Habari zenu wakuu, mimi nimemaliza chuo mwaka huu nimeona mtaani kugumu kwa kweli, kwa kuwa kuna babu yngu mmoja ni mzoefu sana katika masuaala ya biashara nilikaa nae chini kuona nini nitafanya. hapo ndipo aliponipa ushauri wa kuanzisha biashara ya kukamua mafuta ya alizeti na kuuza, bahatai nzuri mashine anazo na amenipa go ahead, kwa maana hiyo nimeungana na wenzangu ambao tumemaliza chuo pamoja na kufikiria kuanza kufanya hiyo biashara. nimekuja humu wakuu mnisaidie kujua soko likoje hasa tunapokamua wenyewe katika mkoa wa dar es salaam na maeneo yake jirani. naomba kuwasilisha.