Ushakosea step ya kwanza ya mradi, umefanya uzalishaji na hujui soko. Mwanza siijui so nakupa back up plan endapo umekosa hili unalotafuta, inahitaji muda ila ni endelevu.
Uza kuku kadhaa tafuta vifaa kama jiko, ndoo, sahani, vikombe, chupa ya chai. Bakiza mtaji kidogo wa kuanzia kununua maziwa, ndizi, mihogo, tangawizi, kahawa, mafuta ya kupikia na mkaa.
Tafuta location yenye watu wengi wanaopita hasa intersections pembeni ya vibarani preferably kuwe na baa za karibu. Tafuta mama mpe kila kitu kazi yake kukaanga na kuuza hivyo nilivyotaja. Siwezi kukupa estimations atauza kuku wangapi kwa siku ila kila siku atauza.
Sasa multiply hicho unachofanya kwa mama mmoja kifanye kwa mama kadhaa kadri unavyoweza. Hakuna haja ya kibanda wala kibari. Unaweza uza kuku kadhaa kwa siku na wengine ukauza kwa kwa njia unayotafuta hapa.
Chukua ushauri huu kama wewe ni mjasiriliamali, kilimo na ufugaji usipojumlisha na ujasiriamali utatia huruma endapo soko la awali litafeli.
Angalizo: Kitu chochote huwa ni chepesi kwenye maandishi, sio kwenye utekelezaji.