Pole aiseeee.unahitaji?

Mimi nahitaji matetea wanaotarajia kuanza kutaga wasiopungua 100 mpaka 200 mwezi january 2015, je mpaka kufika Dar utaniuzia shilingi ngapi?

Na mwezi wa tatu nitaongeza wengine wanaotarajia kuanza kutaga 100 mpaka 200. Ni matetea tu,sio majogoo.
 
dada, wale wajapani wanaouza magari kwn mtandao wangekuwa wanasema tuwapigie ili tupate bei wasingeuza. weka bei hapa watu wapime wakutafute.ni ushauri tu
 
Mimi nauza vifaranga vyeusi kutoka malawi kama unahitaji naomba pm, vifaranga hivi ni chotara ni resistant to disease na wanataga sana mayai
 
safi dada. jitahidi soko lako ulenge kwn migahawa na bar kubwa hasa za uswahilini ndio kuna wateja wengi. hapo kuku 50-200 kwa mwezi bado ni kidogo sana kwa soko la dar. nakushauri kwa kuwa unalenga biashara, usiwaache wakakua sana kwani watu wa mahotel wanataka wadogo. hata ungeuza wa size ya kilo moja tu kwa elf kumi unauza fastafasta. just ushauri
 
50 - 200 kwa mwezi inatosha na kama ukapata soko na utaongeza kulingana,na mahitaji ya soko
Nakutakia mafanikio mema
 
Mimi nauza vifaranga vyeusi kutoka malawi kama unahitaji naomba pm, vifaranga hivi ni chotara ni resistant to disease na wanataga sana mayai

Toa elimu zaidi, wanahudumiwa kama kuku wa kisasa au kuku wa asili, n bei yako ikoje?
 
Toa elimu zaidi, wanahudumiwa kama kuku wa kisasa au kuku wa asili, n bei yako ikoje?
uamuzi ni wako kama ukihitaji uwafuge kama wa kienyeji inategemea space uliyonayo na idadi unayohitaji. Pi Unaweza kuwafuga kama wa kisasa na ukawalisha kama wa kisasa. kifaranga kimoja nauza 2200. Nipo songea natarajia kuweka mayai kwenye incubator tarehe 5 na vitatoka by 26 december kama unahitaji weka oda.
 
Back
Top Bottom